Tafuta

Papa Francisko hakusahau kusali kwa ajili ya watu wa Ukraine. Papa Francisko hakusahau kusali kwa ajili ya watu wa Ukraine.  (ANSA)

Papa:kwa maombezi ya Mt.Josephat,Bwana awape amani watu wa Ukraine waliouawa

“Wapendwa,ninapongeza juhudi zenu za kuwakaribisha wenzenu waliokimbia vita.Bwana,kwa maombezi ya Mtakatifu Josephat, awape amani watu wa Ukraine waliuawa”.Ni maneno ya Papa aliyowalekeza watu wa Milano waliokaribishwa watu wa Ukraine ambao wamefika Roma kuadhimisha miaka 400 tangu kifodini cha Askofu Josephat

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika salamu zake amewakumbuka waroma na wanahija wa Italia na sehemu mbali mbali za nchi. Kwa namna ya pekee amesalimia jumuiya ya Kiukrane ya Milano, ambao wamefika katika tukio la kuadhimisha miaka 400 tangu  kuuawa kwa Askofu, Mtakatifu Josephat, ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya Umoja wa Kikristo. “Wapendwa, ninapongeza juhudi zenu za kuwakaribisha wenzenu waliokimbia vita. Bwana, kwa maombezi ya Mtakatifu Josephat, awape amani watu wa Ukraine waliouawa”.

Makundi mbali mbali ya mahujaji
Makundi mbali mbali ya mahujaji

Baba Mtakatifu akiendelea na salamu zake: Ninawasalimu mahujaji kutoka Lithuania, pamoja na jumuiya ya Kilithuania ya Roma, ambao wanaadhimisha Mtakatifu Casimir; pamoja na jumuiya ya Kikatoliki ya Romania ya Zaragoza (Hispania) na vikundi vya parokia vilivyotoka Murcia na Jerez ya  Frontera (Hispania), na kutoka Tbilisi (Georgia).

Kundi la waamini na mahujaji kutoka Burkina Faso
Kundi la waamini na mahujaji kutoka Burkina Faso

Kadhalia Baba Mtakatifu amewasalima waamini wa Burkina Faso, wanakipaimara  wa Scandicci na Anzio, waamini wa Capaci, Ostia na Mtakatifu Mauro Abate huko Roma. Hatimaye amewasalimia wote akiwatakia Dominika njema. “Tafadhali msimasahau kusali kwa ajili yangu. Mlo mwema na kwaheri ya kuonana”.

Papa Francisko ametoa wito wake mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana
05 March 2023, 15:00