Tafuta

Baba Mtatifu Francisko amekutana na walemavu wa taasisi ya László Batthyány-Strattmann huko Budapest Baba Mtatifu Francisko amekutana na walemavu wa taasisi ya László Batthyány-Strattmann huko Budapest  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa akutana na walemavu katika taasisi ya László Batthyány-Strattmann

Yesu alikuja kuleta ukweli kama ulivyokuwa na kuupeleka mbele.Angekuwa rahisi kuchukua mawazo itikadi na kuzipeleka mbele bila kuzingatia ukweli,hakufanya hivyo.Amesema hayo Papa wakati wa kutoa hotuba fupi bila kusoma katika Tasisi ya Mwenyeheri László Batthyány-Strattmann ta walemavu,Jumamosi 29 Aprili 2023

Na Angella Rwezaula, -Vatican.

Katika ziara yake ya kitume ya  41 huko Budapest  Hungaria, Jumamosi tarehe 29 Aprili  2023,  ikiwa ni siku yake ya pili ya ziar yake ambayo ratiba  ilianza  mapema sana kwa kukutana kwa  faragha na Watoto  wa Tasisi ya Mwenyeheri László Batthyány-Strattmann saa 2.45 hivi,  ambayo inawatunza watoto walemavu na pia vipofu. Papa Francisko baada ya watoto hao kuimba nyimbo, bila kusoma alitoa shukrani nyingi kwao  kwa ukaribisho na huruma. “Asante kwa nyimbo zenu, kwa ishara zenu, kwa mitazamo yenu. Asante Bwa Mkurugenzi kwa sababu ulitaka kuanza tendo hili na maombi ya Mtakatifu Francisko ambayo ni programu ya maisha kwa sababu Mtakatifu daima anaomba neema kwamba mahali ambapo  hakuna kitu mimi niweze kufanya kitu, wakati kitu kinakosekana mimi niweze kufanya kitu”.

Papa akiwa anatafsiriwa kinachozungumzwa
Papa akiwa anatafsiriwa kinachozungumzwa

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea ameeleza kuwa: “Mchakato wa safari ya kutoka katika uhalisia ni jinsi ulivyo, kwa kupelekea mbele na kufanya uhalisi wa kutembea na hii ndiyo Injili safi. Yesu alikuja kuleta ukweli kama ulivyokuwa na kuupeleka mbele. Angekuwa rahisi kuchukua mawazo, itikadi na kuzipeleka mbele bila kuzingatia ukweli. Hii ndiyo njia ya kiinjilisha, hii ndiyo njia ya Yesu na hili ndilo wewe Bwana Mkurugenzi ulitaka kulieleza kwa sala ya Mtakatifu Francis. Asante. Na asanteni nyote”, Papa amehitimisha.

Papa akiwa katika Taasisi ya Walemavu
Papa akiwa katika Taasisi ya Walemavu

Zawadi ya Papa: Maria nayefungua mafundo

Baba Mtakatifu Francisko, lakini hata hivyo aliwazawadia Picha Takatifu ya Mama anayefungua mafundo na ambayo katika historia yake  ina  asili huko Salento mnamo karne ya XVII na ambayo ni rahaisi kuitafsiri hisia za kina za kidini kwa watu wengi. Picha hiyo inayoonesha Bikira, anayetawaliwa na njiwa wa Roho Mtakatifu na kuzungukwa na Malaika, anawasilishwa kama Bikira Mkingiwa dhambi huku akifungua mafundo ya utepe wa harusi wa  wakati huo uliotumiwa na Wajerumani kusherehekea kifungo cha ndoa, wakati chini yake kuna Tobias akisafiri kwenda kumfikia bibi arusi wake, akiongozwa na Malaika Mkuu Raphael na akiongozana na mbwa wake. Padre wa wakati huo Jorge Mario Bergoglio. S.J., (Papa Francisko) alipoina mara moja alichapisha maelfu ya postikadi na kuzituma huko Buenos Aires, Argentina na Amerika Kusini yote.

Papa amezawadia picha ya Maria anayefungua mafundo:
Papa amezawadia picha ya Maria anayefungua mafundo:

Ni kazi ya mwenye ibada Padre Hyeronimus Langenmantel, ambaye alielezea kwa mchoraji Schmidtern ili kukumbuka neema alizopokea kwa babu na bibi zake Wolfgang na Sophie. Kutokana na kwamba wenye ndoa hao ambao walikuwa na mgogoro mkubwa na kila mara walipokuwa wakigombana, Sofia alikuwa anafunga fundo kwa utepe wake wa siku ya ndoa, na huo utepe ulipojaa mafundo na talaka ya ndoa ilikuwa karibu, mme wake akiwa ameshikwa na mahangaiko, alikabidhi Padre Mjesuit Jakob Rem, ambaye alimkabidhi kwa Bikira Maria ili aweze kurudisha maelewano ya ndoa, kwa “kufungua mafundo yote”. Kwa hiyo, ibada ya Mama anayefungua mafundo inapata kiukweli msingi wake katika sala ya kizamani ya Maria Auxilium christianorum, ambaye tayari katika Litania, ya Lauretane katika enzi za Upapa wa Papa Mtakatifu Pio V, na ambaye alikuwa anatambua nafasi kuu ya Mama katika kuingilia kati kwa kila neema, hadi kufikia Mtaguso wenyewe wa II wa Vatican kuelekeza hata “kama ‘Wakili’, ‘Mwokozi’ na Mwombezi’.

Papa amekutana na watoto walemavu katika Taasisi ya Mwenyeheri Strattiman

Hata hivyo kabla ya kuhusisha ibada hii ya Maria, inapatikana katika Maandishi ya Mtakatifu Ireneo wa Lione anayeandika kuwa: “Fundo la kutotii kwa Hawa lilikuwa na suluhisho lake kwa utiifu wa Maria; kile ambacho bikira Eva alikuwa amekifunga kwa kutokuamini kwake, Bikira Maria alifungua kwa imani yake.” Kwa  hiyo ni  mantiki pendwa sana na Papa Franciskol ambaye mara nyingi amekuwa akitaja na kusali Rosari Takatifu. Kumwomba Bikira Maria afungue ‘mafundo’ hayo mengi ambayo hushika ubinadamu kila siku inawakilisha na kuelezea njia ya kuhisi umoja wote chini ya ulinzi wake wa kimama.

Tukirudi katika Taasisi ya watoto walemavu  kiukweli kuna safu ya walezi  ambayo hutegemea kuta za ukumbi wa mazoezi. Katika kuta zimeandikwa majina ya watoto. Vile vile katika chumba hicho  kuna baiskeli ndogo za mazoezi, pia zilizoundwa kwa ajili ya wageni wa muundo ho wa ulemavu. Kuingia katika Taasisi ya László Batthyány-Strattmann iliyoko Budapest kunamaanisha kukutana na tabasamu za wale wanaokabiliana na matatizo yanayohusiana na ulemavu mbaya kila siku. Nyuso za watoto na vijana wanaopata faraja na kuungwa mkono katikaukweli huu ulioanzishwa na Sista Anna Fehér, anayekumbukwa kama ‘Mama Teresa wa Hungaria’ na ambaye, huwaunga mkono wale walio na fursa ya kuwatazama. Kila ushindi mdogo ni hatua kubwa kwao. Kwa sababu hii, pamoja na waelimishaji, wajitolea na wanasaikolojia, wataalamu wa viungo (physiotherapists) wa ngazi ya juu pia hufanya kazi katika jengo hilo. Kila undani unastahili uangalifu mkubwa.

Papa ameembelea Taasisi ya Walemavu
Papa ameembelea Taasisi ya Walemavu
29 April 2023, 10:03