Miaka 10 ya Upapa,Bartholomeo I:Ushirikiano umedumu wa kupeleka faraja na amani
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Patriaki Bartholomeo I wa Kiekumene wa Costantinopoli katika fursa ya kumtakia matashi mema kwa ajili ya miaka kumi ya Upapa wa Baba Mtakatifu Francisko, inayoadhimishwa tarehe 13 Machi ameandika kwamba: “Ni heshima kwangu mimi na furaha ya kina kumpongeza mpendwa kaka yangu Papa Francisko; katika fursa ya miaka 10 tangu kuchaguliwa kwake, kama Askofu wa Kanisa dada la Roma. Katika miaka kumi hii, urafiki wetu na ushirikiano, hasa katika huduma ya kupeleka faraja na amani kwa watu wote wa Mungu na katika hatua ya kuhamasisha utunzaji na uponesha wa kazi ya uumbaji wote wa Mungu, vimetufanya kukaribiana katika kuamini kwetu pamoja na jitihada ya kuona uso na kukaribishwa uwepo wa Bwana wetu Yesu Kristo katika walio wa mwisho kaka na dada wanaoteseka”.
Patriaki Bartholomeo I akiendelea ameandika kuwa: “Mpendwa kaka Francisko, tunakupongeza kipaumbele chako cha uongozi, tunakushangilia kwa hekima ya matendo yako na kushangaza kwa maendeleo ya kutumwa kwako. Kibinafsi, ninatarajia kushiriki hatua zako zinazofuata zilizo barikiwa, wakati tunakaribia kufanya kumbukumbu ya kihistoria na kuadhimisha Mtaguso wa Kwanza maalum wa Nikea, mahali ambapo tunaweza kuweka misingi muhimu ya Imani yetu Kikristo. Ad multos annos, mio caro amico! Chrónia pollá!”