Papa Francisko:Askofu O'Connell aliwajali maskini
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Papa Francisko alimsifu marehemu Askofu David O’Connell kwa miaka yake kama kasisi na askofu huko LA katika ujumbe maalum wa rambirambi uliotangazwa hadharani mnamo tarehe 1 Machi 2023. Ujumbe wa Papa ulisomwa na Askofu Mkuu José H. Gomez wakati wa hotuba ya ufunguzi mbele ya umati uliojaa kwenye Misa maalum ya kumbu kumbu yake Jumatano usiku katika Kanisa la Mtakatifu Yohane Vianney huko Hacienda Heights, katika parokia ambayo Askofu O'Connell aliishi.
Kwa mjia hiyo katika ujumbe wa salamu za rambirambi wa Baba Mtakatifu Francisko ametoa uhakikisho wa ukaribu wake wa kiroho kwa makasisi, watawa na waamini walei wa Jimbo kuu,la Los Angeles, katika ujumbe uliotiwa saini na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin. “Nimesikitishwa sana kusikia kifo cha ghafla na cha kusikitisha cha Askofu Msaidizi David O'Connell,” umeandikwa ujumbe huo uliwasilishwa kwa Askofu Mkuu Gomez na Askofu Mkuu Christophe Pierre, Balozi wa Vatican nchini Marekani, mapema Juma hili.
Papa alimpongeza sana kwa “huduma ya Askofu O'Connell kama padre na Askofu kwa alivyo tambuliwa hasa kwa kuwajali sana maskini, wahamiaji, na wenye mahitaji, jitihada zake za kushikilia utakatifu na adhama ya zawadi ya uhai ya Mungu, na bidii yake kwa ajili ya maisha. kuhamasisha mshikamano, ushirikiano, na amani ndani ya jumuiya ya eneo hilo.” Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo alisali kwamba wale wanaoheshimu kumbukumbu ya O’Connell wathibitishwe katika azimio la kukataa njia za jeuri na kushinda uovu kwa wema. “Kwa wale waliokusanyika kwa ajili ya Misa ya kumumbu na mazishi Kikristo na wote wanaoomboleza kifo cha Askofu O'Connell, kwa matumaini ya uhakika ya ufufuko,” na hatimaye katika ujumbe alihitimisha, "Baba Mtakatifu kwa “kuwapa baraka zake kama ahadi ya amani na faraja katika Bwana.”
Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Yohane M Vianney iliandaliwa na Jimbo kuu la Mtakatifu Gabriel, Kanda ya Kichungaji, ambayo Askofu O’Connell aliisimamia kama kuhani na kama Askofu kuanzia mnamo mwaka 2015 hadi kifo chake mwezi uliopita. Mtazamo wa siku nzima kuhusu Marehemu Askofu O'Connell katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Malaika ulipangwa kufanyika Alhamisi, tarehe 2 Machi na vile vile saa 1 jioni ambayo itakuwa misa ya mkesha. Na Misa ya mazishi ya Askofu O'Connell itafanyika saa 5 asubuhi siku ya Ijumaa tarehe 3 Machi 2023 kwenye Kanisa Kuu, ikifuatiwa na maziko ya kibinafsi katika Kikanisa cha Kanisa Kuu hilo. Zaidi ya maaskofu 20 wanatarajiwa kuhudhuria.