Urbaniana:siku ya wanawake na utakatifu wa kike katika Kanisa
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Wanawake watakatifu, wanawake ambao ni mifano ya maisha ya Kikristo ndiyo walikuwa wahusika wakuu katika mada ya “Siku ya sherehe. Wanawake katika Kanisa: waumbaji wa binadamu” ambayo ilifanyika alasilia tarehe 8 Machi 2023 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana , Roma kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano la Kimataifa ambalo kwa mada hiyo hiyo litafanyika katika kipindi kijacho mwaka mmoja, mnamo tarehe 7 na 8 Machi. Tukio hilo lilifadhiliwa na chuo kikuu kilichobobea katika malezi ya wakleri wa kimisionari pamoja na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Avila (UCAV), Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu, Kitivo cha Taalimungu cha Kipapa cha Teresianum na Taasisi ya Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Juu kuhusu Wanawake katika Chuo Kiuu cha Kipapa cha Regina Apostolorum, kwa udhamini wa Mabaraza ya Kipapa ya Kuwatangaza watakatifu, Utamaduni na Elimu na Uinjilishaji, katika kitengo cha masuala msingi ya Uinjilishaji ulimwenguni.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana, Padre Leonardo Sileo, alifungua kazi hizo, ambaye alisisitiza haja ya kutambua uwepo wa watakatifu wengi katika familia nzima ya binadamu na haja ya kujifunza kuishi kwa uangalifu na matunda kutoka kwa maisha ya watakatifu na utakatifu wa kike hasa. Wakati huo María del Rosario Sáez Yuguero, mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Avila, alirudi kwenye sura ya Mtakatifu Teresa wa Avila, mwalimu wa maisha ya kiroho, mfano wa mwanamke wa wakati wetu na ambaye tunajifunza kutoka kwake kwamba furaha haiwezi kupatikana isipokuwa mtu apate uzoefu wa Mungu na katika maisha ya mtu mwenyewe, alichukua safu ya mkutano wa vyuo vikuu kutazama Madaktari Wanawake wa Kanisa na Wachungaji wa Ulaya katika mazungumzo na ulimwengu wa leo ulioandaliwa mwaka mmoja uliopita, tena Urbaniana, na ambao utafuatiliwa kama ulivyopangwa kwa mwaka ujao.
Askofu Mkuu Rino Fisichella, wa Kitengo cha masuala Msingi ya uinjilishaji katika ulimwengu wa Kanisa alizungumzia “Utakatifu na Jubilee ya 2025”, ambaye alitangaza kujumuishwa kati ya hija za Jubilei ya njia iliyowekwa kwa walezi wanawake, Madaktari wa Kanisa na kusisitiza kwamba mada ya utakatifu inavutia zaidi leo hii katika nuru ya mchakato wa safari ambayo Kanisa linafanya, zaidi ya yote kwa kusoma tena tabia za watakatifu wa karibu ambao Papa Francisko amekuwa akieleza katika Wosia wake wa Kitume Gaudete et Exultate.
Askofu Mkuu Fisichella alieleza kwamba, maisha ya utakatifu yanaoneshwa katika maisha ya kufuata na kwamba njia ya utakatifu inahusishwa na asili ya Kanisa, ambapo hakuna mtu anayetengwa na wito huu. Utakatifu ni dhamira ya maisha kwa waamini – katika wito kwa mtindo wa maisha thabiti, unaoweka kusikiliza Neno la Mungu kwanza. Kisha akikumbuka kauli mbiu aliyoichagua Baba Mtakatifu Fransisko ya Jubilei ya 2025, isemayo “Mahujaji wa matumaini”, Askofu alifafanua kwamba mwito wa utakatifu unahitaji hija inayohusisha wongofu wa moyo na kwamba njia ya utakatifu haifungwi yenyewe, binafsi bali huzaa utakatifu na kuutakasa.
Naye Katibu wa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza watakatifu Monsinyo Fabio Fabene alitoa maelezo ya jumla kuhusu sababu za kutangazwa kuwa watakatifu kwa wanawake, akibainisha kuwa wanawake 26 walitangazwa kuwa watakatifu na Papa Francis, 130 walitangazwa kuwa wenyeheri huku mchakato ukifunguliwa kwa wengine 151. “Wanawake watakatifu wanatoa mfano wa uwezo na ustahimilivu" alisema Monsinyo Fabene, akibainisha kwamba mchango wa kimsingi unaoletwa na wanawake katika kiungo cha kikanisa ni ule wa huruma, ambao mara nyingi hurejewa na Papa Francisko na kwamba jiwe kuu la utakatifu wa kike ni mapenzi ya kujikamilisha na kufanya kila wawezalo kwa ajili ya wengine.
Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu Bi Antonella Sciarrone Alibrandi, yeye alitoa mfano wa Utakatifu wa Kike na elimu kwa kutoa mfano wa sura ya Armida Barelli, mwanzilishi mwenza wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha Moyo Mtakatifu, ambaye alitumia maisha yake hivyo utamaduni huo ulikuwa wazi kwa kila mtu na zaidi ya yote kwa wanawake. Kuhusu utakatifu katika familia na ndoa, Bi Gabriella Gambino, katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha alitoa mifano mbalimbali kuanzia Gregori na bibi hadi wenzi wa ndoa Beltrame Quattrocchi. Leo hii Kanisa linapata ufahamu wa familia nyingi za jirani ambazo zimeacha matokeo mazuri ya maisha ya Kikristo", alisisitiza huko akionesha kwamba ile ya wanandoa ni safari ya pamoja kuelekea mbinguni, ambapo utakatifu unajumuisha kuingiliana kwa mwelekeo mlalo na wima wa maisha. Lakini leo hii, kuna utakatifu, hata katika familia nyingi za kike, ambapo wanawake wa kishujaa, walioachwa peke yao, wanajaribu kuokoa mahusiano ya familia.
Profesa Cristina Reyes, makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu, ambaye alionesha yaliyomo katika mkutano wa wanawake uliopangwa kufanyika 2024, aliliambia Vatican News katika mahojiano kwamba wazo la tukio la siku mbili ambalo kamati ya maandalizi inafanya kazi ni kutafakari juu ya watu halisi, historia ukweli na maneno ya wanawake ambao wameishi uzoefu wao wa Kikristo kwa ukamilifu. Mwaka ujao, kutakuwa na wanawake 10 wasanii wa binadamu" ambao watajadiliwa, kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Miongoni mwao ni Madeleine de Jésus, kutoka Ufaransa, Elizabeth Ann Seton, kutoka Marekani, Mary MacKillop kutoka Australia, Laura wa Mtakatifu Caterina wa Siena, kutoka Colombia, Mama Teresa wa Calcutta, kutoka Albania. Wote ni watawa, kila mmoja akiwa na hali yake ya kiroho, na ushuhuda wake wa maisha, alibainisha Profesa Reyes ambaye pia anakisi kwa kina cha wanawake hawa katika kupitia mateso. "Wanawake wanatofautishwa na kina ambacho wanapata maisha katika awamu zake zote na kisha kwa uwezo wa kuzingatia watu, hasa walio hatarini zaidi, na kwa ukarimu katika kusindikiza na kuchukulia kuwajali wengine". Kuhusu mchango wa wanawake katika Kanisa, Profesa Reyes alisema wanapaswa kutambuliwa, hasa, katika uenezaji wa imani.
Lengo la mkutano mwaka ujao ni uinjilishaji, ali sema Profesa Lorella Congiunti, profesa wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na mjumbe wa sekretarieti ya maandalizi kujifanya chombo cha utume huu tulionao kama wanawake, kama wanawake waliobatizwa. Mkutano huo uliofanyika mwaka mmoja uliopita juu ya madaktari wanawake wa Kanisa na watakatifu walinzi wa Ulaya ulitoa mchango kwa ujuzi wa watu hawa watakatifu, ambao majina yao mara nyingi hujulikana tu, Profesa Congiunti anakiri, mawazo yao, maisha yao na ushuhuda juu ya umuhimu wao. ziliwasilishwa. Lakini mkutano huo pia ulitoa mchango mkubwa wa sinodi za kitaaluma kwa ushirikiano kati ya vyuo vikuu ambavyo vimeendelea. Ushirikiano unaowaona wanawake na wanaume wakifanya kazi, kazi ya utajiri mkubwa, juu ya utafiti wote, kwa sababu inalenga sio tu kuimarisha ujuzi wa wanawake wakuu watakatifu, bali pia wa wengine wengi. “Duniani kote kuna watu wengi wadogo ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa ulimwengu bora, katika ujenzi wa Makanisa mahalia, wametuangazia na wanaweza kutuangazia tena”, alihitimisha Profesa Congiunti.