Papa:Masaa 24 ya sala kwa Bwana,tuombe amani,Bwana anasikiliza sala zetu!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 12 Machi 2023 Baba Mtakatifu Francisko amesema; anawasalimia waroma, mahujaji wengi kutoka nchi mbali mbali na hasa waliotoka Madrid na Spalato. Makundi ya Parokia kutoka Padova, Caerano Mtakatifu Marco, Bagolino, Formia na Mtakatifu Ireneo, Roma.
Massa 24 kwa ajili ya Bwana
Baba Mtakatifu ametoa taarifa kuwa Ijumaa taarehe 17 na Jumamosi 18 Machi 2023 Kanisa zima litapyaisha mpango wa Masaa 24 kwa ajili ya Bwana”. Kwa hiyo "ni wakati uliowekwa kwa ajili ya sala ya kuabudu na sakramenti ya Upatanisho". Katika Siku ya Ijumaa alasiri Baba Mtakatifu anatarajia kwenda katika parokia ya Kirumi kwa ajili ya maadhimisho ya toba.
Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa "Mwaka mmoja uliopita, katika muktadha kama huo walifanya Tendo zito la Kuweka wakfu kwa Moyo Safi wa Maria, huku tukiomba zawadi ya amani. Dhamana yetu haishindwi, tumaini haliyumbishwi! Bwana daima husikiliza maombi ambayo watu wake wanamwambia kwa maombezi ya Mama. Tunabaki kuwa na umoja katika imani na mshikamano na ndugu zetu wanaoteseka kwa sababu ya vita”, Papa amesema. Kwa kuongeza: “Zaidi ya yote, msisahau watu wa Kiukraine waliouawa!" Na hatimaye amewatakia Dominika njema,na tafadhali wasisaha kusali kwa ajili yake.