Papa Francisko:Mawazo kwa wanafunzi waliopata ajali huko Ugiriki
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Mawazo ya kwanza ya Papa Francisko katika salamu zake baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Dominika Machi 5 yamewaendea wahanga na familia zao za mkasa wa treni nchini Ugiriki. Papa amesema “Siku hizi, mawazo mara nyingi yaligeuka kwa waathika wa ajali ya Treni huko Ugiriki: wengi walikuwa wanafunzi vijana. Ninawaombea marehemu; Niko karibu na majeruhi, wanafamilia, Mama Yetu awafariji”.
Wakati huo huo, nchi imepokea samahani kutoka kwa waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis. “Ninaomba radhi kwa jamaa wa waathirika" ni Maneno ya mkuu wa serikali siku tano baada ya mkasa wa treni, huko Larissa, kati ya Thessalonike na Athene, ambayo ilisababisha vifo vya watu 57, vilivyotokana na makosa ya kibinadamu na uzembe, ambao bado leo hii wanashughulikia. Nchi nzima lakini, zaidi ya yote, kwa familia za wale waliouawa katika janga hilo, wanaandamana wakiomba “kujua kwa kile kilichotokea na kueleza kwamba huko Ugiriki mnamo 2023, haiwezekani kwa treni mbili kusafiri kwa njia tofauti kwenye mstari huo huo na usitambuliwe na Mtu.
Wakati huo huo, maandamano hayo yanaendelea, Dominika tarehe 5 Machi asubuhi wanafunzi, wafanyakazi wa reli na wafanyakazi wa sekta ya umma walikusanyika kwa maandamano muhimu dhidi ya serikali katikati ya jiji, katika uwanja wa Syntagma, mbele ya Bunge, ambapo zaidi ya watu elfu saba walikusanyika lakini pia kutokea mapigano kati ya polisi na waandamanaji. Jamaa wa waathiriwa badala yake walikusanyika karibu na eneo la mkasa. Wakati huohuo kikao cha mkuu wa kituo mwenye umri wa miaka 59 anayedaiwa kufanya kosa la vifo kilichosababisha ajali ya magari hayo mawili kugongana kimeahirishwa. Jaji mchunguzi wa Larissa atalazimika kuamua kama atapinga uhalifu wa kuua bila kukusudia.