Je,Juhudi za ubunifu kwa ajili ya amani ziko wapi?
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ni swali la kushangaza ambalo Papa Fransisko ameuliza wakati wa hotuba yake kutoka katika moyo wa Ulaya, huko Hungaria ambapo mipaka ya nchi yake inagusa Ukraine, mwathirika wa vita vya uchokozi vya Urussi. Ni swali ambalo kwanza kabisa linawapatia changamoto viongozi wa mataifa yanayohusika pamoja na wakuu wa serikali za Ulaya na wale kutoka duniani kote. Pia linatia changamoto dhamiri ya kila mmoja wetu. Papa aliyafanya kuwa maneno yake yaliyotamkwa mnamo mwaka1950 na baba mwanzilishi wa Ulaya, Robert Schuman: “Mchango ambao Ulaya iliyopangwa na muhimu inaweza kutoa kwa ustaarabu ni muhimu kudumisha mahusiano ya amani”, kwani “ulimwengu wa amani hauwezi kulindwa isipokuwa kwa juhudi za ubunifu, sawa na hatari zinazotishia.” Papa Fransisko ameyafafanua maneno hayo kuwa “ya kukumbukwa,” ambapo baadaye akajiuliza: “Katika awamu hii ya kihistoria kuna hatari nyingi; lakini, ninashangaa, hata nikifikiria Ukraine iliyopigwa, je juhudi za ubunifu za amani ziko wapi?”
Ni muhimu kutambua kwamba Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella, mwaka mmoja uliopita, akizungumza katika Baraza la Ulaya, alikuwa tayari amenukuu sentensi hii kutoka kwa Schuman kwamba juhudi hizi za ubunifu ziko wapi? Iko wapi diplomasia na uwezo wake wa kuchukua njia mpya na za ujasiri za kujadili kumaliza mzozo? Iko wapi ‘mifumo ya amani’ ya kuweka katika mchezo ili kushinda “mifumo ya vita inayokuja? Swali la Papa Francisko ni la kushangaza na la kweli. Inashangaza, kwa sababu inatukabili na ukosefu wa mpango kwa upande wa Ulaya ambao unaonekana kujisalimisha katika mantiki ya kuweka silaha tena na vita huku ikionekana kutosema lolote kuhusu amani. Ni mwanahalisi kwa sababu anatuonya dhidi ya kuzoea “mchezo wa kitoto wa kivita, kwa mzozo mbaya ambao unaweza kuzorota wakati wowote, na matokeo yake ni janga kwa wanadamu wote.
Lakini maneno ya Papa, bado yamaanisha mchakato wa umoja wa Ulaya, na yana “tumaini kubwa pamoja na Umoja wa Mataifa kuzuia vita zaidi baada ya ile mbaya kumalizika ya mnamo 1945, na mabyo tayari yanajibu. Hi inatokana na mwaliko wa kugundua kwa upya ‘nafsi ya Ulaya’, shauku na ndoto ya mababa waanzilishi, watu wa serikali ambao wameweza kutazama nje ya mipaka yao, ambao hawajashindwa na ving'ora vya utaifa na wameweza kurekebisha badala ya kurarua. Mamilioni ya watu leo hii wanaoona matumaini makubwa yaliyotolewa kufikia mwisho wa Vita Baridi yakipotea na kuona jinamizi la tishio la atomiki likirejea, wanangoja jibu: je juhudi za ubunifu za amani ziko wapi?