Tafuta

2023.03.10   Mahojiano ya Papa na Infobae:“Mungu anakupatia uhuru,siku zote". 2023.03.10 Mahojiano ya Papa na Infobae:“Mungu anakupatia uhuru,siku zote". 

Papa Francisko:Ninahisi amani na furaha ya kumfuata Bwana

Tunachapisha ndondoo kwa upana ya mahojiano ya Papa Francisko akiwa nyumbani Mtakatifu Marta iliyoandaliwa katika gazeti la Infobae na Padre Guillermo Marcó wa Argentina ambaye alikuwa ni msemaji wake mkuu wakati Papa akiwa ni Askofu Mkuu wa Buenos Aires,nchini Argentina.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika gazeti la Infobae limeandika mahojiano ya Padre Guillermo Marcó, wa Argentina ambaye alikuwa ni msemaji wake mkuu wakati Papa akiwa ni Askofu Mkuu wa Buenos Aires. Yeye awali ya yote anaeleza kuwa wakati akitembea katika uwanja wa Mtakatifu Petro,alifikiri mamilioni ya watu ambao wanataka kuzungumza na Papa Francisko. “Nilipata fursa hiyo adhimu kwa miaka. Kutoka Buenos Aires nilikuwa kawaida nikizungumza naye, wakati mwingine zaidi kwa siku.  Leo hii mawasiliano sio mengi, lakini yeye bado anakumbuka kwa uhai wake ukaribu na urafiki ambao ulikuwapo kwa mianga mingi; kwa hiyo katika mantiki hiyo haukubadilika, … kumsikiliza ni muhimu na kunavutia….

Jambo la kwanza ninalotaka kukuuliza ni: ni nini kinachokuvutia zaidi katika kumfuata Yesu... siwezi kueleza kwa maneno. Ninachoweza kusema ni kwamba ninapokuwa katika maelewano naye ninahisi amani, ninajisikia furaha. Nisipomfuata, kwa sababu nimechoka, kwa sababu nilimwekea wakati maalum au kikomo cha wakati, najiona sijisikii. Ni kana kwamba tayari nimejazwa na maisha yangu… Mtu fulani aliwahi kuniambia “Mungu anakupa uhuru, siku zote anakupa uhuru, lakini unapomjua Yesu unapoteza uhuru wako”. Hii iliniweka kwenye mgogoro. Sijui kama utaipoteza au la, lakini jinsi Bwana anavyokuita na kuanzisha mazungumzo nawe hukufanya useme "hapana, siendi popote pengine, hii inanitosha". Kwa hivyo ninahisi usawa huo kwa maana nzuri ya neno hilo, sio la kisaikolojia, la amani, hata katika nyakati hizo za usawa mkubwa kwa sababu ya hali ngumu za kukabili.

Hapo, katika maungamo hayo ya parokia ya Mtakatifu José de Flores, uliweza kutambua wito wako: ni nini ulichohisi ambacho kilikuwa maalum katika wito huo? Inashangaza kwa sababu baada ya uzoefu huo mnamo Septemba 21 niliendelea na maisha yangu bila kujua nitafanya nini. Lakini kulikuwa na kitu tofauti ambacho kilikuwa kikijiimarisha polepole. Sikutoka hapo kwenda seminari… Imekuwa miaka mitatu. Ni kama mchakato unaobadilisha mielekeo yako, marejeo yako. Bwana anaingia katika maisha yako na kuyapanga upya. Na bila kuchukua uhuru wako. Sijawahi kuwa na hisia kwamba siko huru.

Unaendelea kujifafanua kama "kuhani": unapenda nini zaidi kuhusu wito wa kipadre? Kukaa katika huduma. Wakati mmoja Padre aliniambia  kuwa aliishi katika mtaa wa  watu maskini sana, sio makazi duni lakini karibu na alikuwa na nyumba yake ya parokia karibu na kanisa na aliniambia kwamba alipolazimika kufunga mlango, watu waligonga dirisha. Kisha akaniambia: "Ninataka kufunga dirisha hilo kwa sababu hawatakuacha kwa amani". Watu hawatakuacha peke yako kwa amani. Na kwa upande mwingine, aliniambia kuwa nikifunga dirisha nisingekuwa na utulivu, lakini mbaya zaidi. Kwa sababu mara tu unapoingia katika mdundo wa huduma, unajisikia vibaya unapojichukulia kipande cha ubinafsi. Wito wa huduma ni kama huu, huwezi kufikiria maisha ikiwa hauko katika huduma. Kwa hiyo ningebadilisha kuwa kuhani kwa chochote baada ya uzoefu wa kuwa kuhani. Pamoja na mipaka, makosa, dhambi, lakini kuhani. Unasemaje kwa mapadre? Ninachowambia mapadre ni "kuwa kuhani". Na ikiwa haifanyi kazi kwako, tafuta njia nyingine, Kanisa linakufungulia milango mingine. Lakini usiwe rasmi. Ninapenda kusema hivi: kuwa mchungaji wa watu na sio padre wa serikali.

Je unauonaje udugu kati ya Makardinali? Kwa muda mrefu kuna ukaribu. Wanaweza kuwa na maoni tofauti, lakini jambo zuri ni kwamba wanakuambia wanachofikiri. Ninaogopa ajenda zilizofichwa. Unapokuwa na kitu na usiseme. Ninamshukuru Mungu kwamba katika Baraza la Makardinali kuna mawasiliano, kati ya lile jipya na  la zamani,na kwamba wana uhuru wa kuzungumza ... sijui kama wote, lakini wengi wanafanya hiyovyo.  Wakati mwingine “Hey, lazima kuwa makini na hili”, “tazama ...”. Ah asante. Ninafikiria juu yake na kisha ninasuluhisha, ninamwambia jinsi ... au simsikilizi, ninasema: tazama, sikusikilizi kwa hili, hili na hili. Lakini mazungumzo ni huru.

Wewe una ibada zako. Hapa kuna  mchoro huu wa Mama ambaye anafungua mafundo, ibada aliyoifanyika sana nchini Ujerumani. Je, unaweza kutuambia kwa nini uliitumia kila mara kama dokezo kwenye bahasha zako? Sijawahi kwenda mahali ambako inapatika picha asili. Ilitokea kwamba mtawa wa Kijerumani alinitumia kama salamu. Niliipenda. Nilianza kuwa na ibada kwa picha huyo nikiwa Argentina. Historia hii ni nzuri, picha haifai sana, ni kutoka katola baroque ya chini ya miaka ya 1700, ambayo tayari ilikuwa imeharibika. Mchoraji wa wakati huo ambaye alikuwa akimsumbua mkewe. Walikuwa Wakatoliki sana lakini waligombana kila siku. Na siku moja alisoma maandishi ya Mtakatifu Irenaeus wa Lyons, kulingana na mafundo ambayo mama yetu Eva alikuwa amefunga kwa  ajili ya dhambi yake yalikuwa yamefunguliwa na mama yetu Maria kwa utii wake. Mtaguso ulichukua  na kuiingiza, naamini, katika Katiba ya Kanisa. Yeye aliipenda na hivyo akamwomba Maria afungue fundo alilofunga na mkewe kwa sababu walikuwa hawaelewani. Na hii ndiyo sababu hapa chini anachora Malaika mkuu Raphael pamoja na Tobia ambaye anamwongoza kumtafuta mchumba wake, mke wake, kukutana naye. Bikira alifanya muujiza na yote yalianza kutokea hapo. Nimechukua ibada hiyo. Augsburg ni mji.

Katika Kanisa la Mtakatifu Petro huko Perlach. Sijawahi kwenda, na nilikuwa umbali wa kutupa jiwe tu kutoka huko, huko Frankfurt. Lakini hii ilinitosha na ibada ilikuwa tayari inaanza tangu nikiwa Argentina. Ni kana kwamba Mama Yetu anaweza kukusaidia, kama andiko la Mtakatifu Irenaeus linavyosema, kukusaidia kufungua mambo. Kufungua mafundo ya maisha... Ni "umama" wa Maria. Na vipi kuhusu Mtakatifu Joseph? Bibi yangu ndiye aliyemweka Mtakatifu Joseph kichwani mwangu… Nikiwa mtoto alinifanya nisali kwa Mtakatifu Joseph. Ibada ilibaki ndani mwangu. Pia unayo picha ndogo ya Mtakatifu Joseph akiwa amelala. Katika hiyo ninaweka nia maalum juu yake ... Wanaponiomba maombi, mimi ninayaweka hapo chini. Ninasema: “Wewe uliye lala suluhisha matatizo.” Na Mtakatifu  Teresa? Mtakatifu Teresina amekuwa akinivutia kila mara… Ujasiri wa mtu wa kawaida. Ukiniuliza Mtakatifu Teresina alikuwa na vitu gani vya ajabu: hakuna. Alikuwa mtawa maskini na wa kawaida. Katika siku zake za mwisho pia aliteseka na  giza kuu, majaribu makubwa dhidi ya imani, aliyapitia yote. Mwanamke wa kawaida.

Ili kuweza kumalizaia ninakuomba ujumbe mfupi. Ujumbe wa kwanza unalenga watoto: Tunzeni  babu na babi zenu. Zungumza na babu na babi. Nendeni mkawatembelee babu zane. Hacheni  babu na bibi wawadekeze. Kwa vijana…: Msiogope maisha. Msisimame tuli. Endeleeni mbele. Mtafanya makosa, lakini kosa baya zaidi ni la  kusimama, hivyo endelea mbele. Kwa baba na mama…: Msipoteze upendo. Jihadharini, ili muweze kuwatunza watoto wenu vyema. Kwa wagonjwa… Ah, hii ni ngumu kwa sababu kushauri uvumilivu ni rahisi, lakini mimi sina, kwa hivyo ninaelewa mnapokasirika kidogo. Mwombeeni Bwana awape neema ya uvumilivu naye atawapatia neema ya kustahimili haya yote.

Hatimaye kwa wazee, ambao unazungumza nao mara kwa mara…: Kwa wazee ni kwamba msisahau kwamba nyinyi ndio mizizi. Wazee lazima wapitishe hii kwa vijana, watoto na vijana. Katika aya kutoka katika Kitabu cha Yoeli: je  wito wako kama mzee ni upi, wazee wataona maono na vijana watatabiri. Wanapokuwa pamoja, wazee huota wakati ujao na kuupitisha kwa vijana, na wakiungwa mkono na wazee, wanaweza kutabiri na kufanya kazi kwa ajili ya siku zijazo. Pamoja na vijana, wasiogope chochote. Mzee mwenye uchungu anahuzunika sana. Yeye ni mbaya zaidi kuliko kijana mwenye huzuni. Kwa hivyo waendelee, kuwa pamoja na vijana.

Mahojiano ya Papa na Infoabe
14 March 2023, 15:46