Tafuta

2023.04.30:Papa Francisko kama kawaida yake, mara baada ya kutoka ziara ya kitume huko Hungaria amesali mbele ya picha ya Salus populi romani,. 2023.04.30:Papa Francisko kama kawaida yake, mara baada ya kutoka ziara ya kitume huko Hungaria amesali mbele ya picha ya Salus populi romani,. 

Papa baada ya kufika ameshukuru kwa Bikira Maria Mkuu

Papa baada ya kurudi kutoka Hungaria,kama kawaida ya kila Ziara yake ya Kitume,alikwenda moja kwa moja kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kwa kukaa kitambo kwa sala mbele ya Picha ya Bikira Salus Populi Romani.Baadaye alirudi mjini Vatican.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Dominika jioni tarehe 30 Aprili 2023, alitua katika Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Fiumicino, Roma, majira ya saa 1.25 usiku, akiwa anarejea kutoka ziara yake ya 41 ya kitume jijini Budapest nchini Hungaria, iliyoanza Ijumaa tarehe 28 Aprili 2023. Kwa hiyo kama alivyofanya kabla ya kuondoka, ambavyo pia ni kawaida yake mwishoni mwa kila ziara, Baba Mtakatifu Francisko alikwenda kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, Roma  ili  kumshukuru Bikira kwa ajili mafanikio ya siku tatu za ziara hiyo ambazo zimemwona akifanya mikutano mbalimbali huko Budapest. Ni taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican. Katika taarifa hiyo inabainisha kwamba, Baba Mtakatifu alitulia katika maombi kwa dakika chache mbele ya picha ya  Bikira ‘Salus Populi Romani’, yaani Afya ya Watu wa Roma. Hifuatayo ni video fupi inayoelezea ziara hii ya Papa Francisko katika siku ya mwisho wa siku tatu za kina katika nchi ya Hungaria aliyoanza tarehe 28 hadi 30 Aprili 2023.

Ziara ya kitume nchini Hungaria: siku yake ya mwisho

Ikumbukwe, katika ziara yake ya 41 ya kitume, Baba Mtakatifu alipowasili katika uwanja ndege wa kimataifa wa Budapest 28 Aprili, alipokelewa na Balozi wa Vatican; baadaye kulikuwa na wakati wa kukaribishwa rasmi katika uwanja wa Jumba la ‘Sándor’,(yaani Ikulu) ambayo ni makazi ya rais wa Hungaria, Bi Katalin Éva Novák. Kulifuatia mikutano ya itifaki kuanzia na  mkuu wa nchi, Waziri Mkuu Viktor Orban na mamlaka na wawakilishi wa mashirika ya kiraia na mashirika ya kidiplomasia. Siku hiyo ilifungwa saa kumi na moja jioni ambapo Papa alikutana na wakleri, watawa na waseminari katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano.

Ziara ya Papa nchini Hungaria
Ziara ya Papa nchini Hungaria

Jumamosi tarehe 29 Aprili alifanya ziara ya kibinafsi  ya faragha  kwa watoto vipofu ambao ni wageni wa taasisi ya Mwenyeheri László Batthyány-Strattmann  iliyopewa jina la daktari wa macho wa Hungaria wakati wa kutangazwa mwenyeheri mnamo mwaka 2003,  ikifuatiwa na mkutano na maskini na wakimbizi katika Kanisa la Mtakatifu Elizabeth wa Hungaria. Baada ya hapo alitembelea Jumuiya ya Kikatoliki -kigiriki. Mikutano mingine alasili,  ilikuwa ni mkutano na vijana katika Uwanja mkubwa wa mchezo liitwalo  László Papp Budapest na saa 12.00 jioni katika Ubalozi wa Vatican nchini humo, alifanya mkutano wa faragha na wanashrika wa  Shirika Kijesuit. Lakini pia Papa alikutana na kiongozi wa Kiorthodox, Hilarion.

Ziara ya Papa
Ziara ya Papa

Dominika tarehe 30 Aprili 2023  ameadhimisha  Misa Takatifu, katika Uwanja wa Kossuth Lajos jijini Budapest na baada ya misa alitoa wito na Sala ya Malkia wa Mbingu,  na  hatimaye mkutano alasiri ulikuwa ni mktano wa ulimwengu wa chuo kikuu na utamaduni kabla ya kuondoka kurudi Vatican. 

Hotuba ya Papa
Hotuba ya Papa

 

30 April 2023, 21:00