Tafuta

Bado nchini Ukraine inazidi kulipuliwa kila kukicha. Bado nchini Ukraine inazidi kulipuliwa kila kukicha.  (ANSA)

Papa amerudia wito wake kuombea amani duniani hasa Ukraine

Katika salamu zake mara baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu,Papa amepyaisha wito wa kuombea amani nchini Ukraine.Wakati huohuo,baada ya usiku milipuko ya makombora ilisikika katika maeneo mbalimbali ya nchi.Amekumbusha kumbu kumbu ya Belfast nchini Ireland Kaskazini.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mara baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu, Jumatatu ya Pasaka tarehe 10 Aprili 2023, kwa waamini waliunganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu amekumbusha kuwamba: “Leo ni kumbukumbu ya miaka 25 ya kile kilichoitwa 'Makataba wa Ijumaa Takatifu au wa Belfast', ambao ulimaliza ghasia za miongo kadhaa zilizoikumba nchi ya Ireland Kaskazini. Kwa hiyo “kwa roho ya uthamini, ninasali kwa Mungu wa amani kwamba yale yaliyopatikana katika kifungu hicho cha kihistoria yaunganishwe kwa manufaa ya wanaume na wanawake wote wa Kisiwa cha Ireland”.

Salamu za Papa kwa mahujaji

Baba Mtakatifu Francisko aidha  akiendelea amesema: “Kwa mara nyingine tena, ninawatakia Pasaka Njema, Warumi na mahujaji kutoka nchi mbalimbali: “Kristo amefufuka; amefufuka kweli. Ninawasalimua sana, hasa vijana wa parokia za Vigevano, watu kutoka  Pisa na wale wa Appiano.

Asante kwa heri za Pasaka

Papa hakuhasahau kutoa shukrani kwa matashi mema aliyopokea kwamba:“Ninawashukuru wale wote ambao wamenitumia maneno ya kunitakia heri katika siku hizi. Ninashukuru sana kwa maombi; kwa maombezi ya Bikira Maria, Mwenyezi Mungu amlipe kila mmoja zawadi zake!

Kuomba amani kwa dunia na Ukraine

Baba Mtakatifu vile vile amesema matamanio yake kuwa:  “Ni matuamini ya “kila mtu atumie siku hizi za Oktava ya Pasaka katika furaha ya imani, ambayo maadhimisho ya Ufufuko wa Kristo yanarefushwa”. Papa ameomba kuwa na uvumilivu katika kuomba zawadi ya amani kwa ulimwengu wote, hasa kwa Ukraine wapendwa na wanaoteswa.

Baada ya Regina Caeli 10 Aprili 2023
10 April 2023, 15:45