Tafuta

2023.03.28  Papa ametuma msaada wa dawa kwenda Uturuki kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la Ardhi. 2023.03.28 Papa ametuma msaada wa dawa kwenda Uturuki kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la Ardhi. 

Papa ametuma nchini Uturuki madawa elfu kumi kwa ajili ya waathirika wa tetemeko

Madawa ambayo yatawasili kwa njia ya Ndege za Uturuki,yanapelekwa kwa watu wa Uturuki waliokumbwa na tetemeko kali mwezi Februari.Mkuu wa Sadaka ya Kitume kwa maagizo ya Papa ametuma madawa kwa ushirikiano na Balozi wa Vatican huko Uturuki.Hata hivyo CEI pia inaendelea kukusanya msaada kwa ajili ya watu wa Siria na Uturuki.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa mra nyingine tena baada ya tetemeko la nguvu la mnamo tarehe 6 Februari iliyopita ambayo iliikumba nchi ya Siria na Uturuki kwa kusababisha waahirika zaidi ya hamsini elfu, Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, wanaendelea kutoa msaada kwa maagizo ya Papa ili kutuma huko Jijini Instanbul Mzigo mkubwa  mpya wa madawa. Utumaji wa kwanza ulifanywa Jumatatu tarehe 27 Machi lakini unaendelea hata tarehe 28 Machi pia. Hizi ni dawa 10,000 ambazo zilinunuliwa kwa pendekezo la Ubalozi wa Uturuki uliopo Vatican Holy ambaye anafahamu hali ya  nchi yake. Nchini Siria, iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi na vita na watu milioni 15 katika shida, misaada ya kiuchumi kutoka kwa Papa tayari iliwasili katika siku za nyuma shukrani kwa Ubalzoi wa Vatican  ambao naona kuitumia kwa ajili ya wakazi.

Msaada wa madawa kutoka kwa Papa kuelekea Uturuki
Msaada wa madawa kutoka kwa Papa kuelekea Uturuki

Kwa mujibu wa Kadinali Konrad Krajewski, Mkuu wa Huduma ya Upendo ya Kipapa amesema wanatuma msaada kupitia ndege za Uturuki kwa kuzingatia urefu wa Mabox na uzito.  Hiyo ni tiba ambayo inawezekana kutokana na usaidizi wa watu wanaojitolea. Tayari baada ya tetemeko la ardhi lililosababisha takriban watu milioni 2 waliokimbia makazi yao nchini Uturuki, Mkuu wa sadaka hiyo alikuwa amesonga mbele kwa msaada ambao sio tu na madawa bali zaidi ya vyakula vya makopo kama mchele na tuna, sweta za mafuta na nyenzo nyinginezo zinazoweza kustahimili muda na hata baridi. Wakati huo huo, Utume wa  Siria na Uturuki alikwenda Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Makanisa ya Mashariki, Kardinali  Claudio Gugerotti.

Maaskofu Italia CEI wanaendelea na kukusanya msaada kwa Siria na Uturuki hadi 30 Aprili

Dominika tarehe 26 Machi michango ilikusanywa katika makanisa yote ya Italia ili kugawanywa, kulingana na maelekezo ya Baraza la maaskofu Italia ( CEI), kwa wakazi wa Uturuki na Siria kama ishara halisi ya mshikamano na ushiriki wa waamini wote katika mahitaji ya kimwili na ya kiroho kwa  waathirika wa tetemeko la ardhi. Hata hivyo, inawezekana kuendelea kuchangia hadi tarehe 30 Aprili 2023 pia kwa kutumia akaunti ya sasa ya posta Na. 347013, au mchango wa mtandaoni kupitia tovuti www.caritas.it au uhamisho wa benki unaobainisha “Tetemeko la Uturuki-Siria 20232 kwa sababu ya malipo. Ili kukabiliana na dharura za kwanza, CEI imepanga mgao wa awali wa Euro 500,000 kutoka katika fedha za 8xmille.

28 March 2023, 16:04