Papa:Yerusalemu inahitaji amani zaidi ya pande zote
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican tarehe 9 Machi 2023 na washiriki wa mjadala wa Kikundi cha Pamoja cha Kazi kwa ajili ya Mazungumzo kati ya Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na Tume ya wapalestina kwa ajili ya Mazungumzo ya Kidini. Akianza hotuba yake ameshukuru maneno ya Kardinali Coccopalmerio na kuwakaribisha wote ambao wametoa maishia kwa ajili ya mjadala huo. “Ninayo furaha kumkumbuka Kadinali Jean-Louis Tauran, ambaye pamoja na Sheikh Mahmoud Al-Habbash, waliopo hapa na ambaye namsalimia, walitoa uhai kwa Kundi hili. Ari na hekima yake iendelee kutia moyo kujitolea na mipango yenu”. Kuhusu hilo Papa amependa kuwakumbusha kile ambacho walitamka pamoja mnamo 2019 na Mfalme wa Morocco, yaani Wito ili Yerusalemu iweze kuzingatiwa kama urithi wa pamoja wa binadamu na hasa kwa ajili ya waamini wa dini tatu zinzomtambua Mungu kama mahali pa kukutana na alama ya kudumu kwa amani.
Katika Injili, Yerusalemu ni mahali ambapo palitokea matukio mengi ya maisha ya Yesu tangu akiwa mdogo, alipowakilishwa katika hekalu, mahali ambap wazazi wake walikuwa wakiendea kila mwaka katika siku kuu ya Pasaka. Katika Mji Myakatifu , Yesu alifundisha na kutimiza miujiza mingi hasa kwa kupeleka umilifu wa utume wake, kwa mateso, kifo na ufufuko katika moyo wa imani kikristo. Huko Yerusalema kumezaliwa Kanisa, , wakati Roho Mtakatifu aliwashukia wanafunzi waliokuwa wamejikutanya katika sala na Bikira Maria, na hapo aliwasukua kutangza kwa wote ujumbe kwa wokovu. Lakini Yerusalem inathamani ya ulimwengu, ambayo imo tayari katika maana ya jina lake “ Mji wa amani”. Na katika pendekezo hilo Papa amekumbusha wakati wa maisha ya Yesu ambapo alikuwa karibu na siku za mateso yake, Yeye alipofika katika Mji Mtakatifu, kwa karibu na mji huom aliulilia na kusema “ Ikiwa wewe pia ungeelewa, siku hii, nini husababisha amani! (Lc 19,41-42
Yesu alililia Yerusalemu. Haupaswi kupita mbali sana kwa haraka. Katika machozi ya Yesu yanastahili kutafakariwa, kwa kimya. Ni wanaume na wanawake wangappi, wayahudu, wakristo, waislamu, wamelia na bado wanaliwa leo hii kwa ajili ya Yerusalemu! Hata kwetu sisi wakati mwingine kwa kufikiria Mji Mtakatifu machozi yantulenga lenga kwa sababu ni kama mama ambaye moyo wake haupati amani kwa sababu mateso ya watoto wake bado yapo. Tukio hilo la kiinjilia linatukumbusha thamani ya huruma, huruma ya Mungu kwa ajili ya Yerusalemu, ambay lazima igeuka kuwa huruma yetu ya nguvu zaidi dhidi ya itikadi zozote, na wa upande wowote. Upendo kwa ajili ya Mji Mtakatifu lazima uwe mkubwa daima, kama mama ambaye anastahili heshima na kuheshimiwa na wote.