Papa:Nipe maji ya kunywa ni kilio cha kaka na dada wanaokosa maji ili waishi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Dominika hii, Injili inatuwakilisha mikutano mizuri zaidi na ya kustaajabisha ya Yesu kama ule wa Msamaria (Yh 4,5-42). Yesu na wanafunzi wake walipumzika karibu na kisima huko Samaria. Akafika mwanamke na Yesu akamwambia “naomba maji ya kunywa”. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko ameanza tafakari yake, Dominika tarehe 12 Machi 2023, kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, kwa mahujaji na waamini waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro jijini Vatican. Akiendelea ametaka kujikita kuhusu na sentensi ya: “ Nipe maji ya kunywa”. Baba Mtakatifu amesema “Tukio hili la Yesu linatuonesha kiu na kuchoka, na ambaye anajifanya kukutana katika kisima na msamaria wakati wa saa za jua kali, yaani saa sita, na ni kama anayeomba kupumzishwa. Hii ni picha ya kujishusha kwa Mungu, kwa sababu katika Yesu, Mungu alijifanya kuwa kama mmoja wetu, mwenye kiu kama sisi, anayeteseka kama sisi”. Kwa hiyo tutafakari tukio hilo, kwa kila mmoja ambaye anaweza kusema kwamba: “Bwana, Mwalimu ambaye anazungumza ananiomba maji ya kunywa.
Baba Mtakatifu amesema kwamba Yeye kwa hiyo anayo kiu kama mimi. Yeye yuko karibu nami kweli, Bwana! Unajihusisha na umaskini wangu… umeniinua kutoka chini, kutoka chini kabisa yangu binafsi, mahali ambapo hakuna anayeweza kunifikia. Kiu ya Yesu kiukweli sio ya kimwili tu, kwa sababu inadhihirisha kiu kuu ya maisha yetu na hasa kiu ya upendo wetu. Na inajitokeza katika hatima ya mateso, juu ya msalaba. Hapo kabla ya kufa Yesu atasema :“Nina kiu” (Yh 19,28). Baba Mtakatifu aidha amesema kuwa “Lakini Bwana anayeomba maji ya kunywa ndiye ambaye anatoa maji ya kunywa. Akikutana na msamaria alizungumza juu ya maji ya uzima yatokanayo na Roho Mtakatifu,na kutoka katika msalaba yanabubujika katoka ubavuni mwake uliochomwa na mkuki na kutoka damu na maji (Yh 19,34). Yesu mwenye kiu ya upendo, anatuponesha kiu ya upendo. Na anafanya hivyo na sisi kama Msamaria. Kwa sababu anakuja kukutana na kila siku yetu, kushirikisha kiu yetu, na anatuhaidi maji ya uzima ambayo hutupatia uzima wa milele (Yh 4,14).
Nipe maji ya Kunywa. Baba Mtakatifu anasema kuwa kuna mantiki ya pili. Katika maneno hayo sii tu Yesu anaomba msamaria, lakini ni wito ambao mara nyingi wa ukimya, ambao kila siku unatugeukia na kutuomba kutunza kiu za wengine. Nipe maji ya kunywa inatwambia kuwa ni watu wangapi katika familia, katika nafasi za kazi na mahali pengine tunapokuwa, wana kiu ya kupata ukaribu, umakini na kusikilizwa; anatueleza kuwa mwenye kiu ya Neno la Mungu ana haja ya kupata katika Kanisa, kile kijito cha kuweza kunywea. Kwa hiyo “Nipe maji ya kunywa” ni wito katika jamii zetu, mahali ambapo haraka nyingi, mbio za matumizi na kutojali. Kunazalisha ukame na utupu wa ndani. Na hivyo tusisahau kuwa nipe maji ya kunywa ni kilio cha kaka na dada wengi wanaokosa maji ili waishi, wakati inaendelea hali ya uchafuzi na kuharibu nyumba yetu ya pamoja; na hata hiyo imechoka na ina kiu.
Baba Mtakatifu Francisko amesema, kwamba mbele ya changamoto hizi, Injili ya leo inatupatia kila mmoja wetu maji ya uzima ambayo yanaweza kugeuka kuwa kisima cha kunywea wengine. Na kwa hiyo kama msamaria, aliyeacha mtungi wake katika kisima na kukumbia kuwaita watu katika kijiji (Yh 4, 28) hata sisi tusitajifikirie kujitosheleza wenyewe tena kiu yetu, badala yake kwa furaha ya kukutana na Bwana tunaweza kuwaondolea kiu wengine; Mungu aliyetuponesha kiu, anaendelea kutuponesha na tutaweza kujua kiu yao na kushirikisha upendo ambao Yeye aliotupatia. “ Ninaijiwa swali hili, mimi na ninyi: je tuna uwezo wa kujua kiu ya wengine , kiu ya watu, kiu ya wanafamilia wangu na kwa kuongeza Papa amesema, kwa hiyo basi leo hii, tunaweza kujiuliza: “Je mimi nina kiu ya Mungu,na ninataka kutambua kwamba ninahitaji upendo wake kama yale maji ya kuweza kuishi? Na kadiri mimi ninavyopona kiu ndivyo ninahangaikia kiu ya wengine? Kiu ya kimwili na kiu ya kiroho? Mama Maria atuombee na kutusaidia katika safari yetu", Papa amehitimisha.