Papa Francisko:Ndoto yangu ni Kanisa la kichungaji,haki na wazi zaidi!
Vatican News
Kuna jambo moja ambalo limemfurahisha Papa hasa katika miaka ya hivi karibuni: “Kila jambo linalohusu mwenendo wa kichungaji wa msamaha na uelewa wa watu. Kumpa kila mtu nafasi katika Kanisa. Hivi ndivyo Papa Francisko alivyomwambia Elisabetta Piqué, mwandishi wa habari wa gazeti la Argentina La Nación, katika mahojiano yake mapya yaliyotolewa huko katika Nymba ya Mtakatifu Marta mji wa Vatican katika fursa ya maadhimisho ya miaka kumi tangu kuchaguliwa kwake, mnamo tarehe 13 Machi.
Kanisa lililo na milango wazi
Ndoto yake ni kufungua milango kwa sababu anasema:"Kufungua milango, hii inanifaa sana. Kufungua milango na njia za kutembea". Na Kanisa ambalo anafikiri kwa miaka michache ijayo ni Kanisa ambalo ni la kichungaji zaidi, la haki zaidi, na lililo wazi zaidi" kulingana na maelekezo ya yaliyotolewa na Mtaguso wa Pili wa Vatican. Papa Francisko anasema: "Lazima tutembee katika njia hii. Kwa sasa, ukweli wa jambo hili ni mgumu”. Katika mahojiano hayo msisitizao kiukweli wa papa Fransisko alijikita sana juu ya "kondoo waliopotea" na kwamba mtazamo huu umewaweka Wakatoliki katika mgogoro, kama ilivyotokea kwa kaka katika mfano wa mwana mpotevu kwani: "Siku zote hutokea , Papa alithibitisha , Neno kuu la Yesu ambalo ni 'kila mtu'. Kwangu mimi huu ndio ufunguo wa uwazi wa kichungaji. Wote ndani ya nyumba. Ni kelele, lakini kila mtu yumo ndani ya nyumba ". Bila shaka, alisisitiza, kuna upinzani na upinzani katika mabadiliko, hata “Yesu alikuwa na upinzani mwingi” lakini tunatakiwa kutenda katika “uhuru wa Roho Mtakatifu” na kutafuta mapenzi ya Mungu, kwa mapadre na ameonesha haja ya kuwa na mapitio katika seminari.
Mageuzi
Katika suala la mageuzi hayo, alibainisha kuwa “mabaraza yamepangwa kwa upya na Baraza la Makardinali lenyewe sasa liko huru zaidi”. Kwa upande wa uchumi, alitoa heshima kwa Kardinali Pell ambaye alimsaidia kuanzisha mageuzi ya kiuchumi: "Ninamshukuru sana." Sasa Sekretarieti ya Uchumi inanisaidia sana katika maana hii. Kwanza kulikuwa na Padre Guerrero, ambaye katika miaka mitatu na nusu amepanga mambo, na sasa kuna mlei, Maximino Caballero”. Kuhusu uongofu wa upapa uliotajwa katika hati yake ya mwelekeo wa upapa ya, Evangelii Gaudium, alikumbuka kile kilichofanywa na Papa Paulo VI, "mtu muhimu, mtakatifu", na Yohane Paulo II, "mweneza injili mkuu", na Yohane Paulo I, " mchungaji ambaye karibu alitaka kukomesha mambo fulani ambayo hayakuwa sawa" na kutoka kwa Papa Benedikto XVI, "mtu jasiri" ambaye alisimama kwa kina cha mafundisho yake: "Alikuwa Papa wa kwanza kushughulikia rasmi suala la unyanyasaji. Alikuwa Mtaalimungu mkuu, lakini alikuwa ni mtu mwenye msimamo. Ninamkumbuka Benedikto kwa sababu alikuwa ni msindikizaji”.
Haki ya kupiga kura katika Sinodi
Kuhusu sinodi alisisitiza kwamba ni mchakato unaoendelea: "Takriban miaka kumi iliyopita kulikuwa na tafakari ya kina na hati iliundwa ambayo nilitia saini, pamoja na wataalimungu" ambayo ilisemwa: "Hii ndiyo kiwango cha juu tulichofikia, sasa tunahitaji kitu zaidi". Kwa mfano, ilikubaliwa na wote kwamba wanawake hawakuweza kupiga kura: “Hivyo, katika Sinodi ya Amazon swali liliulizwa: Je kwa nini wanawake hawawezi kupiga kura? Je ni Wakristo wa daraja la pili?” Mwandishi wa habari aliuliza ikiwa sasa ni mwanamke mmoja tu au wote watapiga kura na Papa alijibu: "Wale wote wanaoshiriki katika Sinodi watapiga kura. Waalikwa au waangalizi hawatapiga kura. Yeyote anayeshiriki katika Sinodi ana haki ya kupiga kura. Iwe mwanaume au mwanamke. Kila mtu, kila mtu. Neno 'kila mtu' ni la msingi kwangu".
Hatari ya itikadi ya kijinsia
Papa Francisko alithibitisha kwamba haandiki waraka mpya na alijibu kwa ukali juu ya swali ambao iwapo ameombwa kuandika waraka kuhusu mada ya jinsia. Katika suala hilo, anakariri kwamba "daima anatofautisha kazi ya uchungaji na watu wa mwelekeo tofauti wa kijinsia na itikadi ya kijinsia. Ni vitu viwili tofauti. Itikadi ya jinsia, hivi sasa, ni moja ya ukoloni hatari zaidi wa kiitikadi. Inapita zaidi ya nyanja ya ngono. Kwa nini ni hatari? Kwa sababu inapunguza tofauti, na utajiri wa wanaume na wanawake na wa ubinadamu wote ni mvutano wa tofauti. Inakua kupitia mvutano wa tofauti. Swali la jinsia hupunguza tofauti na hufanya ulimwengu uonekane sawa, wote katika mstari sawa. Na hili linakwenda kinyume na wito wa mwanadamu”.
Kuhusu Ukraine
Na katika mada ya Ukraine, alimuuliza Papa ikiwa mauaji yanayotokea katika nchi hiyo yanaweza kufafanuliwa kama mauaji ya halaiki: “Hakika ni neno la kitaalamu, mauaji ya kimbari, lakini ni dhahiri kwamba wakati shule za mabomu, hospitali, makazi, hisia sio sana ya kuchukua mahali, lakini kuharibu ... sijui kama haya ni mauaji ya kimbari au la, lazima isomewe, lazima ifafanuliwe vizuri na watu, lakini kwa hakika si maadili ya vita ambayo tumeyazoea”. Papa anaongeza kuwa kwa sasa Vatican inafanya kazi kupitia njia za kidiplomasia, ili kuona kama kuna kitu kinaweza kupatikana, lakini inabainisha kuwa hakuna mpango wa amani kutoka Vatican, kuna huduma ya amani ambayo inaendelea mbele, busara, pamoja na wale walio tayari kwa mazungumzo, pia kwa kuzingatia mkutano wa wawakilishi katika ngazi ya dunia kuhusu suala hili: Vatican inafanya kazi.
Papa akakariri: “Niko tayari kwenda Kiev. Nataka kwenda Kiev. Lakini katika hali ya kwenda Moscow. Katika suala la nitakwenda sehemu zote mbili au hapana." Alipoulizwa kama haiwezekani kwenda Moscow, alijibu: “Siyo jambo lisilowezekana… sisemi kwamba inawezekana. Si jambo lisilowezekana. Hebu tutumaini kwamba tutafanikiwa… hakuna ahadi, hakuna chochote. Sikuufunga mlango huo.” Lakini Putin anaifunga au la? Aliulizwa, naye Papa akajibu: “Lakini labda atakengeushwa na kufungua, sijui”. “Vita inaniumiza ndivyo ninamaanisha. Vita inaniumiza” aliongeza.
Safari inayoewezakana nchini Argentina
Kisha kuna mada ya safari inayowezekana kwenda Argentina. Ambapo Papa akiri kwamba anatamani kwenda Argentina na kwamba ikiwa hajafanya hivyo hadi sasa ni kwa sababu kadhaa ambazo zimeongeza baada ya muda: “Hakukuwa na kukataa kwenda, kila kitu kilipangwa ... ilitokea kwamba mambo yakawa magumu ... kulikuwa na miaka miwili ya janga la uviko ambalo lililipua safari ambazo zilipaswa kufanywa ... nataka kwenda, natumai kwenda. Natumai naweza kufanya hivyo.” Lakini anaongeza: “Wokovu wa nchi hautatokana na safari zangu. Nitakwenda kwa hiari, lakini fikiria juu ya mambo ambayo yanahitajika kufanywa ili nchi isonge mbele”.
Kuua jinsi ya kuwa na subira
Hatimaye, akijibu swali kuhusu makosa yaliyofanywa katika miaka hii kumi ya upapa wake, Papa anaonesha sababu ya kila kosa, kutokuwa na subira: “Wakati fulani damu yangu hukimbia kichwani mwangu. Kisha unashindwa kujizuia na ukikosa amani unateleza na kufanya makosa. Lazima ujue jinsi ya kusubiri.”