Tafuta

Papa Francisko:Yesu anatukaribia katika kaburi zetu&kusema ondoeni jiwe!

Papa akitafakari Injili ya siku amesisitiza kuwa Injili ya Yohane,sura ya 11 ni wimbo wa maisha na inatamkwa tunapokaribia Pasaka.Labda hata sisi katika wakati huu,tunabeba uzito mioyoni mwetu au mateso fulani,utafikiri yametubamiza.Ni wakati wa kutoa jiwe na kukutana na Yesu aliye karibu.Yeye anatukaribia katika kaburi zetu na kuomba tuzikabidhi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Leo ni Dominika ya tano ya Kwaresima na Injili inatuwakilisha ufufuko wa Lazaro (Yh 11,1-45). Ni muujiza wa mwisho wa Yesu uliosimuliwa kabla ya Pasaka; kuhusu ufufuko wa rafiki yake Lazzaro. Lazaro alikuwa rafiki wa Yesu, ambapo alikuwa anajua kuwa karibu anakufa; alianza safari, lakini alifika nyumbani kwake siku nne baada ya kuzikwa kwake na matumaini  yalikuwa yamepotea. Uwepo wake lakini unawasha kidogo imani katika moyo wa dada zake Marta na Maria (Yh 11.22.27). Wao pamoja na uchungu, wanakwea katika mwanga huu. Yesu anawaalika wawe na imani na kuwaomba wafungue kaburi. Baadaye alisali kwa Baba yake na kwa hiyo akapaza sauti akimwiita Lazaro atoke nje (Yh 11,43). Yeye alirudia maisha na kutoka Nje. Huo ndio muujiza mdogo rahisi.

Papa Francisko wakati wa tafakari yake
Papa Francisko wakati wa tafakari yake

Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, katika Dominika ya tano ya Kwaresima, tarehe 26 Machi 2023 kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican. Papa amesema kwamba: Ujumbe huu huko wazi kwamba Yesu anatoa maisha hata kama utafikiri hakuna tumaini. Inawezekana mara kadhaa kuhisi bila tumaini na hata kukutana na watu ambao wameacha kuwa na matumaini; wote inawatokea hilo, wamepoteza kwa uchungu mkuu, kwa sababu ya ugonjwa, kwa sababu ya kukata tamaa,  wana huzuni kwa sababu waliishi uzofu  mabaya na  moyo ulijeruhiwa na hawawezi kutumania pamoja na makosa au usaliti uliopokelewa, kwa sababu ya makosa makubwa yaliyotendwa.Papa ameongeza kusema: "Ni vipindi ambavyo utafikiri Maisha yamefungiwa kwenye kaburi: yote ni giza, kila kitu kinachotuzunguka ni uchungu tu na mahangaiko".

Makundi mbali mbali ya mahujaji katika sala ya Malaika wa Bwana
Makundi mbali mbali ya mahujaji katika sala ya Malaika wa Bwana

Yesu leo hii anatueleza kuwa sio hivyo, kwamba katika vipindi hivi sisi hatuko peke yetu, zaidi kwamba ni katika vipindi hivyo ambapo Yeye mwenyewe anajifanya kuwa karibu ili kutupatia maisha. Yeye analia machozi pamoja na sisi, kama alivyomlilia Lazzaro: na Injili inarudia mara mbili kwamba aliugua (Yh11,33.38) na kusisitiza kuwa alilia (Yh 11,25). Na wakati huo huo, Yeye anatualika tusiache kumwamini na kumtumainia, tusiache tugadamizwe na hisia zilizo hasi. Yeye anatukaribia katika kaburi zetu na kutuelekeza kama alivyosema wakati ule kuwa "liondoeni lile jiwe" (Yh 11,39). Katika vipindi hivi sisi tunalo kama jiwe ndani  mwetu na uwezo pekee wa kufanya  ni kwenda kwa Yesu kwa njia ya neno lake la 'Ondoeni jiwe'.

Kila makundi ya mahujaji na ishara zao kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro
Kila makundi ya mahujaji na ishara zao kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro

Yesu anatwambia hilo kwamba "ondoeni lile jiwe: uchungu, makosa, hata kushindwa, msifiche ndani mwenu, katika chumba chenye giza na upweke, uliofungwa". Ondoeni jiwe; toeni nje kile ambacho kimo ndani,na kwamba husiwe na aibu bali nenda nje, toa kwake kwa imani, kwa sababu Bwana anasema kuwa Yeye hakashifu; kwa hiyo "Tupeni kwangu kwa imani, bila hofu, kwa sasababu mimi niko nanyi, ninawapenda na ninatamani kwamba ninyi mrudi kwangu". Na kama Lazzaro anarudia hivyo  kwa kila mmoja wetu kuwa, njoo huku nje. Amka, anza tena safari, pata tena imani! Ninakushika mkono kama ulivyokuwa mdogo unajifunza kuanza hatua za kwanza za kutembea". Lakini “Je ni mara ngapi katika maisha, tumejikuta namna hii, katika kesi kama hiyo bila kuwa na nguvu ya kuamka"?. Na Yesu anasema nenda mbele! Mimi niko pamoja nawe”.

Kikos cha wana anga Italia
Kikos cha wana anga Italia

Baba Mtakatifu ameendelea kusema " Mfungueni, leso mkamwache aende zake (Yh 11,45) na msiangukie kwenye ugumu unaowakandamiza, wa hofu inayowabagua, kukata tamaa kwa sababu ya kukumbukauzoefu mbaya, woga ambao unakugandamiza".  Yeye anasema “Ninakupenda uwe huru na hai, sitokuacha na niko nawe. Sitokuacha ufungwe na uchungu, sitoacha tumaini life, kwa hiyo rudi ili uishi tena! " “Je nifanyenje” Nishike mkono” Na Yeye anatushika mkono. Anatuita  kutoka nje na Yeye ana uwezo wa kufanya hivyo katika wakati mbao tunaupitia sisi sote”, Papa Francisko amesisitiza.

Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Akiendelea na tafakari ya Injili  hiyo  amesisitiza kwamba somo hili, ambalo ni sura ya 11 ya Injili ya Yohane, na kusahuri  waisome  tena amesema ni wimbo wa maisha  ambao unatamkwa tunapokaribia Pasaka. Labda hata sisi katika wakati huu miyoni mwetu tuna uzito au mateso fulani, ambayo utafikiri yametubamiza, jambo baya, dhambi ya zamani ambayo haitufanyi tutoke nje, makosa fulani ya ujana, lakini ambayo huwezi kujua katu. Haya mambo mabaya lazima yatoke nje. Na Yesu anasema Njoo nje. Kwa hiyo ni wakati wa kutoa jiwe na kukutana na Yesu ambaye yuko karibu. Katika hilo, Baba Mtakatifu ameuliza maswali: Je tunaweza kumfungulia moyo na kumkabidhi wasiwasi wetu?

Umati Mkubwa ulioudhuria sala ya Malaika wa Bwana na Papa
Umati Mkubwa ulioudhuria sala ya Malaika wa Bwana na Papa

Kwa kufungua kaburi la matatizo, je tunao uwezo na kutazama upeo zaidi kuelekea mwanga wake au tunaogopa hilo? Na kwa mara nyingine tena, kama vioo vidogo vya upendo wa Mungu, je tunaweza kuangaza katika mazingira ambamo tunaishi kwa maneno na ishara za maisha? Kwa kuhitimisha Papa amesema: “Kushuhudia kwa tumaini na furaha ya Yesu sisi sote ni wenye dhambi? Katika muktadaha huo, Papa amependa kuwaeleza neno moja waungamishi kwamba: " Ndugu wapendwa msisahau kuwa hata ninyi ni wenye dhambi na ninyi mko katika maungamo  ambapo sio kwa ajili ya kuwatesa  bali kusamehe na kusamehe kila kitu, kama Bwana asamehevyo kila kitu.”Kwa kuhitimishwa amesema  Maria Mama wa Tumaini, atupyaishe ndani mwetu furaha hili tusijihisi kuwa peke yetu na wito wa kupeleka mwanga katika giza linalotuzunguka”.

Tafakari ya Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 26 Machi 2023
26 March 2023, 12:18