Tafuta

2023.02.28  Kitabu cha Kardinali Lazzaro You Heung-Sik. 2023.02.28 Kitabu cha Kardinali Lazzaro You Heung-Sik. 

Dibaji ya Papa:"Lazzaro You Heung-sik.Kama radi itokayo Mashariki"

Kutokana na kuamini,kunako jionesha katika kurasa hizi ambamo inaonekana kusukana mambo ya wasifu na tafakari za kiroho na kichungaji,Kardinali Lazaro anaibua nje sura ya imani iliyozaliwa kutokana na kukutana bila kuchoka na Neno la Mungu na kwa ushuhuda wa Injili:Ni katika dibaji ya Papa Francisko katika kitabu.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baada ya kusubiri kwa miaka mingi ya faraja ya Bwana, mzee Simeoni alimtambua Mtoto Masiha aliyetumwa na Mungu. Kwa kumchukua katika mikono yake na alimbariki Mungu kwa moyo wa hisia, kwa kumtambua yule Mtoto mwanga wa wokovu ambao ulikuwa unasubiliwa na watu (Lk 2,30-31). Yesu ni mwanga aliyetumwa na Baba katika usiku wa giza wa ubinadamu. Ni yeye machweo ambaye Mungu alipenda achomoze wakati watu walikuwa wakitembea katika giza. Ni Yeye ambaye alifungua milango ya matumaini mahali ambamo tulikuwa tumepotea, kuangazia pembe za mbali za dunia na mifereji ya mioyo yetu iliyovunjika,  na mioyo iliyojeruhiwa. Ni yeye yule mwanga asili wa Uumbaji ambao sasa unaangaza katikati yetu ili kuweza kufukuza giza la maisha yetu. Ndiyo utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko kwenye kitabu kilicho haririwa na Francesco Constino chenye kichwa. "Lazzaro You Heung-sik. “Kama radi itokayo Mashariki” kilichochapishwa tarehe Mosi Machi 2023. 

Baba Mtakatifu katika dibaji hiyo anaeleza kuwa Yesu ni mwanga wa Ulimwengu (Yh 8,12)kwa hiyo hata wakati mwingine tunapozunguka katika giza na kukosa maono, kwetu sisi daima kuna tumaini. Hiyo ni kwa sababu daima tunaweza kwenda kwake kupaza sauti kama kipofu Bartimeo na kupokea kutoka kwa Yesu mtazamo mpya na unaoangaza. Kwa kuongoza na tumaini hili, Kanisa  katika utamaduni wake wa kitaalimungu na kiliturujia, lilitaka daima kuelekeza Mashariki na pale tunaitwa kutazama, kwa sababu kutoka Mashariki, mwanga unachomoza  jua la haki, nyota angavu ambaye ni Kristo.

Kanisa daima linahitaji kuangazwa na Kristo na Injili yake, kwa sababu kama mtumbwi ambao daima hukatisha  mawimbi ambayo mara nyingi huchafuka katika historia, linaweza kupatwa na hatari ambayo sio kuwa Kanisa la Yesu. Kwa hiyo mzee Simeoni anamwambia Maria na Yosefu kuwa “ Mtoto huyu aliyezaliwa atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu; na hivyo mawazo ya watu wengi yataonekana wazi(Lk 2,34). Yesu anaendelea kuwa kashfa hata leo hii, ishara ya mapingamizi ambayo yanaweka migogoro katika usalama wetu, na kutikisa mioyo yetu ili isije ikalemazwa na woga, hisifungwe katika unafiki, hisiwe migumu katika dhambi.

Furaha ya Injili kiukweli wakati inatufariji, na kutuinua, na ni ya kinabii ambayo inatuweka katika mgogoro ambao unaendelea kutusumbua mantiki za madaraka ya kibinadamu, mahesabu ya kidunia, silaha za dhuluma, mantiki ya mgawanyiko na utata. Yesu anaendelea kuwa Yeye ambaye anasumbua amani za uongo wa yule ambaye kwamba kwa “nje wanaonekana wazuri, lakini ndani kumejaa mifupa ya wafu na kila aina ya ubaya… waliojaa unafiki na uovu(Mt 23, 27-28). Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko amefura kuwakilisha kitabu hicho ambacho kinataka kutoa sauti ya Kanisa la Mashariki kwa njia ya simumulizi, za kwanza kabisa, tafakari za Kardinali Lazzaro You Heungsik, ambaye alikutanteua hivi karibuni kuongoza Baraza la Kipapa la Wakleri.

Katika maandiko yake mazuri ya kupendwa na ya kupendeza, yanaturuhusu kuvuna matunda ya imani iliyopandwa katika nchi ya wafiadini na iliyochanua kwa urahisi, shukrani kwa ushuhuda wa furaha wa Kanisa hai. Na kutoka katika simulizi ambayo pole pole inachukua umbo, tunaweza kuona njia ya kubaki,sisi sote kama Kanisa aminifu kwa Yesu na Injili yake, mbali na kila aina ya malimwengu. Kutokana na kuamini, kuliko jionesha katika kurasa hizi, ambamo inaonekana kusukana mambo ya wasifu na tafakari  za kiroho na kichungaji, Kardinali Lazaro anaibua nje sura ya imani iliyozaliwa kutokana na kukutana bila kuchoka na Neno la Mungu na kwa ushuhuda wa Injili; Sura ya Kanisa kijana na linaloanza, lililozaliwa na walei, ambalo linakuwa ni chombo cha matumaini na huruma, kinachowatunza waliojeruhiwa; taswira ya huduma ya kikuhani inayohitaji kujijenga kwa upya katika mwanga wa Injili, likijiondoa katika  aina za ukasisi wote na kujitafakari kwa upya ule karibu na upamoja na ndugu walei, katika jumuiya za kisinodi na huduma.

Kwa kuhitimisha, dibaji hiyo, Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kuelezea shukrani zake kwa Kardinali Lazaro na ambaye alihariri kurasa hizo. Kwa sababu wote tunahitaji mwanga huo ambao unatoka Mashariki. Tunahitaji kusikiliza ushuhuda hai wa kaka dada wengi ambao kwa shauku na licha ya kupitia mateso mengi, walipokea kwa mikono wazi Yesu kama alivyo fanya mzee Simeoni, kwa kupokea mahubiri ya Mtakatifu Andre Kim na wamisionari wengi ambao mara nyingi walipoteza maisha kwa ajili ya furaha ya Injili. Tunahitaji kujikita kwa kina ili kutimiza safari kuelekea Mashariki na kwa kujiweka katika shule ya mtindo mmoja wa maisha ya kiroho na kikanisa ambayo yanaweza kuuhusha imani yetu. Na tunahitaji kukumbuka kuwa hata katika ugumu na katika giza, Bwana anakuja kama radi. Na anataka kuangazia maisha yetu. Anahitimisha kwa tehe 2 Februari 2023 katika Siku Kuu ya Kuwalishwa Bwana Hekaluni.

Kuhusiana na Kardinali Lazzaro

Lazzaro You Heung-sik alizaliwa mnamo tarehe 17 Novemba 1951 huko  Nonsan-qu Chungnam (Korea Kusini). Baada ya kupokea ubatizo akiwa na umri wa miaka 16 alianza kushiriki kwa uhai wote katika maisha ya Kanisa na baadaye kujiunga na Seminari ambapo alipewa daraja takatifu la Upadre mnamo mwaka 1979. Amepata shahada ya udaktari katika Taalimungu maadili na  baadaye huduma ya kichungaji kama msimamizi wa kiparokia , Gambera wa Kituo Katoliki cha Elimu huko Daejeon na hatimaye kuwa Gambera wa Seminari Kuu. Mnamo 2003 aliteuliwa kuwa Askofu Mwambata wa Daejeon ambaye baadaye aliitwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Wakleri mnamo tarehe 11 Juni 2021. Na aliteuliwa kwa Kardinali mnamo tarehe 27 Agosti 2022 na kuwa katika baraza la Makardinali.

Padre Consentino

Wakati Mhariri wa kitabu hicho ni Padre Francesco Cosentino mwalimu wa Taalimungu katika  Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana na anafanya kazi katika ofisi za Katibu wa Vatican. Ni mwandishi wa Vitabu vingi na michango mingi ya kitaalimungu katika mtazamo wa mahusiano kati ya Ukristo wa kwanza na tofauti za kidini kwa umakini juu ya mada ya uongo wa sura ya Mungu.

Papa aandika dibaji ya kitabu cha Kard Lazaro
01 March 2023, 09:04