Tafuta

2023.03.27 Waseminari wa Jimbo la Calabria. 2023.03.27 Waseminari wa Jimbo la Calabria.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Je mnataka nini kwa mustakabali wa ardhi&ndoto gani ya Kanisa?

Hatuwezi tena kumfikiria kama mchungaji aliye peke yake,aliyefungwa kwenye boma la parokia au vikundi vya wachungaji waliofungwa;ni lazima kuunganisha nguvu na kubadilishana mawazo,mioyo,ili kukabiliana na baadhi ya changamoto za kichungaji ambazo kwa sasa zinavuka kwa Makanisa yote ya Majimbo ya Mkoa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 27 Machi 2023, amekutana na maaskofu, wakuu, walezi na waseminari wa Calabria nchini Italia. Katika hotuba yake amewaeleza wale wanaowaongozwa vijana kwamba wamepewa dhamana ya kuwasindikiza na kufanya mang’amuzi na kuwashukuru kwa kazi yao ambayo wakati mwingine iliyofichika na mateso kwa ajili ya waseminari. Hata kama ardhi yao wakati mwingine, ina matukio ya habari na kurudisha mwanga wa majeraha ya zamani na mapya, amependa kukumbusha wao ni watoto wa ustaarabu wa kizamani wa kigiriki ambao hadi leo hii wanahitafadhi tunu za utamaduni na kiroho na  ambazo zinaungana pamoja na zile za Mashariki na Magharibi.

Papa amekutana na waseminari wa Calabria
Papa amekutana na waseminari wa Calabria

Papa amemkumbuka Hisotria ya Omero, katika simulizi ya Odissea, anasimulia kuwa Ulisse wakati wa kuelekea hitimisho la safari yake alisimama katika ardhi ambayo angeweza kushangazwa uzuri wa bahari mbili. Hii inafanya kufikiria ardhi yao, yenye lulu iliyopo kati ya Bahari ya Tirreno na Ionio. Hiyo inag’aa hata kama mahali pa kiroho kwa kukumbusha madhabahu muhimu, watakatifu na watawa wa ndani, pamoja na uwepo wa jumuhiya za Kigiriki- kibinzantine Yote hayo ni urithi wa kidini ambao ingewezekana kuwa na hatari ikiwa wangebakia kushangaa tu na ikiwa wasingekuwepo leo hii kama sehemu yao na kupyaisha jitihada za pamoja za kuhamasisha uinjilisjhi na malezi ya kikuhani.

Baba Mtakatifu  amesema  kutoka katika neno lililochukuliwa kwenye Injili ya Yohane: “Wakakaa pamoja naye” (Yn 1:39) amesema “yanarejea wanafunzi wa kwanza wanaomfuata Yesu na kutukumbusha kwamba huu ndio msingi wa kila kitu: kubaki na Bwana na kumweka kwenye msingi wa huduma yetu, vinginevyo tutajitafuta sisi wenyewe na huku tukijitolea kwa mambo yanayoonekana kuwa mazuri,ambayo inakuwa ni kujaza utupu tulionao ndani”. Kwa njaia hyo papa amesema aliona vizuri mtu mashuhuri wa nchi yao, Mtumishi wa Mungu Cassiodorus ambaye aliandika kuwa: “Vitu vyote huanguka katika uharibifu unaosogea mbali na upendo wa ukuu wako. Kukupenda ni kujiokoa [...] kukupoteza ni kufa”. (CASSIODORO, De anima, XVIII).

Papa amekutana na Jumuiya ya Seminari ya Calabria
Papa amekutana na Jumuiya ya Seminari ya Calabria

Na huu ndio wito wao wa kuwaongoza njia pamoja na Bwana, upendo wa Bwana. Na kuwa waangalifu ili wasije wakaangukia katika taaluma ambayo ni pigo, kwa sababu amsema “taaluma ni moja ya aina mbaya zaidi za ulimwengu ambazo sisi viongozi tunaweza kuwa nazo”. Hata hivyo, amependa pia kusisitiza juu ya swali la kwanza ambalo Yesu aliwauliza wanafunzi wawili alipotambua kwamba wanamfuata: “Mnatafuta nini?” (38). Papa ameongoza: “Wakati fulani tunatafuta “mapishi” mepesi, badala yake Yesu alianza na swali linalotualika kutazama ndani, ili kuthibitisha sababu za safari yetu”. Na leo  hii Papa pia amependa kuwauliza swali hilo. Kwanza kabisa kwa wanaseminari: mnatafuta nini? Ni tamaa gani iliyowasukuma kwenda nje kukutana na Bwana na kumfuata kwenye njia ya ukuhani? Mnatafuta nini katika Seminari? Na mnatafuta nini katika ukuhani? Papa ameongeza “Inatubidi tujiulize hivyo, kwa sababu wakati mwingine hutokea kwamba “nyuma ya kuonekana kwa udini na hata upendo kwa Kanisa”, kiukweli tunatafuta “utukufu wa kibinadamu na ustawi wa kibinafsi” ( Apostolic Exhortation Evangelii gaudium, 93).”

Papa amesema kwamba inasikitisha sana unapokuta mapadre ambao ni watendaji kazi, wamesahau kuwa wachungaji wa watu na kugeuka makasisi wa serikali, sawa na wale wa mahakama za Ufaransa, le monsieur l'Abbé, ambao walikuwa makasisi wa kiserikali; “ni mbaya wakati hisia ya kuhani inapotea; labda tunatafuta huduma ya ukuhani kama kimbilio la kujificha nyuma au jukumu la kupata ufahari, badala ya kutaka kuwa wachungaji wenye moyo uleule wa Kristo wa huruma na huruma”.

Kutokana na hilo Papa amependa kuwauliza kwa maneno sawa na moja ya kitabu chao kinachowaongoza cha mwaka kuwa: “mnataka kuwa makuhani wa makasisi ambao hawajui kukanda na udongo wa wanadamu wanaoteseka, au kuwa kama Yesu, ishara ya huruma ya Baba?”, kwa kuongeza “ Hapa tukumbuke hilo kwamba: Kipindi cha Seminari ni wakati wa kufanya ukweli na sisi wenyewe, kuacha mabarakoa, hila na kuonekana”. Na katika mchakato huo wa utambuzi, wamwache watendewe kazi na Bwana, ambaye atawafanya kuwa wachungaji sawasawa na moyo wake maana kinyume chake ni kuvaa kibarakoa, kujipodoa, kuonekana ni sawa na viongozi, ambapo si wachungaji wa watu bali wachungaji wa viongozi wa serikali.

Mkutano wa Papa na waseminari ya Calabria
Mkutano wa Papa na waseminari ya Calabria

Hata hivyo pia  Papa ameshughulikia swali la Yesu kwa ndugu zake Maaskofu, kwamba wao ndio wako  mstari wa mbele: je wanatafuta nini? Je! wanataka nini kwa ajili ya mustakabali wa ardhi yao, wana ndoto gani ya Kanisa? Na wanafikiria kuhani wa aina gani kwa watu wao? Kwa sababu wana jukumu la kuwafunza watoto hao, wanawafundisha na nani? Na utambuzi huu ni wa lazima zaidi leo hii kuliko wakati mwingine wowote, kwa sababu katika wakati ambapo Ukristo fulani wa zamani umepungua, majira mapya ya kikanisa yamefunguka mbele yetu, ambayo yamehitaji na bado yanahitaji kutafakari pia juu ya sura na huduma ya kuhani.

Papa amesisitiza kwamba “Hatuwezi tena kumfikiria kama mchungaji aliye peke yake, aliyefungwa kwenye boma la parokia au vikundi vya wachungaji waliofungwa; ni lazima kuunganisha nguvu na kubadilishana mawazo, mioyo, ili kukabiliana na baadhi ya changamoto za kichungaji ambazo kwa sasa zinavuka kwa Makanisa yote ya Majimbo ya Mkoa. Kwa hilo Papa amefikiria kwa mfano, uinjilishaji wa vijana; kwa kozi za jando la Kikristo; kwa utauwa maarufu,  utauwa mwingi maarufu -ambao unahitaji chaguzi za umoja zilizovuviwa na Injili; lakini pia amefikiria mahitaji ya upendo na kukuza utamaduni wa uhalali katika sheria”.

Papa kwa waseminari wa Calabria, Italia
27 March 2023, 17:11