Papa akiwa hospitalini alimbatiza mtoto mgonjwa
Na Angella rwezaula, - Vatican.
Alasiri tarehe 31 Machi 2023, Baba Mtakatifu Francisko, baada ya kujiunda katika sala katika kikanisa kidogo kilichombo katika chumba binafsi, alipokea Ekaristi. Baadaye, kama ilivyooneshwa hapo awali, alikwenda kutembelea Idara ya Sratani (Oncology) ya Watoto na Upasuaji wa (Neurosurgery) Mtoto na kumbatiza Malaika mdogo Miguel. Katika tukio hilo,pia alizungumza na wahudumu wa afya waliokuwepo, na kutoa wazo kwa wale wote wanaochangia kupunguza maradhi ya kimwili na uchungu wa wale wanaoitwa kushuhudia msalaba wa Kristo kila siku na akatoa shukrani kwa ajili yao binafsi kwa kunyima na roho yao ya utumishi.
Mwisho wa ziara yake alirudi wodini kweke. Timu ya madaktari inayomfuatilia Baba Mtakatifu Francisko , baada ya kutathmini matokeo ya vipimo vilivyofanyika siku hiyo na matokeo mazuriya kliniki, imethibitisha kuruhusiwa kwake Baba Mtakatifu kutoka Hospitalini A. Gemelli Jumamosi tarehe Mosi Aprili 2023.
Taarifa ya mapema kuhusu Papa
Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kurejea katika Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican, Jumamosi tarehe Mosi Aprili 2023, baada ya kulazwa katika hospitali ya A. Gemelli kwa ajili ya ugonjwa wa mfumo wa hewa unaoambukiza. Hayo yametangazwa katika taarifa mpya kutoka kwa Msemamaji Mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari, Vatican Dk. Matteo Bruni, akidhibitisha habari iliyokuwa imesema tangu asubuhi tarehe 31 Machi na Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Makardinali. Katika dokezo hilo msemaji wa Vatican ametoa taarifa kwamba hali yake iliendelea vizuri na kufanya matibabu yake ya kawaida ya kikliniki.
Chakula cha jioni na pizza pamoja na wale wanaomsaidia
Katika chakula cha jioni, Alhamisi tarehe 30 Machi 2023, Papa Francisko alikula pizza, pamoja na wale wanaomsaidia katika siku hizi za kulazwa hospitalini kama vile: madaktari, wauguzi, wasaidizi na wafanyakazi wa Kikosi cha Ulinzi wa kipapa pamoja na Baba Mtakatifu kwa mujibu wa Dk. Bruni. Ijumaa asubuhi tarehe 31 Machi 2023 hata hivyo, baada ya kupata kifungua kinywa, Baba Mtakatifu Francisko alisoma baadhi ya magazeti na kuanza tena kazi zake. Kwa maana hiyo "Kurudi kwa Baba Mtakatifu kwenye nyumba ya Mtakatifu Marta kunatarajiwa Jumamosi tarehe Mosi Aprili 2023 kufuatia na matokeo ya uchunguzi uliofanyika mapema asubuhi", kwa mjibu wa Dk. Bruni.
Uwepo wa Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro katika Misa ya Matawi
Tena Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican amethibitisha kwamba: “kwa vile anatarajiwa kuondoka hospitalini hapo kesho, Papa Francisko anatarajiwa kuwepo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro katika siku ya Dominika kwa ajili ya adhimisho la Ekaristi Takatifu ambayo ni Dominika ya Matawi na Mateso ya Bwana”. Kwa maana hiyo Dominika tarehe 2 Aprili ni mwanzo wa Juma Takatifu la Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwa kutanguliwa na Dominika ya Matawi.
Kauli ya madaktari
Katika suala la kuruhusiwa kutoka hospitali ya Kirumi tayari ulikuwa unatarajiwa tarehe 30 jioni, katika taarifa ya pili kwa vyombo vya habari vya Vatican, ambapo pia iliripotiwa taarifa ya wafanyakazi wa matibabu ambao wamekuwa wakimsaidia Baba Mtakatifu Francisko tangu Jumatano tarehe 29 Machi 2023 , siku ambayo alilazwa. Kwa mujibu wa wataalamu hao wa matibabu walisema kuwa: “Katika muktadha wa uchunguzi wa kimatibabu uliopangwa kwa Baba Mtakatifu, bronchitis ya kuambukiza ilipatikana ambayo ilihitaji usimamizi wa tiba ya antibiotiki kwa msingi wa infusion ambayo ilileta matokeo yaliyotarajiwa na uboreshaji wa wazi katika hali ya afya".
Tuzidi kumwombea Baba Mtakatifu afya yake itengamae!
Sasisho la mwisho ni saa 3 30 asubuhi tarehe Mosi Aprili 2023.