2023.03.04 Nembo ya Kongamano la Vijana 'Flame 2023', Uingereza na Walles. 2023.03.04 Nembo ya Kongamano la Vijana 'Flame 2023', Uingereza na Walles. 

Papa na vijana wa Uingereza na Wales:shuhudia kwa ujasiri kuwa Injili inawaweka huru

Katika ujumbe kwa ajili ya mkusanyiko kubwa la vijana Katoliki nchini Uingereza na Wales kwa ajili ya maandalizi ya Siku ya Vijana duniani WYD,Papa anatumaini kwamba vijana kama Maria Mama wa Mungu,wataitikia mara moja wito wa Bwana wa kumfuata.Ujumbe umetiwa saini na Katibu wa Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Majimbo ya  Uingereza na Wales yanayotoa huduma mbalimbali kwa ajili ya uchungaji wa Vijana, kuanzia wafanyakazi wa muda wote wa majimbo  hadi vijana wa kujitolea,  kwa hiyo ni  timu za utume zinazoweza kutoa uzoefu wa utume ndani ya shule  na mazingira ya  kazi kwa  huduma ya Kichungaji ya  Vijana, iitwayo CYMFed ambayo  hupanga na kuwezesha huduma yao katika Nyanja mbali mbali kama kuratibu Hija na safari za kwenda katika Siku ya vijana duniani (WYD), Lourdes; Sala na ushirika wa kawaida;  Vituo vya Makazi visivyo vya majimbo,  Sherehe za vipindi vya Majira ya mwaka /Kambi na mengine.

Ukaribu wa Papa Injili itawafanya kuwa huru

Katika fursa hiyo  Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake uliotiwa saini na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolini, Jumamosi tarehe 4 Machi 2023, kuuelekeza kwa Mheshimwa Domini Howarth, Mwenyekiti wa Timu ya Maandalizi ya kongamano hilo la CYMFED, liitwalo ‘Flame’ katika fursa ya mkusanyiko huo mkubwa sana. Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu anabainisha alivyoelewa “kuhusu vijana wakatoliki kutoka Uingereza na Wales walivyo kusanyika pamoja katika uwanja mmoja kwa ajili ya Kongamano la mwaka 2023”. Kwa hiyo anawatumia wote matashi mema na kuwahakikishia ukaribu wake wa kiroho.  Baba Mtakatifu kwa hiyo anasali kwa Mungu mwenyezi “ili awabariki kwa wingi wa neema wakati huo wakiabudu, muziki, shuhuda na kushirikishana  urafiki na Kristo  pamoja wengine waliopo. Kwa kufanya hivyo watakuwa na nguvu katika Imani na upendo na kutoa ujasiri wa ushuhuda kwa ujumbe wa Injili ambao utawafanya kuwa huru”.

Vijana wawe kama Maria aliyekwenda haraka

Kama wafanyavyo hiyo, “ni matumaini  ya Baba Mtakatifu kwamba “mkutano huo, utawaweza kuwa kama Maria mama wa Mungu aliyeitikia kwa haraka wito wa Bwana kumfuata na kwa namna ya pekee bila kuwa na sintofahamu, ili kijikita katika  mawazo na wengine mbali na  ya ulimwengu, ili kushuhudia  uzuri na ukarimu, huduma, usafi, uvumilivu, kusamehana uaminifu kwa wito binafsi, sala, bila kuchoka kwa hakika na kwa mapenzi mema, na kuwa na upendo kwa maskini na urafiki kijamiii (Christus Vivit, 36)”. Baba Mtakatifu kwa imani ya washiriki wote na familia zao anawakaibidhi kwa maombezi ya Mama yetu wa Walsinghan, na kuwabariki kwa neema na hekima, furaha na amani ya Bwana wetu Yesu.

Wito wa kusimama kidete kwa ajili ya imani katoliki

Flame yaani ‘Cheche’   ni tukio kubwa zaidi la vijana wa Kikatoliki nchini Uingereza, lililoandaliwa mwaka huu siku 150 kabla ya  Siku ya Vijana Duniani huko Lisbon nchini Ureno itakayofanyika mnamo tarehe 1-6 Agosti 2023. Kichwa cha toleo la 2023, 'Amka!' ambacho kimetolewa katika kauli mbiu  ya ya Siku ya Vijana Duiniani (WYD): “Maria aliamka akaenda haraka”. Kwa upande wa waandaaji wamebainisha kwamba “huo  ni  mwaliko, awa kuamka baada ya janga, kuamka kama Wakatoliki vijana ili kama Maria alivyofanya  kwa tukio la kushangaza na zuri ambalo ni imani yetu ya Kikatoliki.”

UJUMBE WA PAPA KWA VIJANA UINGEREZA
04 March 2023, 17:51