Tafuta

2023.03.30 Nia za maombi ya Sala kwa Mwezi Aprili 2023:Kwa ajili ya utaduni usio na vurugu 2023.03.30 Nia za maombi ya Sala kwa Mwezi Aprili 2023:Kwa ajili ya utaduni usio na vurugu 

Nia za Sala mwezi Aprili 2023:Kwa ajili ya utamaduni wa amani na usio na vurugu!

Katika nia ya Sala ya Papa kwa mwezi Aprili 2023 unajikita kuelezea juu ya utamaduni wa amani na usio na vurugu.Katika ulimwengu wa sasa ambao umegubikwa na kila aina ya ghasia na mbio za silaha kama ambavyo mara kadha Papa amesema,kuna haja ya kuishi na kuzungumza bila jeuri.

Na Angella Rwezaula, -Vatican.

Katika ujumbe kwa njia ya Video wa Papa Francisko kwa lugha ya Kihispania wenye nia ya Sala ya mwezi Aprili 2023,unaoandaliwa na Mtandao wa Kimataifa wa Sala ya Papa ni wito madhubuti ambao unajikita juu ya kutafuta: “amani kwa kila njia ili kuishi ulimwengu ulio bora na usio na vurugu” na kwamba inawezekana! Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu anabainisha kwamba: “Kuishi, kuzungumza na kutenda bila jeuri haimaanishi kukata tamaa, kupoteza au kuacha chochote. Badala yake: “Inamaanisha kutamani kila kitu”.   

Vita haina mantiki yoyote ni kupoteza tu

Kwa kufafanua zaidi anamtaja mtangulizi wake kwamba: “Kama Mtakatifu Yohane XXIII alivyosema miaka 60 iliyopita katika Waraka wake wa Kitume wa ‘Pacem in Terris’, yaani, ‘Amani Ulimwenguni’ kwamba: “vita haina mantiki yoyote zaidi ya kutofikiri. Vita yoyote, ile na mapigano yoyote ya kisilaha, daima huishia kwa wote kushindwa”. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anahimiza kwamba: “Tujenge utamaduni wa amani. Tukumbuke hata katika kujilinda, na amani ndio lengo kuu”.

Baba Mtakatifu Francisko, anaamini kwamba: “amani ya kudumu inawezekana tu ikiwa kuna amani isiyo na silaha”. Kwa hiyo anahimiza zaidi kwamba:  “Hebu tusifanye vurugu katika maisha ya kila siku na katika mahusiano ya kimataifa” na  “huu uwe mwongozo wa matendo yetu”. Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha maombi yake anasema: “Tuombe kwa ajili ya kueneza zaidi utamaduni wa kutotumia mabavu, ambao unahusisha utumiaji mdogo wa silaha, kwa serikali na raia.” 

Mtandao wa Kimataifa wa  Nia za Maombi ya Papa ulianza mnamo 2016

 

Ikumbukwe kwamba Ujumbe wa Papa kwa njia ya Video umetafsiriwa katika lugha 23 na kusambazwa katika nchi 114, na ambao hadi sasa umetazamwa zaidi ya mara milioni 189 kwenye mitandao yote ya kijamii ya Vatican tangu 2016. Mtandao wa Nia ya Maombi  ya Papa Kimataifa ni Kazi ya Kipapa, ambayo dhamira yake ni kuwahamasisha Wakatoliki wote kwa njia ya sala na matendo thabiti katika kukabiliana na changamoto za binadamu na utume wa Kanisa.

Kuna umuhimu wa Kusali kwa ajili ya Amani duniani
Kuna umuhimu wa Kusali kwa ajili ya Amani duniani

Kulingana na utafiti wa  Amnesty International, kila siku zaidi ya watu 500 wanakufa kutokana na silaha na takriban 2,000 hujeruhiwa, huku asilimia 44 ya mauaji yanafanywa kwa kutumia bunduki. Hali hiyo  kulingana na sheria kama ilivyotolewa kwenye  Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni kote inahusishwa moja kwa moja na tasnia ya silaha ambapo  kila mwaka silaha nyepesi milioni 8 na risasi bilioni 15 zinatolewa. Njia pekee inayowezekana ya kukomesha ongezeko hilo, ikichochewa na mizozo inayoendelea huko Ukraine, Asia, Afrika na Mashariki ya Kati,  kwa  kujaribu kuanzia nzai za chini za ndani kwa ndani mahalia.

Padre Fornos S.J, - Vita na mgogoro huanzia na kuona tofauti

Katika kufafanua muktadaha huo, Padre Frédéric Fornos S.J., Mkurugenzi wa Kimataifa wa Mtandao wa Nia za  Sala ya Papa Ulimwenguni amebainisha kwamba  “ Kwa kukabiliwa na vurugu za wakati wetu, Papa Francisko anapendekeza kuomba kwa mwezi mzima kwa ajili ya kuenea zaidi kwa utamaduni wa kutokuwa na vurugu. Amani baina ya watu huanzia katika sehemu halisi na ya ndani kabisa ya moyo: ninapokutana na mtu mwingine barabarani, sura zao, macho yao, hasa yule anayetoka mahali pengine, ambaye haongei kama mimi hana  utamaduni wangu, yule ambaye anaonekana wa ajabu kwangu katika mitazamo yake na kwa sababu hii anaitwa 'mgeni'”.

Kwa hiyo Padre Fornos anasema kwamba “Vita na migogoro huanzia hapa na sasa, katika mioyo yetu, wakati wowote tunaporuhusu vurugu kuchukua nafasi ya haki na msamaha. Injili inatuonesha kwamba maisha ya Yesu yanafunua njia ya kweli ya amani na inatualika kumfuata. Ni katika roho hii tunaitwa kujivua silaha, kwa maana ya kupokonya silaha ya maneno yetu, matendo yetu, chuki zetu”, alisisitiza Padre Fornos. Video hii imetengeneza na kikundi kazi za video za Papa za Mtandao wa Sala kwa msaada wa Shirika La Machi  Kwa ushirikiano na Vatican Media. Kwa maelezo zaidi unaweza kutazama: www.ilvideodelpapa.org.

Nia za Sala ya Papa kwa Mwezi Aprili 2023
30 March 2023, 16:16