Papa Francisko:Kanisa lazima litoke nje yake kukutana na mwili wa Fumbo!
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican tarehe 11 Machi 2023 na wajumbe wa Tume ya Baraza la Maaskofu wa Hispania kwa ajili ya Utume na ushirikiano na Makanisa na bodi ya utendaji ya NGO ‘Misión América’. Katika hotuba yake kwa lugha ya Kihispaniia anaeleza alivyoelezwa kuwa utume wa Amerika Kusini unadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, kwamba unakaribia kuwa muda kama ule wa Kristo wakati wa Mateso na Kifo chake. Katika furaha hii muhimu tarehe ambayo wamependa kutembelea Makao makuu ya Petro, ili kupyaisha jitihada zao na Kanisa la Ulimwengu, ambalo linatimizwa katika kazi yao kwa ajili ya utume wa Amerika na Afrika. Baba Mtakatifu amewaalika kwa miaka mitatu inayokosekana kufikia umri kamili uwe ni mchakato wa safari ya kina ambayo wanaweza kuendelea na tabia ya kujitambulisha na Kristo. Katika kile ambacho Kristo alisema: “Kama Baba alivyo nituma mimi, nami ninawatuma ninyi (Yh 20,21, kwa namna ya Kanisa kujifungulia utume. Kanisa lazima litoke nje, lazima likae mtaani. Andiko hilo kutoka Ufunuo linamweleza mengi. Yesu anasema “niko mlangoni nabisha hodi”. Kulingana na jibu, nitaingia, kukaa na wewe, kula. Tatizo la leo hii ni tofauti kidogo.
Yesu anaendelea kubisha mlango, lakini mara nyingi hatutoki ndani ili tumfungulie mlango na kumwacha aingine na kutoa. Nadhani hii ni changamoto ya leo. Kufunga Kanisa katika utume. Lakini kiukweli kazi yao tayari waliyoipitia ni muhimu katika mchakato wa safari. Kwa hakika mchakato wao unajikita katika maneno manne ambayo yanajilezea kuwa ni mwonekano, heshima, kujitolea na kushirikiana. Kwa hiyo Papa amesema itakuwa vizuri kusoma vema katika nuru ya Injili ya utume. Kwa hakika katika neno ambalo ametaja, Yesu anawaonesha kwanza kabisa, mikono na ubavu. Inashangaza picha hiyo kwa sababu kwa maana nyingine inakusanya mtindo ambao Yesu alitumwa na Baba yake na sasa anawatuma wao, kwa kuonesha uhalisia wa uchungu, wa dhambi na kifo si kwa ajili ya kuhukumu kila mmoja lakini kwa kuponesha kwa kina ubinadamu, na kujitwika mwenyewe katika nafsi yake. Wakati huo huo mfano, katika kuandaa kampeni ya kuhamasisha ili kufikia hali halisi ya Amerika Kusini, upendo wao ambao siyo kitu kingine ambacho wanawacha kuona juu yake katika mkono uliofunguliwa wazi wa Yesu ambaye katika madonda yake yanatupatia kimbilio bora.
Andiko la kibiblia, kama wao wanavyotambua, linaendelea na tukio la Mtakatifu Thomas. Ni wazo jingine linalovutia mbali ya thamani ya kitaalimungu ya kusimulia, hiyo kulinganisha na mwingine, katika wakati wake na nafasi zake. Yesu daima ni makini kwa hitaji, hasa kwa mtu katika utu wake katika Kanisa. Ni ukweli wa usawa, ukweli wa haki na halazimishi mchakato mmoja na wa kipee kwa wote, lakini wa kuwa na uwezo wa kumsindikiza kila mmoja, katika uhuru wake na mahitaji yake ili wote waweze kujua wito wa Mungu na mpango wa upendo kwa kila mmoja wao. Zaidi ya hayo, Yesu katika tukio hilo, kulingana na Injili ya Yohane, anawamiminia Roho Mtakatifu wanafunzi, akiwapa zawadi hiyo nguvu na mamlaka ya kutekeleza utume waliokabidhiwa. Kuanzia wakati huo na kuendelea, ni kana kwamba wanafunzi waliingia katika ngazi nyingine, yenye bidii zaidi na ya kustaajabisha. Kwa njia hiyo hiyo, na daima kutambua kwamba nguvu zetu ziko kwa Mungu tu, kujaribu kutoa, kuanzia Kanisa la Hispania, kwa wito huu wa kujitolea kwa bidii, ambayo si kitu kingine isipokuwa kusaidia kwa sala, kazi, mshikamano, wale ambao wakiongozwa na Roho huyo huyo wanakwenda ulimwenguni wakihubiri Habari Njema ya Ufalme.
Hatimaye, neno muhimu kwa kuelewa zawadi kubwa ya ufufuko wa Bwana: "Amani iwe nanyi”. Ingawa haiwezekani kufahamu maana yote ambayo ni ya dhana hii unaitafsiri kwa ushirikiano. Ni kitu kizuri, ina maana kwamba “amani” ambayo Mungu anaiweka na mwanadamu na kati ya wanadamu inabadilisha kuwepo kwetu, inakuwa maisha ya kila siku katika kutembea pamoja, katika kutafuta mema, katika kueneza upendo na maelewano; kuzalisha ukweli mpya, kujenga madaraja, kuharibu hofu na manung'uniko, yale yale ambayo, kama andiko la Biblia linavyoonesha, yaliwaweka wanafunzi wamefungwa. Yesu akubariki kweli kwa yale unayofanya. Utasema kuwa ni kitu kidogo, kwamba ni "nyumbani" sana. Lakini vitu vidogo, vitu "vya nyumbani" ndivyo vinavyodumu zaidi, wakati mwingine vitu vikubwa havidumu. Bikira Mtakatifu awasindikize. Na wasipoteze hali yao nzuri.
Katika sura hii ya Yesu anayelituma Kanisa lake katika utume iwe kichocheo kwao, ili kutoa mwonekano wa majeraha ambayo bado yanaonekana katika Mwili wake wa fumbo; kudai heshima ya kila mtu na haki yake ya kuweza kutambua njia ambayo Mungu anamfuata; kufanya kazi na kutegemeza kazi ya wale wote ambao, kama sisi, wametumwa, wakishirikiana na watu wote wenye nia njema, kwa utukufu wa Mungu ambaye si mwingine ila mwanadamu aliye hai (rej. Mtakatifu Irenaeus, Dhidi ya uzushi; 4, 20.5-7). Baba Mtakatifu ameesema Yesu awabariki na Bikira Mtakatifu awasindikize katika safari hii. Na tafadhali wasisahau kumwombea.