Tafuta

Mkutano wa Papa na wakimbizi na wahamiaji:Haitoshi mkate bali kulisha hata mioyo ya watu

Baba Mtakatifu akiwa katikati ya maskini na wakimbizi amesisitiza juu ya kutumia lugha ya upendo.Imani isiwe mawindo ya aina fulani ya ubinafsi wa kiroho kwa kadiri ya utulivu wa ndani wa mtu.Imani ya kweli ni ile ambayo haina raha na inaongoza nje kukutana na maskini.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 29 Aprili 2023 mara baada ya kusikiliza shuhuda kadhaa ameanza hotuba yake  ikiwa ni ya Tatu tangu amefika katika Ziara yake ya kitume huko Budapest nchini Hungaria, kwa kuonesha furaha ya kuwa katikati yao na kushukuru,  maneno ya makaribisho na shukrani ambapo imekumbusha huduma ya ukarimu ambayo Kanisa la Hungaria linatekeleza kwa ajili ya maskini. Papa amesema maskini na wenye kuhitaji wasisahaulike kamwe kwa sababu wako kwenye moyo wa Injili:Yesu kiukweli alikuja kuwaletea habari njema maskini(Lk 4:18). Kwa hiyo wao wanaonesha changamoto ya kusisimua, ili imani wanayokiri isiwekama ya mfungwa wa ibada iliyo mbali na maisha na isiwe  kama mawindo ya aina fulani ya  ubinafsi wa kiroho, yaani, hali ya kiroho ninayojenga kulingana na utulivu wa mtu binafsi wa ndani na kuridhika kwa mtu. Imani ya kweli, kwa upande mwingine, Papa amesisitiza ni ile ambayo inasumbua, ambayo inahatarisha, ambayo huleta kukutana na maskini na kuwafanya waweze kuzungumza lugha ya upendo na maisha. Kama Mtakatifu Paulo anavyothibitisha, Baba Mtakatifu amenukuu “inawezekana kuzungumza lugha nyingi, kuwa na hekima na utajiri, lakini kama hatuna upendo, hatuna kitu na sisi ni kitu bure (1 Wakor 13:1-13).

Mkutano wa Papa na wakimbizi na wahamiaji
Mkutano wa Papa na wakimbizi na wahamiaji

Lugha ya upendo amebainisha  Papa kwamba ilikuwa ni lugha iliyozungumzwa na Mtakatifu Elizabeth, ambaye watu wa Hungaria  wana ibada kubwa na upendo.  Papa ameeleza kwamba akiwa amefika  hapo aliona sanamu yake katika  uwanja, na msingi ukimuonesha akipokea kanuni ya  Wafransisko na  wakati huo huo, akitoa maji ya kukata kiu ya maskini. Ni taswira nzuri ya imani: wale “wanaojifungamanisha na Mungu”, kama alivyofanya Mtakatifu Fransisko wa Assisi aliyemvuvia Elizabeth, wanajifungua wenyewe kwa upendo kwa maskini, kwa sababu “mtu akisema: ‘Nampenda Mungu’ na kumchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana mtu ye yote asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu asiyemwona” (1 Yoh 4:20). "Mtakatifu Elizabeth, binti wa mfalme, alikulia katika raha ya maisha ya mahakama, katika mazingira ya anasa na upendeleo; hata hivyo, kwa kuguswa na kubadilishwa na kukutana na Kristo, mara moja alihisi kukataliwa kwa utajiri na ubatili wa ulimwengu, akihisi hamu ya kujiondoa kutoka kwao na kuwatunza wale walio na shida. Kwa hiyo, hakutumia mali yake tu, bali pia maisha yake kwa ajili ya watu wadogo kabisa, wenye ukoma, wagonjwa hadi kuwatibu kibinafsi na kuwabeba mabegani mwake, hii ndiyo  lugha ya upendo", amesisitiza Papa.

Mkutano wa Papa na maskini na wakimbizi
Mkutano wa Papa na maskini na wakimbizi

Papa Francisko amesema kuwa Brigitta pia aliwambia kuhusu hilo, wakati wa ushuhuda wake  kwa hiyo amemshukuru ushuhuda huo. Mapungufu mengi, mateso mengi, kazi ngumu sana ya kujaribu kusonga mbele na kutowaacha watoto wake wakose mkate na, katika wakati wa kushangaza zaidi, Bwana alikuja kukutana naye ili kumsaidia. "Lakini tumesikia kutoka katika maneno yake mwenyewe jinsi gani Bwana aliingilia kati? Yeye, anayesikia kilio cha maskini, huwahesabia haki walioonewa, huwapa wenye njaa chakula na huwainua walioanguka (Zab 146:7-8), kamwe hafiki kwa kutatua matatizo yetu kutoka juu, lakini hukaribia kwa kukumbatia na huruma yak, ikichochea huruma ya akina ya kaka na dada wanaotambua jambo hilo na hawabaki kughafilika. Brigitta alisema alivyoweza kujionea ukaribu wa Bwana kwa shukrani kwa Kanisa Katoliki la Kigiriki, kwa watu wengi waliojitahidi kadiri wawezavyo kumsaidia, kumtia moyo, kumtafutia kazi na kumtegemeza katika mahitaji ya kimwili na katika maisha safari ya imani. “Huu ndio ushuhuda unaotakiwa kwetu: huruma kwa wote, hasa kwa wale walio na alama ya umaskini, magonjwa na maumivu. Tunahitaji Kanisa linalozungumza kwa ufasaha lugha ya upendo, lugha ya ulimwenguni pote ambayo kila mtu anaisikia na kuielewa, hata walio mbali zaidi, hata wale wasioamini”.

Mkutano wa Papa na wakimbizi na mahamiaji
Mkutano wa Papa na wakimbizi na mahamiaji

Na katika suala hili Papa ametoa shukrani zake kwa Kanisa la Hungaria kwa kujitolea kwa upendo, ahadi msingi ambayo  imeunda mtandao unaounganisha wafanyakazi wengi wa kichungaji, wanaojitolea wengi, parokia na Caritas  jimbo, lakini pia vikundi vya sala, jumuiya za waamini, mashirika ya madhehebu mengine, lakini yameungana katika umoja huo wa kiekumene unaobubujika kutoka katika upendo. Papa amewashukuru kwa jinsi ambavyo wamekaribisha, si tu kwa ukarimu lakini pia kwa shauku, wakimbizi wengi kutoka Ukraine. Papa aidha amethitisha alivyo sikiliza kwa hisia kali ya ushuhuda wa Oleg na familia yake; kwani safari yao ya siku zijazo ya mustakabali tofauti, mbali na vitisho vya vita,  kiukweli ilianza na safari ya chini ya kumbukumbu, kwa sababu Oleg alikumbusha ukaribisho mzuri aliopokea huko Hungaria miaka iliyopita alipokuja kufanya kazi kama mpishi. Kumbukumbu ya jambo hilo ilimtia moyo aondoke pamoja na familia yake na kufika Budapest, ambako alipata ukarimu mwingi. Kumbukumbu ya upendo uliopokea hufufua tumaini, unawahimiza kuanza njia mpya za maisha.

Papa amekutana na watu wanaohitaji msaada
Papa amekutana na watu wanaohitaji msaada

Hakika Papa amesema, hata katika maumivu na mateso, mtu hupata ujasiri wa kwenda mbele wakati amepokea ari ya upendo: ni nguvu ambayo husaidia kuamini kwamba yote hayapotei na kwamba wakati ujao tofauti unawezekana. “Upendo ambao Yesu anatupatia na anatuamuru tuishi hivyo unasaidia kutokomeza katika jamii, kutoka katika miji na maeneo tunamoishi, maovu ya kutojali na ubinafsi, na kufufua tumaini la ubinadamu mpya, wenye haki zaidi na wa kidugu ambapo kila mtu anaweza kujisikia nyumbani”. Katika hotuba hiyo, ameendelea kukazia kuwa kwa bahati mbaya, watu wengi huko hawana makazi: dada na kaka wengi walio na hali dhaifu peke yao, na usumbufu wa mwili na kiakili, huharibiwa na sumu ya dawa za kulevya, huachiliwa kutoka gerezani au kutelekezwa kwa sababu ni wazee , kwa hiyo wameathiriwa na aina mbaya za umaskini wa mali, hata umaskini wa kiutamaduni na kiroho, na hawana paa na nyumba ya kuishi.

Zoltàn na mkewe Anna walitoa ushuhuda wao juu ya balaa hilo kuu, kwa hiyo Papap amewashukuru  kwa maneno yao. Amewshukuru kwa kukubali mwendo huo wa Roho Mtakatifu uliowaongoza, kwa ujasiri na ukarimu, kwa kujenga kituo cha kuwakaribisha watu wasio na makazi. Baba Mtakatifu amefafanua jinsi gani alivyovutiwa kusikia kwamba, pamoja na mahitaji ya kimwili, wanatilia maanani historia na hadhi iliojeruhiwa ya watu, wakitunza wapweke wao, mapambano yao ya kujisikia kupendwa na kukaribishwa duniani. Kwa mujibu wa Anna alieleza kwamba “ni Yesu, Neno lililo hai, anayeponya mioyo yao na uhusiano wao, kwa sababu mtu huyo hujijenga upya kutoka ndani”; yaani, amezaliwa upya, yaani, anapopata uzoefu kwamba anapendwa na kubarikiwa machoni pa Mungu. Hii inatumika katika Kanisa zima: haitoshi kutoa mkate unashibisha tumbo, bali kuna haja ya kulisha hata  mioyo ya watu!

Papa Francisko amekutana na wakimbizi na wahamiaji
Papa Francisko amekutana na wakimbizi na wahamiaji

Upendo si msaada wa kimwili na kijamii tu, bali humjali mtu mzima na kutamani kumrudisha katika miguu yake kwa upendo wa Yesu: upendo unaosaidia kurejesha uzuri na heshima. “Kufanya hisani kunamaanisha kuwa na ujasiri wa kuwa na mtazamo ambao  huwezi kumsaidia mwingine kwa kuangalia pembeni. Ili kufanya upendo unahitaji ujasiri wa kugusa, huwezi kutupa sadaka kwa mbali bila kugusa. Kugusa na kutazama na hivyo kwa kugusa na kutazama unaanza safari, mchakato wa safari ya mtu huyo mhitaji, ambaye atakufanya uelewe ni kiasi gani wewe ni mhitaji, mtazamo wa macho na mkono wa Bwana. Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo wazungumze daima kwa lugha ya upendo. Sanamu katika uwanja, unaelezea muujiza maarufu wa Mtakatifu Elizabeth, inasimulia kwamba Bwana siku moja aligeuza mawaridi kuwa mkate ambao alikuwa anapeleka kwa wenye kuhitaji.  Ndivyo hivyo hata kwao, wanajibidisha kupelekea mkate kwa wenye njaa, Bwana anafanya kuchanua furaha na arufu nzuri ya msaada wao kwa upendo ambao wanautoa. Amewatakia walepeke daima arufu ya upendo katika Kanisa na katika Nchi. Kwa kuhitimisha ameomba waendelee kusali kwa ajili yake. Wamesali nsala ya Mwisho na kuwabariki.

29 April 2023, 11:45