Papa Francisko ameondoka Hungaria:Ametoa shukrani kwa rais kwa ukarimu
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko aliondoka Hungaria Dominika tarehe 30 Aprili 203 saa 12.08. Kwa hiyo ndiyo hitimisho la Ziara yake ya 41 ya kitume, kwa siku tatu alizokaa Budapest, kufanya ratiba yake kama ilivyokuwa imepangwa. Nchini, Hungaria Baba Mtakatifu kama kharifa wa Mtume Petro alitoa hotuba sita, ambapo aliwaimarisha imani kwa watu waamini watakatifu wa Mungu wa Hungaria, akiwataka wajenge amani barani Ulaya inayoitwa kuwa jumuishi na wazi zaidi kwa kila mtu bila kufungwa na itikadi zozote.
Ni ndege ya Blu A320) ya Italia, ambayo itatua Fiumicino, baada ya masaa mawili kutoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ferenc Liszt wa mji mkuu. Kabla ya kuondoka afla ilifanyika ya kuagwa. Akisalimiana na Papa Rais wa Jamhuri Bi Katalin Novák, alizungumza naye kwa dakika chache, kisha akaondoka kuelekea kwenye ndege. Walionekana watu wengi sana waliokuwa wamefika kumuaga kuanzia viongozi wa Kanisa, serikali pamoja na baadhi ya waamini wa Hungaria.
Muda mfupi baada ya kuondoka, Baba Mtakatifu Francisko alituma telegramu ya kawaida ya kuaga kwa Rais Novák, ambapo shukrani inaoneshwa kwa mamlaka ya Hungaria na raia kwa mapokezi ya joto na ukarimu mkubwa. Kwa hiyo Papa, anamwakikishia maombi yake, na kuliombea taifa baraka za Mwenyezi Mungu kwa umoja, udugu na amani.