Tafuta

2023.03.11 Papa amekutana na washiriki wa Mungano wa Kimkakati wa Vyuo Vikuu vya Utafiti vya Kikatoliki",SACRU, na Taasisi ya Centesimus Annus Pro Pontifice 2023.03.11 Papa amekutana na washiriki wa Mungano wa Kimkakati wa Vyuo Vikuu vya Utafiti vya Kikatoliki",SACRU, na Taasisi ya Centesimus Annus Pro Pontifice  (Vatican Media)

Papa Francisko:Tusiwabague wanawake hasa katika mazingira ya kazi!

Haiwezekani kunyamaza kuhusu majeraha ya wanawake waathirika wa vurugu na unyanyasaji.Ni wito wa Papa wakati wa kukutana na washiriki wa mkutano mjini Vatican ulioandaliwa na Mungano wa Kimkakati wa Vyuo Vikuu vya Utafiti Kikatoliki(SACRU)na Taasisi ya Centesimus Annus Pro Pontifice.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko akikutana na wajumbe wa Mkutano wa Muungano wa Kimkakati wa Vyuo Vikuu vya Utafiti vya Kikatoliki (SACRU) na Taasisi ya Mfuko wa Centesimus Annus Pro Pontifice, ametumia fursa ya kutoa wito wake huku akilaani ubaguzi dhidi ya wanawake katika mazingira ya kazi, ambapo mara nyingi kwa sababu yakuwa wajawazito wanatupwa nje na amepongeza kwa  ushujaa wa wanawake wengi wa jirani. Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo katika hotuba yake Jumamosi tarehe 11 Machi 2023 jijini Vatican ameanza kumshukuru Profesa Tarantola na Gambela Anelli kwa maneno yao na salamu kwa wote wajumbe. Wamekutana katika fursa ya kuwakilisha kitabu chenye kichwa “Uongozi zaidi wa kike kwa ajili ya ulimwengu bora. Kutunza kama Injili ya nyumba yetu ya pamoja”. Hiyo ni mada ambayo Baba Mtakatifu amekiri kuipenda sana kuhusu umuhimu wa utunzaji. Ilikuwa ni moja ya ujumbe wa kwanza ambao alipenda kuutoa kwa Kanisa tangu mwanzo wa upapa wake kwa kukumbusha mfano wa Mtakatifu Yosefu, mpole na mlinzi wa Mwokozi.

Papa alitana na watafiti wa vyuo vikuu katoliki na mfuko wa kipapa wa Cebtesimus Annus
Papa alitana na watafiti wa vyuo vikuu katoliki na mfuko wa kipapa wa Cebtesimus Annus

Papa Francisko amebainisha kuwa kama walivyotanguliza kukumbusha, kiukweli ni tunda kubwa lamichango mbali mbali iliyokusanywa na kufanyiwa kazi kwa njia ya ushirikiano, ambao hadi sasa haukuwa umechapishwa, kati ya  baadhi ya vyuo vikuu vilivyotawanyika ulimwenguni na Mfuko wa Vatican ambao wote ni wa kilei. Huu ni mtindo mpya kabisa na wa maana ambao utajiri wa yaliyomo yanatokana na uhusiano wa uzoefu, ujuzi tofauti na wa ziada, njia za hisia na mbinu. Ni mfano wa taaluma nyingi, tamaduni nyingi na kushirikiana kwa hisia tofauti: maadili muhimu sio tu katika vitabu, bali pia kwa ulimwengu ulio bora. Katika nuru hiyo, Papa Francisko amependa kuchambua mantiki tatu za utunzaji ambazo wanawake katika sehemu kubwa wanajikita yao: Sehemu kubwa ya heshima na kwa ajili ya kukabiliana kwa namna mojao ya changamoto mpya.

Ya kwanza ni ujumuishaji zaidi. Katika kitabu chao kinazungumza juu ya tatizo la ubaguzi ambao mara nyingi unawakumba wanawake, kama tabaka la wadhaifu wa kijamii. Papa amesema mara nyingi amekumbusha kwa nguvu kuwa tofauti haipaswi kamwe kutokea katika ukosefu wa haki lakini zaidi shukurani na ukarimu wa pamoja. Hekima ya kwli na sura zake nyingi, ni kujifunza na kuishi kwa kutembea pamoja na ndiyo hivyo tu tunaweza kugeuka kuwa wazalishaji wa amani. Mchango wa pili: kwa heshima zaidi kwa mwingine. Utu na haki za kimsingi za kila mtu lazima ziheshimiwe: elimu, kazi, uhuru wa kujieleza na kadhalika. Hii ni kweli hasa kwa wanawake, ambao ni rahisi zaidi kukabiliwa na ukatili na unyanyasaji. “Niliwahi kusikia mtaalamu wa historia akisema jinsi ambavyo vito vya thamani vilizaliwa ambavyo wanawake huvaa kwa sababu  wanawake wanapenda kuvaa vito, lakini sasa  hata wanaume .

Watafiti wa vyuo vikuu katoliki
Watafiti wa vyuo vikuu katoliki

Kulikuwa na ustaarabu ambapo ilikuwa ni desturi kwamba mume, alipokuwa akifika nyumbani, akiwa na wake wengi, ikiwa hapendi mmoja, alimwambia: "Nenda huko, toka nje!; na yule ilikuwa inabidi aondoke na alichokuwa amevaa, kwa sababu hakuweza kuingia kuchukua vitu vyake, na alikuwa akiondoka hivyo. Ni kwa sababu kulingana na historia hiyo kwamba wanawake walianza kuvaa dhahabu, na hapo ndipo ikawa mwanzo wa kuvaa vito vya thamani. Ni hadithi, labda, lakini ya kuvutia. Kwa muda mrefu sasa, wanawake wamekuwa nyenzo za kwanza za kutupa. Hii ni mbaya. Haki za kila mtu lazima ziheshimiwe, Papa amesisitiza. Hatuwezi kukaa kimya mbele ya janga hili la wakati wetu. Mwanamke anatumiwa. Ndio, hapa, katika jiji! Wanawalipa kidogo eti kwa sababu ni mwanamke. Alafu ole wake aende akiwa na tumbo yaani wakimuona ana mimba, wanamfukuza arudi nyumbani, kinyume chake wakikuona unaanza kazi wanakurudisha nyumbani. Hii ni moja ya njia ambazo hutumiwa leo hii katika miji mikubwa: kuwatupa wanawake, kwa mfano na akina mama wajawazito. Ni muhimu kuona ukweli huu, kwa sababu ni pigo.

Tusiwaache bila sauti wanawake wahanga wa unyanyasaji, unyonyaji, kutengwa na shinikizo zisizostahili, kama hizo zilizotawaja za kazi. Hebu tuseme uchungu wao na kukemea kwa nguvu dhuluma wanayotendewa, mara nyingi katika mazingira ambayo yanawanyima uwezekano wowote wa ulinzi na ukombozi. Lakini pia tunatoa nafasi kwa matendo yao, ambayo ni nyeti kiasili na yenye nguvu na yenye mwelekeo kuelekea ulinzi wa maisha katika kila hali, katika kila zama. Papa amefikia kufafanua hatua ya mwisho  ya kukabili changamoto mpya kwa njia mpya. Ni Ubunifu. Umaalum usioweza kubadilishwa wa mchango wa wanawake kwa manufaa ya wote hauwezi kukanushwa. Tayari tunaona hili katika Maandiko Matakatifu, ambapo mara nyingi ni wanawake ambao huamua mambo muhimu ya mabadiliko katika nyakati za maamuzi katika historia ya wokovu. 

Papa akizungumza na watafiti wa vyo vikuu katoliki
Papa akizungumza na watafiti wa vyo vikuu katoliki

Kwa kutoa mfano amesema tumfikirie Sara, Rebeka, Judith, Susana, Ruthu, kwa kuhitimisha na Maria na wanawake waliomfuata Yesu hadi chini ya msalaba, ambapo  tunayemwaona  kati ya wanaume ni Yohane pekee aliyebaki, wengine wote walikimbia. Wale wajasiri waliokuwepo hapo ni wanawake. Katika historia ya Kanisa, basi, tunafikiria watu kama Catherine wa Siena, Josephine Bakhita, Edith Stein, Teresa wa Kalcuta na pia wanawake wa mlango wa karibu ambao tunawajua kwa ushujaa mwingi wa kuendeleza ndoa ngumu. watoto wenye matatizo... mashujaa wa wanawake. Zaidi ya mitazamo ya mtindo fulani kijiofrafia, ni watu wa kuvutia kwa azimio lao, ujasiri, uaminifu, uwezo wa kuteseka na kusambaza furaha, uaminifu, unyenyekevu, uvumilivu. Papa amerudia kusimulia uzoefu wake alipokuwa Buenos Aires na kusafiri kwa Bus akienda katika Sekta ya Kaskazini Magharibi, ambapo kulikuwa na Parokia nyingi, Bus hiyo ilikuwa ikipita karibu na Gereza ambalo kulikuwa na mstari wa watu ambao walikuwa wanakwenda kutembelea wafungwa na asilimia 90 walikuwa ni wanawake,  mama ambao walikuwa hawawaachi watoto wao. Ni nguvu hii ya mama na nguvu ya kimya, lakini ya siku ziku zote.

Historia yetu imejaa wanawake kama hawa, maarufu na wasiojulikana lakini sio kwa Mungu!  wanaoendeleza safari ya familia, jamii na Kanisa; wakati mwingine na waume wenye matatizo, wakorofi... watoto wanaendelea... Pia tunaona hapa, Vatican, ambapo wanawake wanaofanya kazi kwa bidii  hata katika majukumu makubwa, kwa sasa ni wengi, asante Mungu. Kwa mfano, tangu wakati ambapo kuna mwanamke, katika masuala ya jumbla mjini Vatican, mambo yanakuwa bora zaidi. Na sehemu nyingine, ambapo kuna wanawake, makatibu, Baraza la Uchumi, kwa mfano, kuna makadinali sita na walei sita, wote wanaume. Baada ya kusimulia kisa fulani Papa amesema Mwanamke pekee ndiye anayeweza kufanya hivyo kwa hiyo kwa hiyo tunapaswa kuangalia jinsi wanawake wanavyofanya: ni jambo kubwa. Tuko katika wakati wa mabadiliko ya nyakati ambayo yanahitaji majibu ya kutosha na yenye kusadikisha. Katika muktadha wa mchango wa wanawake katika michakato hii, Papa amependa kutaja mmoja wao: maendeleo yanayoendelea na matumizi ya akili bandia na shida dhaifu iliyounganishwa nayo ya kuzaliwa kwa mienendo mpya na isiyotabirika ya mamlaka. Ni hali ambayo bado hatuijui, ambayo utabiri unaweza kuwa wa kukisia tu na wa kukadiria.

Papa na wajumbe wa watafiiti wa vyuo vikuu katoliki
Papa na wajumbe wa watafiiti wa vyuo vikuu katoliki

Kiukweli, wanawake katika uwanja huo wana mengi ya kusema. Kwa sababu  wanajua jinsi ya kuunganisha kwa njia ya pekee, katika njia yao ya kutenda, lugha tatu: ile ya akili, ya moyo na ile ya mikono. Lakini yenye maelewano. Mwanamke, wakati yeye ni mtu mzima, anafikiri nini anahisi na kufanya; anahisi kile anachofanya na kufikiria; anafanya kile anachohisi na kufikiria: ni maelewano. Hii ni fikra ya mwanamke; na hufundisha wanaume kuifanya, lakini ni mwanamke ambaye hufika kwanza kwenye upatanisho huo wa usemi, pia wa kufikiria na lugha tatu. Ni muunganisho unaofaa kwa mwanadamu pekee na ambao mwanamke hujumuisha kwa njia ya ajabu  ambo amesema hasemi kipekee, wa kushangaza na pia kimsingi kwani kama jinsi ambavyo hakuna mashine ingeweza kufikia, kwa sababu hahisi moyo wa mtoto anayembeba tumboni,ukidunda  ndani yake, haanguki, amechoka na mwenye furaha, karibu na kitanda cha watoto wake, hailii kwa uchungu na furaha ikishiriki katika uchungu na furaha za watu anaowapenda. Papa Francisko amehitimisha hotuba yake kwa maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II katika waraka wake wa Mulieris dignitatem: Kanisa linatoa shukuran kwa wanawake wote na kwa kila mmoja, kwa mama , dada na wachumba; kwa wanawake watawa… kwa ajili ya wanawake wanafanya kazi kitaaluma… kwa wote … katika uzuri na utajiri wa kike

11 March 2023, 15:33