Papa:unabii na ubunifu zinahitajika kwa ajili ya amani katika Ulaya
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Papa Francisko Alhamisi tarehe 23 Machi 203 ameshirikisha ndoto zake mbili kuu za waanzilishi wa Ulaya kwa Tume ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya (COMECE) ambayo imemchagua hata Askofu Mariano Crociata kuwa kama rais mpya. Kwa hiyo ndoto ya kwanza ya Papa kwa ajili ya umoja na amani ameilezwa ni jinsi gani ilivyo ngumu kuilewa leo hii. Umoja ni suala la kwanza, ambalo ni muhimu kutaja kwamba umoja wa Ulaya hauwezi kuwa umoja, kamili lakini kinyume chake lazima we umoja unaoheshimu na kuthamini umoja, sifa za watu na tamaduni zinazounda.
Umoja katika utofauti na kazi ya Kanisa
Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka waanzilishi wa Umoja wa Ulaya ambao ni “De Gasperi na Spinelli kutoka Italia, Monnet na Schuman kutoka Ufaransa, Adenauer kutoka Ujerumani, Spaak kutoka Ubelgiji, Beck kutoka Luxembourg na katika mataifa na tamaduni tofauti na kusisitiza kwamba utajiri wa Ulaya upo katika muunganiko wa vyanzo mbalimbali vya mawazo na uzoefu wa kihistoria, lakini ametoa onyo kwamba “Ulaya ina mustakabali ikiwa kweli ni muungano na sio kupunguzwa kwa nchi zenye sifa zao.” Changamoto hii hasa ni ile ya umoja katika utofauti.
Na inawezekana ikiwa kuna msukumo wenye nguvu; la sivyo kifaa kinatawala, dhana ya kiteknolojia inatawala, ambayo hata hivyo haina matunda kwa sababu haisisimui watu, haivutii vizazi vipya, haihusishi nguvu hai za jamii katika ujenzi wa mpango wa pamoja. Katika changamoto hii, kazi ya Kanisa, Papa Francisko amebainisha kuwa ni kuwafundisha watu ambao kwa kusoma alama za nyakati, wanajua kutafsiri mpango wa Ulaya katika historia ya leo”.
Kujitolewa kwa ajili ya umoja kwa amani kunahitajika
Akizungumzia juu ya kuishi pamoja kwa amani, Papa Francisko amesisitiza haja ya kujitolea zaidi kwa upande wa nchi mbalimbali hasa kwa ajili ya amani. Kwa hiyo amesema kwamba historia ya leo inahitaji wanaume na wanawake kuhuishwa na ndoto ya Umoja wa Ulaya katika huduma ya amani. Papa hakukosa kukumbuka kwamba leo tunaweza sasa kuzungumza juu ya vita vya tatu vya dunia na kwamba vita vya Ukraine vimetikisa amani ya Ulaya. Kwa hiyoamesisitiza anavyoona mataifa jirani yamefanya yote yawezayo kuwakaribisha wakimbizi na kwambawatu wote wa Ulaya wanashiriki katika ahadi ya mshikamano na watu wa Ukraine lakini pamoja na mwitikio huu wa kwaya juu ya kiwango cha hisani inapaswa kuendana ,hata kama si rahisi na dhahiri, dhamira ya kushikamana kwa amani.
Baba Mtakatifu Francisko aidha amefafanua kuwa ni changamoto tata sana, kwa kuwa nchi za Umoja wa Ulaya zinahusika katika ushirikiano, maslahi, mikakati, mfululizo wa nguvu ambazo ni vigumu kuleta pamoja katika mradi mmoja, ambao lazima ukataa vita. Vita haviwezi na havipaswi kuonekana tena kama suluhisho la migogoro. Ikiwa nchi za Ulaya leo hazishiriki kanuni hii ya kimaadili-kisiasa, basi ina maana kwamba wameondoka kwenye ndoto ya awali. Ikiwa, kwa upande mwingine, wanashiriki, lazima wajitolee kutekeleza, kwa juhudi zote na utata ambao hali ya kihistoria inahitaji. Kwa sababu vita ni kushindwa kwa siasa na ubinadamu. Inabidi turudie haya kwa wanasiasa.
Jukumu la Comece
Comece pia, kwa asili ni daraja kati ya Makanisa katika Ulaya na taasisi za Muungano, kwa kujenga mahusiano, kukutana na mazungumzo, hufanya kazi kwa ajili ya amani, amesisitiza hilo Papa ambaye pia amejiuliza juu ya unabii, kuona mbele na ubunifu kufanya kuendeleza mambo ya amani. Ni uwanja wa kazi ya ujenzi, aambao unahitaji wasanifu na mafundi, amehitimisha Baba Mtakatifu Francisko.