Papa:Hati ya Pacem in Terris inahamasisha maamuzi na mipango ya wakuu wa mataifa
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mtazamo wa utulivu katikati ya mawingu meusi. Kielelezo cha uwazi kilikuwa cha Pacem in Terris, ambao ni waraka wa amani wa Papa Yohana XXIII, katika siku zake za mwisho wa upapa wake, uliochapishwa tarehe 11 Aprili 1963. Kwa hiyo mawingu meusi yalikuwa ni makabiliano ya kisiasa na kijeshi kati ya mataifa mawili makubwa yaliyoshinda Vita vya Pili vya Dunia ambayo yaliiweka dunia katika mashaka kutokana na hatari ya tishio la nyuklia. Papa Francisko Jumatano tarehe 12 Aprili 2023 mara baada ya Katekesi yake amekumbuka hati muhimu ya Papa Roncalli.
Papa amesema kwamba tarehe 11 Aprili ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka sitini ya andiko la Pacem in Terris ambalo Mtakatifu Yohane XXIII alielekeza kwa Kanisa na kwa ulimwengu mzima katikati ya mvutano kati ya kambi mbili zinazopingana katika kile kinachoitwa Vita Baridi. Papa alifungua mbele ya kila mtu upeo mpana wa kuweza kuzungumza juu ya amani na kujenga amani, mpango wa Mungu kwa ulimwengu na familia yake ya kibinadamu.
Ujumbe wa wakati muafaka
Kwa upande wa Papa Francisko amebainisha kuwa , andiko hilo lilikuwa baraka ya kweli, kama taswira ya utulivu katikati ya mawingu meusi. Ujumbe wake unafaa sana, alisisitiza Papa huku akinukuu kifungu kizima, cha 62: Mahusiano kati ya jumuiya za kisiasa, kama yale kati ya binadamu binafsi, lazima yadhibitiwe si kwa kutumia nguvu za silaha, bali kwa mwanga wa sababu; yaani, katika ukweli, katika haki, katika mshikamano tendaji”.
Mwaliko kwa viongozi wa mataifa
Baba Mtakatifu amewaalika waamini, wanaume na wanawake wenye mapenzi mema, waraka wa “kusoma Pacem in Terris” kwamba “ Ninaomba viongozi wa mataifa wajiachie wahamasishwa nayo katika mipango na maamuzi yao.
Maombi kwa ajili ya Ukraine iliyopigwa
Papa Francisko aidha amezingatia mizozo mingi na ya umwagaji damu inayoharibu mabara matano, kuanzia na lile la Ukraine. Kwa taifa lililoshambuliwa, Papa ameomba kwa mara nyingine tena, kama kawaida katika miito kwa umma tangu mwanzo wa vita, kuomba na kutosahau nchi hiyo kwamba “ Tudumu katika maombi kwa ajili ya Ukraine iliyouawa kishahidi. Tuombe kwa ajili ya kile Ukraine inateseka
Tunahitaji Huruma ya Baba
Papa alikuwa tayari ameeleza hitaji la amani duniani katika salamu zake kwa mahujaji wa Poland, ambao aliwakumbusha maadhimisho ya karibu ya Dominika ya Huruma ya Mungu, iliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kama alivyotaka Bwana Yesu kupitia Mtakatifu Faustina Kowalska karibu karne moja iliyopita. Leo katika ulimwengu unaozidi kujaribiwa na vita na kujitenga na Mungu, tunahitaji hata zaidi Huruma ya Baba. Papa alisisitiza tena juu ya huruma katika salamu zake kwa lugha ya Kiitaliano, ambayo haikosi kamwe kwa upande wa Mungu: “Bwana hakosi kamwe kuwa na huruma, tufikirie huruma ya Mungu anayetukaribisha daima, inatusindikiza daima. Hatuachi peke yetu kamwe”.