Papa amekutana na Hilarion Mhusika wa zamani wa mahusiano ya Upatriaki,Moscow
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Katika siku pili ya ziara yake ya kitume nchini Hungaria, Jumamosi tarehe 29 Aprili, Papa Francisko amempokea kwa faragha Hilarion, Mkuu wa Kiorthodox wa Budapest nchini Hungaria na ambaye amepokea wadhifa huo tangu mwezi 2022 baada ya miaka kumi na tatu kama mwenyekiti wa Idara ya Masuala ya Kikanisa ya Nje ya Upatriaki wa Moscow, Kimsingi kama ‘Waziri wa mambo ya nje wa Patriaki Kirill’.
Mabadiliko ya ghafla yaliyotokana na mfululizo wa maamuzi yaliyochukuliwa wakati wa kikao cha Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiorthodox ya Urussi, iliyokutana katika monasteri ya Danilov huko Moscow, ambayo ilikuwa imebadilisha miundo ya baadhi ya tawala za maeneo. Hilarion pia alikuwa ameondolewa kazini kama Mkuu wa Volokolamsk na mshiriki wa kudumu wa Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiorthodox la Urussi na mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Juu ya Watakatifu Cyril na Methodius.
Uwezekano wa kukukutana na Papa ulikuwa umeelezwa na msemaji wa Vatican Dk. Matteo Bruni, wakati wa uwasilishaji wa ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican. Kwa hiyo Dk. Bruni katika fursa hiyo alisisitiza, hata hivyo, kwamba usikilizaji huo haukuwa kwenye ajenda. Kwa maana hiyo Mkutano huo kwa sauti ya upole, kama ilivyoripotiwa, ulidumu kama dakika 20, mbele ya Balozi wa Vatican, Askofu Mkuu Michael Wallace Banach, na ulifanyika katika Ubalozi wa Vatican huko Budapest, makazi ya Papa Francisko katika siku hizi za ziara.
Papa alimsalimia mkuu huyo kwa kumkumbatia na kubusu msalaba wake wa kifuani. Kulingana na ripoti kutoka kwenye tovuti ya Ukuu wa Kiorthodox ya Budapest, Hilarion alimweleza Papa juu ya maisha katika jimbo kuu la Hungaria la Upatriaki wa Moscow; shughuli zake za kijamii na kielimu, uhusiano na Kanisa Katoliki na madhehebu mengine ya Kikristo. Kama zawadi, alimpatia Papa Francisko vitabu vinne vikubwa kuhusu Yesu Kristo. Maisha na Mafundisho yametafsiriwa katika lugha ya Kiitaliano.
Ikumbu kwe Papa Francisko alikuwa amekutana na Hilarion kwa mara ya mwisho katika Jumba la Kitume, Vatican tarehe 22 Desemba 2021. Katika hafla hiyo kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, ilisema kuwa “ baadhi ya mada zilijadiliwa ambazo zinajumuisha sababu ya wasiwasi wa kawaida na katika uso wa ambao ni kawaida kujitolea kutafuta majibu halisi ya kibinadamu na kiroho”. Na Mkutano wa kwanza kati ya Papa Francisko na Mkuu huyo wa kirthodox ulifanyika mnamo tarehe 20 Machi 2013, siku iliyofuata mwanzo wa huduma ya Upapa Papa. Lakini kwa miaka mingi kumekuwa na matukio mengi Vatican, ikiwa ni pamoja na mmoja wa mwezi Februari 2020, na mkutano wa Roma kwa ajili ya uteuzi wa kimataifa “Watu, ndugu, ardhi ya baadaye”, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambapo sura hiyo ilionekana kuwapo.