Tafuta

Papa:Pande zote mbili ziheshimu maeneo ya kidini na Kanisa la Italia lilifanya maombi kwa ajili ya Ukraine Papa:Pande zote mbili ziheshimu maeneo ya kidini na Kanisa la Italia lilifanya maombi kwa ajili ya Ukraine 

Papa,Ukraine:Pande zote mbili ziheshimu maeneo ya kidini

amekubuka tena watu wa Ukraine na umuhimu watawa wa kiorthodox nchini humo.Ameonesha ukaribu nchini Malawi,iliyozidiwa na kimbunga Freddy kilichosababisha waathirika wapatao 130:“Ninawaombea marehemu,waliojeruhiwa na waliohamishwa.Mungu awasaidie familia na jamii zilizojaribiwa zaidi na msiba huu".

Na Angella Rwezauala- Vatican.

Mwishoni mwa Katekesi ya Papa Jumatano 15 machi 2023 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko amewakabidhi kwa Mama Maria mfariji kwa walioteswa na Malkia wa Amani watu waliouawa waathirika  wa uchokozi wa Urussi. “Leo, ninaomba pande zinazopigana ziheshimu maeneo ya kidini” Mawazo yake Papa hasa  yamewaendea pia kwa watawa wa Kiorthodox wa Kyiv Lavra lakini pia wengine wa madhehebu yote kwamba  wote wanahitaji msaada watu waliowekwa wakfu na kila msaada wa Watu wa Mungu.”

Kimbunga nchini Malawi

Mtazamo wa Papa umehamia Malawi, nchi iliyokumbwa na kimbunga cha kitropiki kiitwacho Freddy ambacho katika muda majuma matatu kilisababisha vifo vya watu 130, hasa kuathiri jiji la Blantyre na kusababisha njia ya uharibifu na machafuko. “Ninawaombea marehemu, waliojeruhiwa na waliohamishwa. Mungu awasaidie familia na jamii zilizojaribiwa zaidi na msiba huu”.

Shukrani kwa viongozi wa Argentina

Hatimaye, wakati wa salamu za lugha mbalimbali, Papa akiwahutubia waamini na mahujaji wa Uhispania, anaongeza shukrani zake kwa wanasiasa na viongozi wa kijamii wa Argentina waliomtumia barua ya kumtakia heri kwa miaka kumi ya Upapa wake, iliyoadhimishwa tarehe 13 Machi 2023. Umoja uleule uliooneshwa katika kuandika barua, ndio matakwa ya Baba Mtakatifu,  kwamba ingekuwa vyema kuudumisha katika maisha na kazi za kila siku, ili kufanya mazungumzo na kuendeleza taifa kwa pamoja. “Asante kwa ishara hii. Inatokea kwangu kuwaambia kama vile mlivyokusanyika kusaini barua hii,  ni vyema kukusanyika kuzungumza, kujadili na kuipeleka nchi mbele”.

Katekesi na wito kwa Ukraine na Malawi
15 March 2023, 17:10