Papa apyaisha Baraza la Makardinali:C9
Vatican News.
Papa Francisko amepyaisha Baraza la Makardinali, liitwalo 'C9', kwani muda wake umekwisha. Kwa njia hiyo amewateua wajumbe wa Baraza jipya ambao ni makadinali: Pietro Parolin, Katibu wa Vatican; Fernando Vérgez Alzaga, rais mjiwa Vatican; Fridolin Ambongo Besungu, Askofu mkuu wa Kinshasa; Oswald Gracias, Askofu Mkuu wa Bombay; Seán Patrick O'Malley, Askofu Mkuu wa Boston; Juan José Omella Omella, Askofu mkuu wa Barcelona; Gérald Lacroix, Askofu mkuu wa Québec; Jean-Claude Hollerich, Askofu mkuu wa Luxembourg; Sérgio da Rocha, Askofu mkuu wa Mtakatifu Salvador de Bahia.
Katibu wa tume hiyo ni Askofu Marco Mellino, wa Cresima. Mkutano utakaofuata wa Baraza la washauri utafanyika mnamo tarehe 24 Aprili saa 3.00 asubuhi katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, Vatican. Mkutano wa mwisho wa Baraza hilo uliofanyika mnamo Desemba mwaka 2022, ambao ulijikita miongoni mwa mada nyingine juu ya awamu ya bara ya Sinodi inayoendelea sasa. Mkutano wa kwanza kabisa ulifanyika kuanzia tarehe 1 hadi 3 Oktoba 2013.
Baraza la Makardinali lilianzishwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa barua ya mkono wake tarehe 28 Septemba 2013 kwa ajili ya jukumu la kumsaidia katika utawala wa Kanisa la Ulimwengu na kusoma mpango wa marekebisho ya Curia Romana ambayo mwisho wake unatekelezwa na Katiba mpya ya Kitume iitwayo 'Praedicate Evangelium' iliyochapishwa mnamo tarehe 19 Machi 2022. Kwa mujibu wa maandishi ya mkono wa Papa yanasomeka kuwa: “Baraza la Makardinali linakusudiwa kama kielelezo zaidi ya ushirika wa kiaskofu na usaidizi wa munus petrinum ambao Uaskofu wa ulimwengu unaweza kutolewa”.