Tafuta

Watu sita waliuawa katika  shule ya Convenant Nashville, huko Tennessee,Marekani. Watu sita waliuawa katika shule ya Convenant Nashville, huko Tennessee,Marekani.  (AFP or licensors)

Uchungu wa Papa kwa janga la risasi huko Nashville:Kitendo kisicho na maana cha vurugu

Katika telegramu kwa Askofu wa mji la Nashville nchini Marekani,eneo la mauaji ya kutisha,Papa Francisko anawahakikishia ukaribu na sala wote walioguswa na mkasa huo na anaomba ili kwamba mema yaweze kutoka kwenye uovu usioelezeka.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Salamu za rambirambi na maombi za Baba Mtakatifu Jumatano tarehe 29 Machi 2023 aliwatumia kwa wote walioguswa katika tukio la ufyatuaji wa risasi katika Shule ya Covenant huko Nashville, nchini Marekani. Ni katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali, Pietro Parolin, Katibu wa Vatican ikielekezwa kwa Askofu wa mji huo, Askofu Joseph Mark Spalding. Papa Francisko ameufafanua mkasa huo kuwa ni kitendo cha ukatili kisicho na maana na anaungana na jamii nzima kuomboleza kwa ajili ya watoto na watu wazima waliokufa na kuwakabidhi kwa kumbatio la upendo la Bwana Yesu.

Machozi kwa ajili ya waathirika katika Shule huko Nashville
Machozi kwa ajili ya waathirika katika Shule huko Nashville

Zaidi ya hayo, Baba Mtakatifu Francisko anaomba faraja na nguvu za Roho Mtakatifu kwa ajili ya familia zinazoomboleza na kusali kwamba waimarishwe katika imani yao katika uwezo wa Bwana Mfufuka kuponya kila jeraha na waweze kuwa na wema dhidi ya uovu usioelezeka.

Watu waliwasha mishumaa katika mkesha wa kuombea marehemu waliokufa
Watu waliwasha mishumaa katika mkesha wa kuombea marehemu waliokufa

Waathirika ni sita katika shambulio hilo kweny shule ya Kikristo lililotokea mnamo terehe 27 Machi 2023 ambapo watoto watatu na watu wazima watatu walikufa. Mshambuliaji huyo alikuwa mwanafunzi wa zamani wa umri wa miaka 28, ambaye aliuawa katika mapigano ya moto na polisi. Mamlaka bado haijatoa sababu za mauaji hayo, lakini mkuu wa polisi alidaiwa kusema kwamba, kulingana na wachunguzi, msichana huyo alikuwa na chuki fulani kwa kulazimika kuhudhuria shule hiyo akiwa mtoto.

Papa ametuma rambi rambi huko Nashville,Marekani
30 March 2023, 10:00