Kanisa linalorudisha huruma iliyopokelewa
Na Andrea Tornielli
Kanisa linalotoka na “kuchukua hatua” kwa sababu lilikuwa la kwanza kupata mpango wa Bwana na “lilitanguliwa kwa upendo”. Miaka kumi baada ya uchaguzi wa Jorge Mario Bergoglio mnamo Machi 13, 2013, inafaa kurudi kwenye mambo muhimu. Yafaa tukumbuke kile ambacho Fransisko mwenyewe anaendelea kupendekeza na kushuhudia: uso wa Kanisa ambalo tunasoma katika Waraka wa Evangelii gaudium “linajua jinsi ya kuchukua hatua ya kwanza, linajua jinsi ya kuchukua hatua bila woga, kuelekea; kutafuta walio mbali na kufika njia panda kuwaalika waliotengwa. Anaishi hamu isiyokwisha ya kutoa huruma, tunda la kupata huruma isiyo na kikomo ya Baba na uwezo wake wa kugawanya”.
Anachopendekeza Francisko ni uso wa jumuiya za Kikristo zilizo huru kutokana na janga la kujirejea binafsi, wakifahamu kuwa ni wamisionari wa kweli pale tu wanapoakisi mwanga wa Bwana wao bila kujiona kuwa chanzo cha nuru. Jumuiya ambazo hazitumii mbinu za uuzaji na kugeuza watu imani na ziko huru kutokana na tamaa mbaya ya wale wanaotamani “Ukristo” ambao haupo tena. Jumuiya ya “wenye dhambi waliosamehewa” - kukumbuka ufafanuzi ambao Askofu wa Roma anajitolea yeye mwenyewe na ambaye, akiendelea kupata huruma ya Mungu isiyo na kikomo, anairudisha kwa wengine. Ni neno la “huruma” ambalo linatoa muhtasari bora wa mafundisho ya Papa wa Argentina anapoingia katika muongo wa tatu wa upapa wake. Huruma ni kama ujumbe muhimu wa Yesu katika Injili, kama ufahamu wa kupendwa na kuinuliwa kila mara baada ya kila anguko. Huduma ni kama ufunguo wa dhamira ya mabadiliko ya enzi yetu.
“Jumuiya ya wainjilishaji, tunasoma tena katika Evangelii gaudium, “inajiweka yenyewe kwa njia ya matendo na ishara katika maisha ya kila siku ya wengine, kufupisha umbali, kujishusha hadi kiwango cha kudhalilishwa ikiwa ni lazima, na kuchukua maisha ya mwanadamu, kugusa mwili wa Kristo unaoteseka katika watu”. Ni jumuiya iliyo tayari kukaribisha, kusikiliza, kusindikiza yaani, “kujihusisha”, kama Yesu alivyofanya na wanafunzi wake, akipiga magoti, akiwaosha miguu. Jumuiya ya subira, ambayo haihitaji maadui kupata uthabiti wake, lakini “hutunza nafaka” bila kupoteza amani kwa sababu ya magugu”.
Fransisko alishuhudia ujumbe huu katika miaka kumi ya kwanza ya utumishi wake, akijumuisha maneno ambayo yeye mwenyewe alitamka akiwa bado kardinali, katika hotuba yake fupi katika baraza la Makardinali kabla ya mkutano mkuu wa uchaguzi alisema: “Tukimfikiria Papa ajaye, kuna haja ya mtu ambaye, kutokana na kutafakari na kumwabudu Yesu Kristo, alisaidie Kanisa kujitoa lenyewe kuelekea pembezoni mwa mwanadamu, ili liwe mama mwenye kuzaa matunda kwa furaha tamu na ya kufariji ya uinjilishaji”.