Papa Francisko amepokea heri za Pasaka kutoka kwa Rais wa Italia
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, tarehe 9 Aprili 2023 katika siku kuu ya Pasaka amemwelekeza Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wake kwa kumtakia heri ya Pasaka akiandika kuwa: “ kwa kukabiliwa na kuendelea kwa uchokozi wa kikatili wa Urussi dhidi ya Ukraine na hali ya mzozo inayokumba maeneo mbalimbali ya duniani, maombi yako ya mara kwa mara ya maelewano kati ya watu yanamtaka kila mtu kuanzia wale walio na majukumu ya serikali kwa madai ya dhamana hiyo ya udugu kwamba inatuelekeza kwenye mazungumzo na kuelewana”. Ni katika muktadha huu wa siku kuu kubwa ya ukombozi wa ulimwengu kupitia mwana wake Yesu Kristo.
Rais wa Italia anatoa hata tafakari kuhusu Pacem in Terris.
Kiongozi wa Jamhuri ya Italia ameandika kwamba“Pasaka Takatifu inanipa fursa nzuri sana ya kukutakia wewe Baba Mtakatiu matashi mema ya dhati ya Jamhuri ya Italia na yale yangu ya kibinafsi”, na amenukuu katika Waraka wa Pacem in Terris, ambao waraka wa Mtakatifu Yohane XXIII unaotimiza maiaka 60 tangu kuchapishwa kwake mnamo tarehe 11 Aprili huko akitarajia tafakari ya kina zaidi juu ya ujumbe wake kuhusu “amani kati ya watu wote iliyojengwa juu ya ukweli, haki, upendo, uhuru. Kwa hakika, zaidi ya hapo awali, mchango wa wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema ni muhimu katika utekelezaji wa manufaa ya wote, ili kutoa jibu kwa hamu ya amani inayohisiwa na ubinadamu, amesisitiza Bwana Mattarella katika ujumbe wake”
Heri ya siku kuu ya somo wake
Ujumbe wa Rais wa Italia unahitimishwa kwa matashi ya dhati na ya upendo kwa Pasaka, pamoja na pongezi za dhati kwa maadhimisho yajayo ya Mtakatifu George kwa hiyo wa somo wa Papa Francisko, yaani Jorge Mario Bergoglio, ambayo itaadhimishwa tarehe 23 Aprili ijayo.