Papa Francisko: Mkristo aliyebatizwa anayo ari na ushuhuda wa kuinjilisha
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Katika katekesi ya mwisho tuliona kwamba Mtaguso wa kwanza katika historia ya Kanisa kama ule wa II wa Vatican, ambapo wa kwanza uliitishwa huko Yerusalemu kwa ajili ya suala linalohusiana na uinjilishaji, yaani, tangazo la Habari Njema kwa wasio Wayahudi, ilifikiriwa kwamba tangazo la Injili lilipaswa kuletwa kwa Wayahudi pekee. Katika karne ya 20, Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican uliwasilisha Kanisa kama Hija ya Watu wa Mungu kwa wakati na kimisionari kwa asili (taz Dikrii ya Ad Gentes, 2). Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko amenza tafakari yake ya Katekesi kwa waamini na mahujaji waliofika katika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican, Jumatano tarehe 8 Machi 2023. Baba Mtakatifu amesema “Je hii ina maana gani? Kuna kama daraja kati ya Mtaguso wa kwanza na wa mwisho, katika ishara ya uinjilishaji, daraja ambalo mbunifu wake ni Roho Mtakatifu.
Leo hii tunasikiliza Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, ili kugundua kwamba uinjilishaji daima ni huduma ya kikanisa, na kamwe si ya faragha, kamwe haijatengwa au, kamwe si ya mtu binafsi. “Siku zote uinjilishaji unafanywa katika eklesia, yaani katika jumuiya na bila kugeuza imani kwa sababu huo si uinjilishaji”. Kiukweli, sikuzote mwinjilishaji hupitisha mambo ambayo amepokea. Mtakatifu Paulo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuiandika kwa: “injili aliyoitangaza na ambayo jumuiya ziliipokea na walikaa imara ni ile ile ambayo Mtume naye aliipokea (rej. 1Kor 15:1-3). “Imani inapokelewa na imani hupitishwa”. Mwenendo huu wa kikanisa wa uwasilishaji wa Ujumbe ni wa lazima na unahakikisha uhalisi wa tangazo la Kikristo. Paulo mwenyewe anawaandikia Wagalatia hivi: “ Ikiwa sisi wenyewe au malaika kutoka mbinguni atawahubiri ninyi Injili tofauti na ile tuliyowahubiri, na alaaniwe” (1:8). “Hii ni nzuri na hii ni nzuri kwa maono mengi ambayo ni ya mtindo ...”, Papa amesisitiza
Kwa hiyo mwelekeo wa kikanisa wa uinjilishaji unajumuisha kigezo cha kuthibitisha ari ya kitume. Uthibitishaji wa lazima, kwa sababu jaribu la kuendelea kufanya binafsi daima linanyemelea, hasa wakati njia inakuwa mbaya na tunahisi uzito wa jitihada. Hatari sawa ni jaribu la kufuata njia rahisi za kikanisa ya kughushi, kupitisha mantiki za kidunia na tafiti, kutegemea nguvu ya mawazo yetu, programu, miundo, ya mahusiano muhimu. Hii si sawa, hii inapaswa kusaidia kidogo lakini nguvu ambayo Roho anatupatia kutangaza ukweli wa Yesu Kristo, kutangaza Injili, ni ya msingi. Mambo mengine ni ya ziada. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amependa kujikita zaidi katika shule ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, kwa kusema tena baadhi ya vipengele vya Hati ya Dikrii ya Ad Gentes (AG), ni hati juu ya shughuli za kimisionari za Kanisa. Maandiko haya ya Mtaguso wa II wa Vatican yanahifadhi thamani yake kikamilifu hata katika muktadha wetu wa changamano na wingi.
Baba Mtakatifu awali ya yote, waraka huu, AG, unatualika kuuzingatia upendo wa Mungu Baba, kama chanzo, ambacho “kwa ukarimu wake mkubwa na wa huruma ya ukombozi hutuumba na, zaidi ya hayo, kwa neema hutuita kushiriki katika maisha yake na katika utukufu wake. Huu ndio wito wetu. Kwa ukarimu mtupu amemimina na anaendelea kumimina wema wake wa kimungu, ili kwamba, kama yeye ni muumba wa yote, aweze pia “kuwa yote katika yote” (1 Kor 15:28), akipata utukufu wake pamoja na furaha yetu"(n. 2). Kifungu hiki ni cha msingi, kwa sababu kinasema kwamba upendo wa Baba una kila hatima ya mwanadamu kama mpokeaji wake. “Upendo wa Mungu si wa kikundi kidogo tu,… kwa kila mtu. Baba Mtakatifu amesisitiza kuzingatia vema akilini na moyoni kwamba kila mtu, hakuna mtu aliyetengwa, ndivyo anasema Bwana. Na upendo huu kwa kila mwanadamu ni upendo unaomfikia kila mwanamume na mwanamke kupitia utume wa Yesu mpatanishi wa wokovu na mkombozi wetu (rej. AG, 3), na kupitia utume wa Roho Mtakatifu (rej. AG, 4), ambaye , Roho Mtakatifu, hutenda kazi ndani ya kila mtu, katika waliobatizwa na wasiobatizwa. Roho Mtakatifu anafanya kazi!”
Zaidi ya hayo, Mtaguso unakumbuka kwamba, ni wajibu wa Kanisa kuendeleza utume wa Kristo, ambaye “alitumwa kuwahubiri maskini habari njema; kwa hili hati ya kitume ya Ad gentes inabainishw a kuwa ni muhimu kwamba Kanisa, daima chini ya ushawishi wa Roho Mtakatifu, Roho wa Kristo, hufuata njia sawa na hizi, yaani, njia ya umaskini, utii, huduma na ya sadaka yake mwenyewe hadi kifo, ambapo aliibuka mshindi kwa kufufuka tena” (AG, 5). Iwapo litaendelea kuwa mwaminifu kwa “njia” hii, utume wa Kanisa ni "udhihirisho, yaani, epifania na utambuzi, wa mpango wa kimungu katika ulimwengu na katika historia” (AG, 9). Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema, maelezo haya mafupi pia yanatusaidia kuelewa maana ya kikanisa ya ari ya kitume ya kila mmisionari, mfuasi. “Ari ya kitume si shauku, ni kitu kingine, ni neema ya Mungu, ambayo tunapaswa kuienzi. Ni lazima kuelewa maana kwa sababu katika Hija na kuinjilisha Watu wa Mungu hakuna masomo ya kazi na wanaokaa. Hakuna wale wanaohubiri, wale wanaotangaza Injili kwa njia moja au nyingine, na wale wanaonyamaza tu. Hapana."
Baba Mtakatifu Francisko: “Kila mtu aliyebatizwa kwa mujibu wa Wasia wa Evangelii Gaudium , kwa chochote kile cha kazi yake katika Kanisa na kiwango cha elimu ya imani yake, ni somo hai la uinjilishaji" (Evangelii Gaudium, 120). “Je, wewe ni Mkristo? “Ndiyo, nilipokea Ubatizo…” Na je, unainjilisha? Lakini hii inamaanisha nini ...? Ikiwa ni mwinjilishaji na hutoi ushuhuda, wa Ubatizo uliopokea, wa imani ambayo Bwana amekupatia,wewe si Mkristo mwema. Kwa sababu ni kwa nguvu ya Ubatizo uliopokelewa na matokeo yake ya kuingizwa katika Kanisa, kila mtu aliyebatizwa anashiriki katika utume wa Kanisa na, ndani yake, katika utume wa Kristo Mfalme, Kuhani na Nabii”. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba shughuli hiyo ni moja na haibadiliki katika kila mahali na katika kila hali, hata kama haifanyiki kwa njia sawa kwa misingi ya hali tofauti" (AG, 6). Hii inatualika kutofungamana au kujiweka kisukuku; kwani anatukomboa kutoka katika hali hii ya kutotulia ambayo si ya Mungu.
Ari ya kimisionari ya mwamini pia inajieleza kama ubunifu wa kutafuta njia mpya za kutangaza na kutoa ushuhuda, wa njia mpya za kukutana na wanadamu waliojeruhiwa ambao Kristo alichukua juu yake mwenyewe. Kwa ufupi, njia mpya za kutoa huduma kwa ajili ya Injili na kutoa huduma kwa ajili ya wanadamu. “Uinjilishaji ni huduma. Ikiwa mtu anajiita mwinjilishaji na hana tabia hiyo, moyo huo wa mtumishi, na kuamini kuwa yeye ni bwana, yeye si mwinjilishaji, hapana... ni maskini”. Kurudi kwenye upendo kimsingi wa Baba na utume wa Mwana na Roho Mtakatifu hatufungi katika nafasi za utulivu wa kibinafsi. Kinyume chake, unatuongoza kutambua zawadi ya bure ya utimilifu wa maisha ambayo tumeitwa, zawadi hii ambayo kwayo tunamsifu na kumshukuru Mungu. Zawadi hii si kwa ajili yetu tu, bali ni kuwapatia wengine. Na pia inatuongoza kuishi kwa ukamilifu zaidi yale tuliyopokea kwa kuyashirikisha na wengine, tukiwa na hisia ya kuwajibika na kutembea pamoja kwenye njia zenye mateso na ngumu za historia, tukiwa makini na kwa ari tukingojea utimilifu wake. “Tumwombe Bwana neema hii, tuchukue wito huu wa Kikristo mikononi mwetu na kumshukuru Bwana kwa yale aliyotupatia, hazina hii. Na tujaribu kuwasiliana na wengine.”