Papa:mafundisho ya Mtaguso wa II wa Vatican yahamasisha Sanaa Takatifu
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Katika fursa ya Mkutano wa XXVI wa adhara kwa Taasisi za Kipapa, Papa Francisko amefurahi kuwaelekeza matashi mema kuanzia na Kardinali José Tolentino de Mendonça kwa ajili ya huduma wa urais wa Baraza la Uratibu kati ya Taasisi za kitaaluma za kipapa. Kiukweli yeye amekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni na Elumu ambapo amechukua jumumu hata katika kazi hiyo na kujikita katika Roho na kwa mujibu wa Katiba ya Kitume ya Praedicate Evangelium (cfr Art. 162). Papa Francisko amependa kuelezea shukrani zake kwa Kardinali Gianfranco Ravasi,ambaye kwa miaka kumi na tano aliongoza Baraza la Uratibu kwa kutoa mwamko mkubwa wa maisha ya Taasisi za Kitaaluma za Kipapa na kuthamanisha Mikutano kwa Umma. Amewasalima Marais na wajumbe wote walioshiriki na hata viongozi wa mamlaka ambao wanashiriki Mkutano wa kiutamadun.
Tuzo kwa ajili ya sanaa
Baba Mtakatifu amebainisha kuwa Wanataaluma wameomba, kwa ajili ya toleo hilo la Mkutano wa adhara kutoa Tuzo, na kwa hiyo mapendekezo ya wale ambao, katika nyadhifa mbalimbali, wanashughulikia sanaa Takatifu na kwa hiyo kupanga, kuanzisha, kurekebisha liturujia na kutumia tena nafasi zilizokusudiwa kwa ajili ya ibada, kwa kuzingatia mahitaji mapya na lugha ya kisasa ya usanifu. "Tunajua vizuri jinsi mazingira ya maadhimisho yalivyo muhimu katika kukuza sala na hisia ya ushirika: nafasi, mwanga, sauti, rangi, picha, ishara, vyombo vya kiliturujia vinajumuisha vipengele vya msingi vya ukweli huo, wa tukio hilo la binadamu na kimungu kwa wakati mmoja, ambayo ndiyo hasa liturujia. Kwa hiyo Kikao hicho kiliwaonawa kupewa tuzo ya Taasisi ya kipapa ya Elimu kwa ajili ya Barua Nzuri na Sanaa Kuu ya Pantheon, ambayo ni taasisi kongwe zaidi kati ya taasisi zinazowakilishwa katika Baraza kwa Rais, wake Profesa Pio Baldi. Papa amesema Mada ambayo ni ya sasa na mihimu kwa sababu ni hatua na mara nyingi hata hai , mjadala kuhusu mapendekezo ya upyaisho wa Akiolojia Takatifu, ambayo ina kazi kubwa ya kuunda, hasa katika mitaa mipya, iwe ya pembeni katika mji na katika vituo vya mijini, nafasi zinazotofja katika jumuiya ya kikristo ambayo inaweza kusheherekea utakatifu wa litutujia kwa mujibu wa magunzoshi ya Mtaguso II wa Vatican.
Baba Mtakatifu amependa kukazia juu ya Barua ya kitume ya Desiderio desideravi ambayo imejikita hasa juu ya mafunzo ya kiliturujia kwa ajili ya watu wa Mungu ili kususuitza mantiki mbili ambazo kwa hakika ni swa hata katika matatizo ya akiolojia na kisanii. Kwanza kabisa ni muhimu kutafuta lugha ya alamua ya kua na iwezo wa kuilewa: Kupoteza uwezo wa kuelewa thamani ya mfano ya mwili na kila kiumbe hufanya lugha ya mfano ya Liturujia isiweze kufikiwa na mwanadamu wa kisasa. Hata hivyo, si suala la kuacha lugha hii: haiwezekani kuiacha kwa sababu ndiyo Utatu Mtakatifu Zaidi umechagua kutufikia katika mwili wa Neno. Badala yake, ni suala la kurejesha uwezo wa kuweka na kuelewa alama za liturujia (n. 44).
Mantiki nyingine muhimu ilikuwa shughuli za kisanaa na akiolojia ambayo katika maono ya kikristo yanatoa shughuli yenyewe ya maisha ya liturujia, katika matendo ya Roho na sio tu kitu cha kibinadamu. Kwa hiyo Barua ya Kitume inaendelea kuwa“Ni muhimu kujua jinsi Roho Mtakatifu anavyotenda katika kila maadhimisho: sanaa ya kusherehekea lazima ipatane na utendaji wa Roho. Ni kwa njia hiyo tu itakuwa huru kutokana na dhana [...] na tamaduni [...]. Mbinu inatosha kwa fundi; msanii, pamoja na ujuzi wa kiufundi, hawezi kukosa msukumo, ambayo ni aina chanya ya milki: msanii, yule wa kweli, hana sanaa bali anamilikiwa nayo.”(49-50).
Kwa kupokea mapandekezo ambayo Taasisi za kitaaluma wameweka kwa ajili ya Tuzo la uwakilishi wa toleo hilo, Papa Francisko amekuwa na furaha ya kutoa Medali ya dhahabu ya Kipapa ya Tuzo za Kipapa kwa ajili ya Taasisi za Kipapa katika Mafunzo OPPS, kwa upangaji upya na marekebisho ya kiliturujia ya Kikanisa cha Msingi la Watakatifu Francis wa Assisi na Katherine wa Siena huko Roma. Papa amemtukia Medali ya shaba ya Kipapa kwa Mwanaakiolojia Federica Frino, kwa ajili ya mpango wa Kanisa jipya la Mtakatifu Tommaso huko Pontedera. Kwa kuhitimisha amewatakia wote wahusika wa kielemu juhuda yenye matunda katika muktadha wote wa utafiti na huduma na kuwakabidhi chini ta ulinzi wa Mama yetu Bikira Maria, Hekalu na Sanduku la Agano, na kuwaomba sala zao huku akiwabariki kwa moyo na baraka ya kitume.