Tafuta

2023.03.18 Papa amekutana na vijana wa "Progetto Policoro" unaohamasishwa na Baraza la Maaskofu Italia(CEI) 2023.03.18 Papa amekutana na vijana wa "Progetto Policoro" unaohamasishwa na Baraza la Maaskofu Italia(CEI)  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Vita ni kushindwa kwa siasa&sera bora za siasa ni kuhusisha watu!

Papa akikutana na vijana wanaojishughulisha na mafunzo ya kijamii na kisiasa,ndani ya Mpango uitwa Policoro wa Baraza la Maaskofu wa Italia(CEI),amewambia kuwa leo hii siasa haina sifa bora,zaidi ya yote kwa sababu haina ufanisi na iko mbali na maisha ya watu watu.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Papa Francisko amekutana na Vijana wanaojishughulisha na mafunzo ya kijamii na kisiasa wa “Mpango uitwao Policoro” wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI), Jumamosi tarehe 18 Machi 2023, katika ukumbi wa Clementina mjini Vatican. Akianza hotuba yake alishukuru salamu walizompatia na kwamba mkutano wao unampatia fursa ya kuwatia moyo mchakato wa mafunzo ya kisiasa na kijamii ambao ni mwendelezo wa Mpango huo wa Policoro wa Kanisa la Italia. Amependa kusisitiza jukumu la huduma katika jamii na katika siasa na hata mamlaka kwa mara nyingine tena kushirikishana katika malezi ya vijana wengine. Baab Mtakatifu amesema juu ya  chaguzi zao mwaka huu zinapeleka mbele mada ya amani. Ni mada ambayo haiwezi kukosa katika mafunzo ya sera za kisiasa na ambapo kwa bahati mbaya ni ya dharura katika hali ya sasa.

Papa amekutana na vijana wa mpango wa Policoro
Papa amekutana na vijana wa mpango wa Policoro

Vita ni kushindwa kwa siasa. Kwa kusisitiza zaidi amesema “vita ni kushindwa kwa sera za kisiasa” Vinazidisha sumu ambayo inamfikiria mwingine kama adui. Vita vinatufanya tuguse kwa mkono wetu uwazimu wa mbio za silaha na matumizi yake katika migogoro.  “Fundi mmoja alinieleza kuwa ikiwa kwa mwaka mmoja hakuna silaha, njaa ingeisha ulimwenguni” Kwa hiyo inahitajika sera ya kisiasa iliyo bora ambayo inachukuwa wajibu kama ile ambayo wao wanafanya, yaani kuelimisha jamii. Huo ni uwajibikaji kwa wote. “Kufanya vita lakini vita vingine, vita vya ndani, vita vya ndani kwa ndani na kufanya kazi kwa ajili ya amani”. Papa Francisko amesisitiza.

Papa Francisko ameijiwa akilini  mwake na tukio la Biblia la Mfalme Ahabu na shamba la mizabibu la Nabothi. Mfalme alitaka kumiliki shamba la mizabibu la Nabothi, ili kupanua shamba lake; lakini Nabothi hakutaka na hakutana kuliuza, kwa sababu shamba hilo la mizabibu lilikuwa  ni urithi wa baba zake. Mfalme alikasirika na kununa kama mtoto aliyedekezwa. Kisha mke wake, Malkia Yezebeli ambaye ni ibilisi mdogo! papa amesema, alitatua tatizo hilo kwa kufanya Nabothi aondolewe kwa shtaka la uwongo, yaani auawe. Kwa hiyo Nabothi aliuawa na mfalme  kwa kuchukua shamba lake la mizabibu. Ahabu anawakilisha sera mbaya zaidi, ile ya kusonga mbele, kwa kutengeneza nafasi kwa kuua wengine, sera hii mbaya zaidi ambayo haifuatii manufaa ya wote bali maslahi fulani na inatumia kila njia kuwaridhisha. Ahabu si baba, yeye ni bwana, na utawala wake ni wa mabavu; Papa amesititiza na kuongeza. Mtakatifu Ambrose aliandika kijitabu kuhusu historia hii ya kibiblia, yenye kichwa “Shamba la Mzabibu la Nabothi”.

Vijana wa Mpango wa Policoro wa Baraza la Maaskofu Italia wakutana na Papa
Vijana wa Mpango wa Policoro wa Baraza la Maaskofu Italia wakutana na Papa

Wakati mmoja, akiwahutubia wenye nguvu, Ambrose aliandika: “Kwa nini unawafukuza wale wanaoshiriki katika mali ya asili na kudai milki ya mali asili kwa ajili yako peke yako? Dunia iliumbwa kwa ushirika kwa wote, kwa matajiri na maskini. [...] Asili haijui matajiri ni nani, yeye anayezalisha wote maskini kwa usawa. Tunapozaliwa hatuna nguo, hatuji duniani tukiwa tumebeba dhahabu na fedha. Dunia hii inatuleta ulimwenguni tukiwa uchi, inatuweka ulimwenguni tukiwa tunahitaji chakula, mavazi na vinywaji. Asili […] hutuumba sote tukiwa sawa na hutufunga sote kwa usawa katika tumbo la kaburi” (1, 2). Kazi hii ndogo lakini ni thamani ya Mtakatifu Ambrogio itakuwa muhimu kwa malezi yao. Siasa zinazotumia mamlaka kama kutawala na si kama utumishi haziwezi kuwajali, huwakanyaga maskini na hunyonya ardhi. Kama mfano mzuri wa kibiblia tunaweza kuchukua sura ya Yosefu mwana wa Yakobo.

Papa Francisko ameomba wakumbuke kwamba yeye aliuzwa utumwani na ndugu wale wale waliokuwa na wivu na kupelekwa Misri. Huko, baada ya misukosuko fulani, aliachiliwa, na akaingia katika utumishi wa Firauni na akawa kama aina ya Makamu. Yosefu hakujifanya bwana, lakini kama baba: alitunza nchi na wakati njaa ilipofika, yeye alipanga akiba ya nafaka kwa manufaa ya watu wote, hadi kufikia kwamba Farao aliwaambia watu hivi: “Fanyeni chochote atakachowaambia Yosefu”(Mwa 41:55), maneno yaleyale ambayo Maria atawaambia watumishi kwenye harusi ya Kana akimaanisha Yesu”. Yosefu  ambaye binafsi alidhulumiwa, aliuzwa na ndugu zake, hakutafuta masilahi yake mwenyewe bali yale ya watu, alilipa kibinafsi kwa manufaa ya wote, alikuwa fundi wa amani, alisuka mahusiano yenye uwezo wa kuvumbua jamii. Padre Lorenzo Milani aliandika kuwa : “Tatizo la wengine ni sawa na langu. Kuondokana na hayo yote kwa pamoja ni sera. Kujiondoa peke yako ni ubadhirifu”, kwa hiyo Papa ameongeza kusema kuwa  ni kweli na ni rahisi.

Papa akisikiliza hotuba ya mwakilishi wa vijana wa mpango wa policoro
Papa akisikiliza hotuba ya mwakilishi wa vijana wa mpango wa policoro

Mifano hii miwili ya kibiblia, mmoja ni hasi, na mwingine chanya, inatusaidia kuelewa ni hali gani ya kiroho inaweza kuchochea siasa. Papa Francisko amesema kwamba anaona vipengele viwili muhimu tu vyake: kwanza upole na kuzaa matunda. Upole ni upendo ambao unakuwa karibu na thabiti. [...] Ni njia ambayo wanaume na wanawake wajasiri na wenye nguvu zaidi wametembea nayo. Katikati ya shughuli za kisiasa, mdogo zaidi, dhaifu zaidi, maskini zaidi lazima watuguse, kwa sababu  wana haki ya kuchukua nafsi na moyo wetu (Fratelli tutti, 194). Ni uzazi unaofanywa kwa kushirikiana, kwa maono ya muda mrefu, mazungumzo, uaminifu, uelewa, kusikiliza, muda uliotumika, majibu ya haraka na si kuahirishwa. Inamaanisha kutazama siku zijazo na kuwekeza katika vizazi vijavyo; kwa hiyo ni muhimua kuanza michakato badala ya kuchukua nafasi. Hii ndiyo kanuni ya dhahabu, je, biashara yako itachukua nafasi kwako? Haifanyi kazi. Kwa kikundi chako? Haifanyi kazi. Kuchukua nafasi haifanyi kazi, michakato ya kuanza inafanya kazi. Wakati ni bora kuliko nafasi”.

Kwa kuhitimisha kwa kupendekeza maswali ambayo kila mwanasiasa mzuri anapaswa kujiuliza: “Nimeweka upendo kiasi gani katika kazi yangu? Nimewaendelezaje watu? Nimeacha alama gani kwenye maisha ya jamii? Nimejenga vifungo gani vya kweli? Je, ni nguvu gani chanya ambazo nimetoa? Nimepanda amani ya kijamii kiasi gani? Nilizalisha nini mahali nilipokabidhiwa?” (Ft 197). Wasiwasi wao usiwe  makubaliano ya uchaguzi au mafanikio binafsi, lakini kuhusisha watu, kuzalisha ujasiriamali, kuzalisha kiasi kwamba ni kufanya ndoto istawi, kufanya watu kuhisi uzuri wa kuwa mali ya jamii. Ushiriki uwe mafuta kwenye majeraha ya demokrasia. Papa amewaalika watoe mchango wao, kushiriki na kuwaalika wenzao kufanya hivyo, fanya hivyo kila wakati kwa lengo na mtindo wa huduma. Mwanasiasa ni mtumishi, wakati mwanasiasa si mtumishi ni mwanasiasa mbaya, si mwanasiasa. Amewashukuru  kwa juhudi zao. Waendelee mbele na Mama Yetu awasindikize. Amewabariki kutoka moyoni mwake, na amewaomba wamwombee.

Papa akutana na vijana wa Mpango wa Policoro wa CEI
18 March 2023, 16:40