Papa Francisko akiwa anainga kwenye ndege kuelekea Budapet Hungaria Papa Francisko akiwa anainga kwenye ndege kuelekea Budapet Hungaria  (ANSA)

Papa Francisko ameondoka kuelekea Hungaria:Kujenga madaraja kati ya watu

Katika ziara ya 41 ya kitume ya Papa ambayo imeanza,ameondoka kutoka uwanja wa ndege wa Fiumicino saa 2.21 kuelekea Budapest.Papa atakaa katika mji mkuu wa Hungari hadi 30 Aprili.Kabla ya kuondoka Nyumba ya Mtakatifu Marta,alikutana na watu 15 wasio na makazi ambao wanaishi karibu na Mtakatiu Petro.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa kuongozwa na kauli mbiu: "Kristo ni maisha yetu ya baadaye", Papa Francisko Ijumaa tarehe 28 Aprili 2023 amendoka  saa 2.21 asubuhi kutoka katika uwanja wa  ndege wa Kimataifa  Fiumincino, Roma kuelekea Hungaria, ambapo atakaa huko hadi tarehe 30 Aprili 2923. Ni katika ziara yake ya 41 ya kitume, ambayo Papa alimkabidhi Bikira katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu siku mbili zilizopita katika muktadha wa kwenda huko Budapest nchini Hungaria.

Papa akiingia kwenye ndege iliyompelekea Hungaria
Papa akiingia kwenye ndege iliyompelekea Hungaria

Kabla ya kuondoka katika nyumba ya Mtakatifu  Marta, mjini Vatican kama kawaida Baba Mtakatifu alipokea salamu za watu kumi na watano wasio na makazi wanaoishi karibu na Mtakatifu Petro, wakisindikizwa na Mwenhekiti wa Baraza la Kipapa la huduma ya upendo  Kardinali Konrad Krajewski. Baba Mtakatifu Francisko anarudi nchini huko miaka miwili baada ya Kongamano la Kimataifa la Ekaristi Takatifu na baada ya Ziara ya Papa Yohane Paulo II  mnamo  mwaka wa 1991 na 1996, kwa hiyo anakuwa Papa wa pili kwenda katika taifa la Hungaria.

Safari  inayotualika kuponya mateso yaliyosababishwa Ukraine

Kama kawaida, baada ya kuondoka, Papa alituma salamu zake kwa Rais wa Jamhuri ya Italia Sergio Mattarella. Katika telegramu, yake Papa Francisko anaandika kwamba anafika Hungaria "akisukumwa na hamu ya kukutana na ndugu katika imani na kutoa ushuhuda wa umuhimu wa kujenga madaraja kati ya watu". Kwa upande wake Rais Mattarella, katika ujumbe uliotumwa kwa Papa, anaandika kwamba: "safari yake ya kitume kwa nchi ambayo ni chimbuko la mapokeo ya Kikristo ya kale, karibu sana na mahali ambapo ghasia zisizoelezeka za Kirusi dhidi ya watu wa Kiukraine zinafanyika, bado zinaalika mara moja kutafakari juu ya haja kamili ya kurejesha utaratibu wa kimataifa uliokiukwa kikatili na kuponya mateso makubwa yaliyosababishwa na uchokozi dhidi ya Ukraine". Mkuu wa nchi ya Italia  anahitimisha ujumbe wake kwa kusema kwamba ana uhakika kwamba ushuhuda wa Papa "utawahimiza watu wa huku kufuata njia za udugu na kukubalika".

28 April 2023, 09:14