Papa kwa watawa wa Kibudha wa Taiwan:Hija ya kielimu ni muhimu katika kukutana
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 16 Machi 2023, amekutana mjini Vatican na wanachama zaidi ya mia moja wa Umoja wa Umoja wa Ubudha wa Kibinadamu, kutoka Taiwan na wajumbe wakatoliki zaidi ya miako ameonesha furaha ya kuwakaribisha kama wawakilishi wa kibudha pamoja na Wajumbe wa Kanisa Katoliki. Uwepo wao leo hii unashuhudia, roho ya urafiki na kushirikisha ambako kunakuza kama waamini msimamo uliosimikwa katika mchakato kwa wote ya kidini. Mkutano wao umekuja siku chache baada ya kifo cha Mwalimu Hsing Yun, ambaye ni Mwanzishili wa Monasteri ya Fo Guang Sham. Yeye anajulikana sana ulimwenguni kwa mchango wake wa Kibinadamu, yeye pia alikuwa mwalimu wa makaribisho ya kidini.
Papa Francisko amesema kwamba, ziara yao ambayo wamejieleza kama hija ya kielimu, inawakilisha fursa muhimu kwa ajili ya kuendeleza utamaduni wa kukutana ambapo kwa sasa wote tunajikuta katika hatari ya kutojifunguliwa wengine, kwa kuaminiana na kugundua katika wao urafiki wa kaka na dada, na kwa namna hiyo kujifunza kujigundua sisi wenyewe binafsi. Kwa hakika kwa kufanya uzoefu na wengine katika utofauti ni wazi kwamba tunatiwa moyo wa kutoka ndani mwetu na kukubali huku kukikumbatia tofauti zetu. Baba Mtakatifu amesema kuwa hija ya kielimu inaweza kuwa kisima cha utajiri mkubwa na kutoka fursa nyingi za kukutana, kwa kujifunza mmoja na mwingine na kuthamanisha uzoefu wetu tofauti. Utamaduni wa kukutana unajenga madaraja na kufungua madirisha juu ya thamani takatifu na misingi ambayo inasaidia wengine.
Utamaduni kukutana unaangusha kuta ambazo zinagawana watu na kuwaweka mateka wa dhana, chuki au kutojali. Hija ya kielimu, katika maeneo matakatifu ya kidini, kama ile wanayojikita nayo, inaweza pia kuboresha uthamini wetu wa upekee wa njia yake Mungu. Kazi nzuri ya sasa ya kisanii ambayo inatuzunguka jijini Vatican na Roma yote, Papa ameongeza kusema kuwa, inaangazia kukubali kwamba katika Yesu Kristo, Mungu mwenyewe alijifanya mhujaji katika ulimwengu kwa ajili ya upendo wa familia yetu ya binadamu. Kwa Wakristo, Mungu alijifanya kuwa mmoja kati yetu katika ubinadamu wa Yesu anayeendelea kutupeleka katika hija ya utakatifu, shukrani ambamo tunaweza kupata na kukua katika mfanano na Yeye na kugeuka hivyo kwa mujibu wa maneno ya Mtakatifu Petro “ili mpate kuwa washirika wa asili ya kimungu, (2 Pt 1,4).
Katika mchakato wa kihistoria, waamini waliunda kipindi na nafasi takatifu kama kijito cha kukutana, mahali ambapo wanaume na wanawakwe wanaweza kuchukua mifano ya lazima ili kuishi kwa hekima na wema. Katika mtindo huo, wao wanachangia mtindo wa elimu fungamani ya binadamu, kwa kuhusisha “kichwa, mikono, moyo na roho” na kupeleka hivyo kufanya uzoefu wa maelewano fungamani ya binadamu, yaani uzuri wote katika maelewano haya (Mkutano kuhusu Mapatano ya Kielimu“Dini na Elimu,5 Oktoba 2021). Maeneo hayo ya mikutano bado ni muhimu zaidi katika wakati wetu, ambao unaendelea kuona michaniko ya mabadiliko ya kibinadamu na sayari na kuunganisha leo hii, tamu tamu za kina za maisha na kazi (Laudato si 18). Hali halisi hii inaonekana hata katika maisha na juu ya utamaduni wa dini na kutambua kuwa na mafunzo yanayofanywa na elimu kwa vijana kuhusu ukweli bila wakati na mitindo muhimu ya shauku ya sala na ujenzi wa amani.
Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa hii ni muhimu kuona kwa mara nyingine tena kwamba “daima dini zimepata uhusiano wa kina na elimu, kwa kusindikiza shughuli za kidini na zile za elimu, shuleni na taaluma za juu. Kama ilivyokuwa wakati uliopita, hata leo hii, kwa hekima na ubinadamu katika tamaduni zetu za dini, tunataka kutoa chachu kwa ajili ya upyaishaji wa matendo ya kielimu ambayo yanaweza kukuza katika ulimwengu udugu wa ubinadamu” (Dini na Elimu 5 Oktoba 2021). Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu Francisko anawatakia kila jema kwamba hija hiyo ya kielimu iwafikishe, na kuwaongoza na wazo la mwalimu wao wa kiroho Budha, katika mkutano wa kina zaidi wao binafsi na kwa wengine na tamaduni ya kikristo na uzuri wa dunia na nyumba yetu ya pamoja. Ziara yao jijini Roma iweze kuwa tajiri ya vipindi vya mkutano wa dhati, ambao unaweza kugeuka kwa namna moja au nyinge wenye thamani na fursa ya ukuaji katika utambuzi, hekima, majadiliano na uelewa.