Tafuta

Mji wa Vatican. Uwanja wa Mtakatifu Petro. Mji wa Vatican. Uwanja wa Mtakatifu Petro. 

Papa ameshiriki Mkutano wa kwanza na Baraza la Makardinali washauri

Mkutano wa kwanza wa Makardinali washauri wa Papa aliopyaisha baada ya kuwaunda mnamo 2013 ili kumsaidia katika uongozi wa Kanisa la Ulimwengu na kwa ajili ya mageuzi ya Curia Romana, ambapo Katiba ya kitume Praedicate Evangelium imeundwa 2022.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mkutano umeanza tarehe 24 Aprili 2024 kwa uwepo wa Papa Francisko, katika Baraza la Makardinali. Huu ni mkutano wa kwanza wa  Makardinali tisa (C9) washauri wa Papa  baada ya upyaisho wa kiungo hicho kwa upande wa Papa mnamo tarehe 7 Machi iliyopita. Wajumbe wa Baraza jipya la makardinali ni Pietro Parolin, Katibu wa Vatican,  Fernando Vérgez Alzaga, Rais wa Serikali ya Mji wa Vatican; presidente del;Fridolin Ambongo Besungu, Askofu Mkuu wa  Kinshasa; Oswald Gracias, Askofu Mkuu wa  Bombay; Seán Patrick O'Malley, Askofu Mkuu wa  Boston; Juan José Omella Omella, Askofu Mkuu wa  Barcellona; Gérald Lacroix, Askofu Mkuu wa  Québec; Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa  Lussemburg; Sérgio da Rocha, Askofu Mkuu wa Mtakatifu  Salvador de Bahia. Katibu wa Kamati ni Askofu Marco Mellino, wa  Cresima.

Baraza la Makardinali washauri 9  lilianzishwa na Papa Franciko na barua ya mkono wake mnamo tarehe 28 Septemba 2013 kwa ajili ya  shughuli ya kumsaidia katika kuliongoza Kanisa la Ulimwengu na kujifunza mpango wa kusasisha katiba ya Curia Romana,  ambayo hatimaye imeweza kutolewa katiba mpya ya kitume ‘Praedicate Evangelium’ iliyochapishwa mnamo tarehe 19 Machi 2022. Mkutano wa kwanza wa makardinali (C9) ulifanyika mnamo Mosi Oktoba 2013 Na wakati huo huo mkutano wa mwisho ulifanyika mnamo Desemba 2022 ambao ulikuwa umejikita na mada ya hatua ya kibara ya mchakato wa  Sinodi, iliyohitimishwa hivi karibuni, katika maandlizi ya Instrumentum laborius kwa ajili ya mkutano wa XVI wa Kawaida wa Sinodi, mnamo Oktoba ijayo.

MKUTANO WA MAKARDINALI 9 WASHAURI WA PAPA (C9)
24 April 2023, 15:35