Tafuta

Utafiti unaonesha matatizo ambayo wanawake bado wanakutana nao ili kufikia nafasi ya ngazi ya juu katika ulimwengu wa kazi. Utafiti unaonesha matatizo ambayo wanawake bado wanakutana nao ili kufikia nafasi ya ngazi ya juu katika ulimwengu wa kazi. 

Papa:usawa katika utofauti kati ya wanaume na wanawake unafanya dunia kuwa bora

Tunachapisha dibaji ya Papa Francisko kwenye kitabu cha“Uongozi zaidi wa kike kwa ulimwengu bora:kujali kama injini ya nyumba yetu ya pamoja”,kilichohaririwa na Anna Maria Tarantola na kuchapishwa na “Vita e Pensiero”.Maandishi hayo ni matokeo ya utafiti uliohamasishwa kwa pamoja na Taasisi ya Centesimus Annus Pro Pontifice na Muungano wa Kimkakati wa Vyuo Vikuu vya Utafiti vya Kikatoliki (Sacru).

Papa Francisko

Kitabu hiki kinazungumza juu ya wanawake, talanta zao, uwezo wao na majukumu na ukosefu wa usawa, vurugu na hukumu ambazo bado zinajieleza katika ulimwengu wa kike. Masuala yanayohusu ulimwengu wa kike yamo kwa namna ya pekee moyoni mwangu. Katika hotuba zangu nyingi, nimewarejea nikisisitiza ni kiasi gani  bado kinapaswa kufanywa kwa ajili ya maendeleo kamili ya wanawake. Nimekuwa na fursa kati ya mingine ya kuthibitisha kuwa “Mwanaume na mwanamke si sawa na si bora kuliko kila mmoja, hapana. Ni mwanaume huyo tu ambaye haweza kuleta maelewano, bali ni mwanamke analeta maelewano ambayo yanatufundisha kubembeleza, kupenda kwa upole na ambayo hufanya ulimwengu kuwa kitu kizuri.(Mahubiri katika nyumba ya Mtakatifu Marta, 9 Februari 2017). Tuna haja sana ya maelewano ili kupambania ukosefu wa haki, tamaa kipofu ambazo zinadhulu watu na mazingira, vita visivyo haki na havikubaliwi.

Kitabu hiki kinakusanya matokeo ya utafiti wa pamoja, uliohamasishwa na Mfuko wa Cntesimus Annus pro Potefice na Mkakati wa Umoja wa utafiti vya vyuo vikuu katoliki ambao waishiriki wasomi 15 kutoka fani mbalimbali za vyuo vikuu 10 vinavyoishi katika nchi 8. Ninapenda kuwa mada inashughulikiwa kutoka kwa mtazamo wa taaluma nyingi, njia tofauti na uchambuzi huruhusu maono mapana ya shida na utafutaji wa suluhisho bora. Utafiti unaonesha matatizo ambayo wanawake bado wanakutana ili kufikia nafasi ya ngazi ya  juu katika ulimwengu wa kazi na wakati huo huo, faida zinazosukana na uwepo wake kwa wingi na thamani kamili katika muktadha wa uchumi, kisiasa na katika jamii yenyewe.

Hata Kanisa linaweza kujivunia na thamani ya wanawake: kama nilivyosema kwenye hotuba ya kuhitimisha Sinodi ya Maaskofu wa Kanda ya Amazonia mwezi Oktoba 2019: “ Hatukuweza kuzingatia nini maana ya mwanamke katika Kanisa na tunaishia tu katika sehemu ya kazi (…). Lakini nafasi ya mwanamke katika Kanisa inakwenda mbali zaidi ya kazi. Na katika hilo kuna haja ya kuendelea kuifanyia kazi. Mbali zaidi. Haiwezekani kuendelea katika ulimwengu bora, haki zaidi, jumuishi na fungamani endelevu bila uhusiano na wanawake. Na tazama kwamba tunapaswa kufanya kazi, wote pamoja, kwa ajili ya kufungua fursa, zinazofanana na wanaume na wanawake kwa kila muktadha kwa ajili ya kufuata msimamo na hali ya kudumu kuanzia na usawa katika utofauti kwa sababu njia ya kuthibitisha ya kike ambayo ni ya hivi karibuni ni shida na kwa bahati mbaya, sio dhahiri. Inawezekana kwa urahisi kurudi nyuma. Fikra za wanawake ni tofauti na za wanaume, huwa makini zaidi na ulinzi wa mazingira, mtazamo wao haulengi  yaliyopita bali yajayo. Wanawake wanajua kuwa wanajifungua kwa uchungu ili kufikia furaha kubwa: kutoa maisha na kufungua upeo mpya.

Kwa maana hiyo wanawake wanataka amani, daima. Wanawake wanajua kujieleza pamoja na nguvu na huruma, wana akili, washindani, waliojiandaa, wanajua kuhuisha vizazi vipya (si kwa watoto  tu). Ni haki kwamba wanaweza kujieleza uwezo wao huo kwa kila  muktadha, si tu ule wa kifamilia, ambao unapaswa kuonekana unaofanana na wanaume katika nafasi, bidii na uwajibikaji. Mapungufu ambayo bado yapo ni dhuluma kubwa. Mapengo haya, pamoja na chuki dhidi ya wanawake ndiyo chanzo cha ukatili dhidi ya wanawake. Mara nyingi nimelaani jambo hili; mnamo tarehe 22 Septemba 2021 nilisema kuwa unyanyasaji dhidi ya wanawake ni janga la wazi linalotokana na utamaduni wa ukandamizaji wa mfumo dume na wa kiume. Lazima tutafute dawa ya kutibu janga hili, tusiwaache wanawake peke yao.

Utafiti uliowakilishwa na hitimisho lililofikiwa unatafuta kuponesha jeraha la ukosefu wa usawa na kwa njia hiyo ya vurugu. Ninapenda kufikiria kuwa ikiwa wanawake wangeweza kufurahia usawa kamili wa fursa, ingewezekana kuchangia kimsingi ulazima wa mabadiliko kuelekea ulimwengu wa amani, jumuishi, mshikamano na uendelevu fungamani. Kama nilivyothibitisha katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake mnamo tarehe 8 Machi 2019, wanawake wanafanya ulimwengu kuwa mzuri , wanaulinda na kuhuisha. Wanapeleka neema ya upyaisho, mkumbatio wa kujumuisha na ujasiri wa kujitoa wenyewe. Amani, basi, huzaliwa na wanawake, hujitokeza na kuwashwa tenana huruma ya wa mama. Kwa hiyo ndoto ya amani inatimia unapo watazama wanawake. Ni mawazo yangu kwamba, kama inavyojitokeza katika utafiti, usawa lazima upatikane katika utofauti. Sio usawa, kwa sababu wanawake wana tabia kama wanaume, lakini ni usawa kwa sababu milango ya uwanja iko wazi kwa wachezaji wote, bila tofauti za jinsia (na pia rangi, dini, utamaduni…). Hii ndio wanauchumi wanaita utofauti bora. Inapendeza kufikiria ulimwengu ambapo kila mtu anaishi kwa upatanisho na kila mtu anaweza kuona vipaji vyao vikitambuliwa na kuchangia katika uundaji wa ulimwengu bora.

Uwezo wa kutunza kwa mfano bilashaka kuna tabia ya kike ambayo inapaswa kujieleza si tu katika muktadha wa familia lakini katika kipimo cha usawa na kwa matokeo mazuri hata katika siasa, uchumi, elimu na juu ya kazi. Uwezo wa kutunza lazima ujieleze kwa wote wanawake na wanaume. Wanaume wanaweza kukuza uwezo huu hata katika shughuli za wazazi. Ni uzuri gani ambao familia kwa pamoja na wazazi mama na baba wote wanatunza watoto wao, wanawasaidia kukua vizuri na kuwaelimisha kwa heshima watoto wao mambo ya ukarimu, huruma na kulinda kazi ya uumbaji. Ninapenda hata kutaja kidogo umuhimu wa elimu. Elimu ni njia mwalimu, kwa upande mmoja kwa ajili ya kuwapatia wanawake ushindani na ufahamu wa lazima kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mpya za ulimwengu wa kazi,na kwa upande mwingine, kurahisisha mabadiliko ya utamaduni wa kimfumo dume ambao bado unatawala. Kwa bahati mbaya bado leo hii karibu milioni 130 ya wasichana ulimwenguni hawaendi shule. Hakuna uhuru, haki, maendeleo fungamani, demokraisia na amani bila elimu.

Dibaji ya Papa katika kitabu
08 Machi 2023, 09:40