Tafuta

Papa akutana na wakimbizi kupitia mikondo ya kibinadamu na kupongeza umoja

Papa Francisko amekutana na wakimbizi waliofika Ulaya kupitia mpango wa pamoja wa Mtakatifu Egidio,Makanisa ya Kiinjili, Meza ya Waaldensia na Kanisa la Italia:Papa amewashukuru Wakristo wanapoungana kufanya kazi pamoja kama ndugu.Shughuli yao ni muafaka kwa wakati huu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 18 Machi 2023, amekutana na wakimbizi waliofika Ulaya kwa njia ya mikondo ya kibinadamu na wawakilishi wa Jumuiya zinazowakaribisha. Akianza hotuba yake ameshukuru hotuba zilizotangulia kuelezea mpango na kwa ajili ya kujitoa kwao ushuhuda. Ni furaha yake kukutana na wakimbizi wengi pamoja na familia zao waliofika nchini Italia, Ufaransa, Ubelgiji na Andora kwa kupitia njia ya mikondo ya kibinadamu. Utimizwaji wake umetokana na ubunifu wa ukarimu wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Shirikisho la Makanisa ya Kiinjili na Meza ya Waaldensia na pia mtandao wa makaribisho wa Kanisa katoliki la Italia kwa namna ya pekee Caritas na pamoja na juhudi za Serikali ya Italia na Nchi nyingine ambazo zimewapokea. Mikondo ya kibinadamu ilizinduliwa mnamo 2016 kama jibu la hali inayozidi kuwa mbaya kwenye njia ya Mediterania.

Leo hii tunapaswa kusema kwamba mpango huo ni wa kwa wakati unaofaa katika kipindi cha kusikitisha kiukweli, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali; na kwa bahati mbaya pia ajali ya hivi karibuni ya meli ya Cutro inathibitisha hali halisi hiyo. Ajali hiyo ya meli haikupaswa kutokea, na kila linalowezekana lazima lifanyike ili lisitokee tena. Mikondo huu hujenga madaraja ambayo watoto wengi, wanawake, wanaume, wazee, wanaotoka katika mazingira hatarishi na hatari kubwa, hatimaye wamevuka kwa usalama, uhalali na heshima kwa nchi mwenyeji. Wanavuka mipaka na hata zaidi, kuta za kutojali ambazo matumaini ya watu wengi mara nyingi huvunjika, ambao wanasubiri kwa miaka katika hali zenye uchungu na zisizoweza kudumu.

Papa amekutana na wakimbizi waliofika kupitia mikondo ya kibinadamu
Papa amekutana na wakimbizi waliofika kupitia mikondo ya kibinadamu

Kila mmoja wao anastahili kuzingatiwa katika historia ngumu ambayo wameishi. Hasa, Papa Francisko amependa kuwakumbuka wale ambao wamepitia kambi za kizuizini huko Libya; mara kadhaa alipata fursa ya kusikiliza uzoefu wao wa maumivu, unyonge na vurugu. Mikondo ya misaada ya kibinadamu ni njia mwafaka ya kuepuka majanga na hatari zinazohusiana na biashara haramu ya binadamu. Hata hivyo, juhudi nyingi bado zinahitajika ili kupanua mtindo huu na kufungua njia zaidi za kisheria za uhamiaji. Mahali ambapo nia ya kisiasa inakosekana, mifano bora kama yao hutoa njia mpya za kuchukua hatua. Baada ya yote, uhamiaji salama, utaratibu, mara kwa mara na endelevu ni kwa maslahi ya nchi zote. Ikiwa hii haitasaidiwa kutambua, hatari ni kwamba hofu hufunga siku zijazo na kuhalalisha vikwazo ambavyo maisha ya binadamu yamevunjwa.

Kazi wanayoifanya, ya kutambua na kukaribisha watu walio katika mazingira magumu, inatafuta kujibu kwa njia inayofaa zaidi kwa ishara ya nyakati. Inaonesha njia kwa Ulaya, ili isiweze kukwama, hofu, bila maono ya siku zijazo. Kiukweli, kujifungia au katika utamaduni wa mtu mwenyewe binafasi sio njia ya kurejesha matumaini (Hotuba katika Chuo Kikuu cha Roma Tre,17 Februari 2017). Kwa hiyo, historia ya Ulaya imeendelea kwa karne nyingi kupitia ujumuishaji wa watu na tamaduni tofauti. Kwa hiyo ameomba wasiogope wakati ujao.

Mkutano na wakimbizi kupitia njia salama ya mikondo ya kibinadamu
Mkutano na wakimbizi kupitia njia salama ya mikondo ya kibinadamu

Mikondo ya kibinadamu sio tu inalenga kuleta wakimbizi Italia na nchi nyingine za Ulaya, kuwanyakua kutoka katika hali ya kutokuwa na uhakika, hatari na matarajio yasiyo na mwisho; pia wanafanya kazi kwa ushirikiano, kwa sababu hakuna kukaribishwa bila ushirikiano. Wakati huo huo, wamejifunza katika kazi yao kwamba ushirikiano sio bila matatizo yake. Sio wote wanaofika wamejitayarisha kwa ajili ya safari ndefu inayowangoja. Ndio maana ni muhimu kutekeleza umakini na ubunifu zaidi ili kuwajulisha vyema wale walio na fursa ya kuja Ulaya kuhusu ukweli ambao watakutana nao. Na tusisahau kwamba watu wanahitaji kusindikizwa tangu mwanzo hadi mwisho. Jukumu lao linaisha pale mtu anapounganishwa kikweli katika jamii yetu. Maandiko Matakatifu yanafundisha: “Mgeni akaaye kati yenu mtamtendea kama mtu aliyezaliwa kati yenu” (Mambo ya Walawi 19:34).

Amewasalimia mamia ya watu, familia, jumuiya ambazo zimejitolea kwa ukarimu kutekeleza mchakato huu adhimu. Wamefungua mioyo yao  na nyumba zao. Waliunga mkono ujumuishaji na rasilimali zao na wakahusisha watu wengine. Amewashukuru kwa dhati: wanawakilisha uso mzuri wa Ulaya, ambao hufungua kwa siku zijazo na hulipa kibinafsi. Kwa wale wahamasishaji wa mikondo ya kibinadamu, kwa wanaume na wanawake watawa kwa watu binafsi na mashirika yaliyoshiriki kwao, amependa kusema: “ninyi ni wapatanishi wa historia ya ushirikiano, sio wapatanishi wanaopata kwa kutumia fursa. hitaji na mateso. Nyinyi si wasuluhishi bali wapatanishi, na mnaonyesha kwamba, mkifanya kazi kwa umakini kuweka misingi, inawezekana kukaribisha na kujumuika kwa ufanisi”.

Papa na wakimbizi waliofika kwa njia salama
Papa na wakimbizi waliofika kwa njia salama

Historia hii ya makaribisho ni juhudi ya dhati kwa ajili ya amani. Kuwa uwakilishi kati yao wakimbizi kutoka Ukraine; kwa wao Papa amesema hakosi kamwe kuomba na kutafuta amani, kutamania amani na kusali kwa ajili yake. Anafanya hivyo kwa sababu ya nchi yao iliyopondwa ponda na kwa wengine ambao wamepihwa na vita: kiukweli kina watu wengu waliokimbuwa vita vingine. Na huduma hii kwa maskini, wakimbizi na wahamiaji ni uzoefu wa ngvu sana wa umoja kati ya wakristo. Kwa hakika mpango huu wa mikondo ya kibinadamu ni wa kiekumene. Ni ishara nzuri ambayo inaunganisha kaka na dawa ambayo wanashirikishana imani katika Kristo.

Kwa hiyo amewasalimu kwa upendo wao ambao wamepitia njia za kibinadamu na ambao sasa wanaishi maisha mapya. Wameonesha nia thabiti ya kuishi bila woga na ukosefu wa usalama. Wamepata marafiki na wafuasi ambao ni familia ya pili kwao leo hii. Wamejifunza lugha mpya na kukutana na jamii mpya. Yote haya yamekuwa magumu, lakini yana matunda. Pia amesema hivyo Papa  kutokana na kuwa kama mtoto wa familia ya wahamiaji ambao walifanya mchakato wa uzoefu wa  safari hiyo. Mfano wao mzuri na uchapakazi wao hunasaidia kuondoa hofu na kengele kwa wageni. Kiukweli, kuwapo kwao kunaweza kuwa baraka kwa nchi waliyomo na ambayo sheria na utamaduni wake wanajifunza kuheshimiana na kuheshimu.

Ukarimu ambao umetolewa kwao umekuwa sababu ya wao  kurudi: kwani kiukweli, baadhi yaowamejitolea kuwahudumia wengine wanaohitaji. Kwa hiyo, Papa Francisko amesema kwamba mkutano huo wale wanaokaribisha na wale wanaokaribishwa wako pamoja na karibu kuchanganyika, wanaweza kufurahia neno la Bwana Yesu lisemalo “Nalikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha (Mt 25) :35). Neno hili linatuonesha njia yote. Njia ya kusafiri pamoja, kwa uvumilivu.  Amewashukuru tena kuifungua na kuifuatilia! Amewaomba waendeleze mbele na Bwana awabariki na Mama Yetu, Mama wa safari, awalinde. Yeye pia anawabariki kutoka moyoni mwake.

Papa awahutubia wakimbizi waliofika Ulaya salama
18 March 2023, 16:21