Tafuta

Siku ya kumpongeza Papa na kumtakia heri ya kutumiza miaka kumi tangu kuchaguliwa kwake Siku ya kumpongeza Papa na kumtakia heri ya kutumiza miaka kumi tangu kuchaguliwa kwake 

Papa:kwa ajili ya miaka kumi ya upapa nizawadieni amani

Papa anasimulia katika podicast iliyotolewa na vyombo vya habari vya Vatican katika kuadhimisha miaka kumi ya upapa wake:“Sikufikiri ningekuwa Papa wakati wa Vita Kuu ya Tatu.Na wakati mzuri zaidi?Ni ule wa mkutano na wazee katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.Kuhusu vita hapendi kuona watoto wanakufa kutokana na migogoro.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika fursa hii ya kutimiza miaka 10 tangu Papa Francisko alipochaguliwa mnamo 13 Maci 2013, waandishi wetu wa Vatican walitayarisha mazungumzo kati yao yaliyofayika katika makao ya Papa alasili  huko Mtakatifu Marta. Haya hata hivyo hayakuwa  mahojiano, kwa sababu tayari kulikuwa na mengi yanayohusiana na tukio hilo. Lakini ilikuwa ni mawazo yanayofanya kuwa mfululizo wa kipindi cha kina cha kikanisa, cha upapa wake. Kwa miaka kumi, aliishi katika “mvutano”, anlisema, katika wakati ambao ni mkubwa zaidi kuliko nafasi na ambao umeona kukutana, safari, nyuso zikibadilishana. Waandishi walipofika walimkuta Papa Francisko akisubiri amesimama mlangoni, akiwa ameshikilia fimbo yake. Alitabasamu mbele ya vipaza sauti vyenye nembo ya vyombo vya habari vya Vatican na kuuliza “ni nini maana ya “Popecast?  baada ya kueleza maana yake alijibu "Ni nzuri basi na tufanye”.

Kwa hivyo swali la kwanza lilikuwa ni jinsi gani anavyohisi kushirikishana na ulimwengu katika wakati huu wa hatua hii muhimu kwa ajili ya maisha na huduma yake. Akijibu alisema " Muda unaendelea. Kupitia na unakwenda kwa haraka. Na unapotaka kukamata ya leo hii, tayari imeshakuwa jana. Kuishi  namna hii ni mapya. Miaka hii kumi imekuwa hivyo ya mvutano, kuishi katika mvuto

Kati ya maelfu ya katekesi, kati ya mamia ya ziara za majimbo na parokia na kati ya ziara arobaini za kitume katika kila kona ya dunia, Papa anaweka moyoni mwake kumbukumbu sahihi. Anautambulisha kama “wakati mzuri zaidi”: “Mkutano katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na wazee”, yaani, watazamaji na babu kutoka duniani kote tarehe 28 Septemba 2014.  Papa alisema kuwa “Wazee ni hekima na wananisaidia sana. Mimi ni mzee pia, sawa? Kwa upande mwingine, kulikuwa na nyakati mbaya kadhaa na zote zinazohusiana na hofu ya vita. Kwanza ziara za makaburi ya kijeshi ya Redipuglia na Anzio, ukumbusho wa kufika kwa wanajeshi huko Normandy, kisha mkesha wa kuepusha vita nchini Siria na sasa unyama ambao umeendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja nchini Ukraine. “Nyuma ya vita kuna sekta ya silaha, hii ni ya kishetani”, alisema Papa Francisko.

Swali jingine lilikuwa  kama Askofu kutoka mwisho wa dunia, ambaye hakutarajia kuwa Papa ambaye aliongoza Kanisa la ulimwengu wote wakati wa Vita vya Kidunia vya Tatu alijubu: "Sikutarajia kwamba ... nilifikiri Siria ilikuwa kitu cha pekee, kisha wengine wakafika”. Ninaumia kuona watu waliokufa na wanaokufa Warussi na Waukraine, sijali kwa maana hawa hawarudi tena. Ni vigumu. Jorge Mario Bergoglio hana shaka, kwa hivyo, juu ya nini cha kuomba ulimwengu kama zawadi kwa kumbukumbu hii muhimu: ambapo amesema “Amani, tunahitaji amani.” Kwa hivyo, maneno matatu ambayo yanalingana na "ndoto tatu za Papa” kwa Kanisa, kwa ulimwengu na kwa wale wanaotawala ulimwengu, kwa wanadamu. Udugu, machozi, tabasamu ...

Popecast: Miaka Kumi ya Upapa wa Papa Francisko
13 March 2023, 12:53