Miaka 10 ya Upapa,Di Segni:Umedumisha uhusiano mwema hata kwa Wayahudi
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Matashi mema kwa ajili ya Baba Mtakatifu anayefikisha miaka 10 tangu kuchaguliwa kwake mnamo tarehe 13 Machi 2013, yanaendelea kutolewa hata kutoka kwa Riccardo Di Segni, Mkuu wa Jumuiya ya Wayahudi Roma, ambaye ameandika kuwa: “Imefika miaka kumi ya Upapa wa Papa Francisko. Namba 10 ni muhimu, ishara, msingi wa mfumo wa kuhesabu; ni vidole kumi vya mikono, lakini pia kwa msomi wa Biblia “10” inakumbusha Amri Kumi, inakumbusha hata maneno kumi msingi ambayo yaliumba ulimwengu na kwa mujibu wa maneno ya Musa yalikuwa ni maasi ya watu wa Israeli wakati wa kukaa kwao jangwani. Kwa hiyo “10” inakumbusha, kwa maana ya kibiblia, tabia na hata shauku, wakati mwingine kudhoofisha misingi hii.
Kwa hiyo mkuu wa kiyahudi Roma anabainisha kwamba: “Matashi yangu kwa Papa Francisko ni kwamba aendelea kuwa na afya, nguvu nyingi na hasa kuwa na hekima na kuendelea kuongoza jumuiya yake kwa nguvu na hekima ambayo amekuwa nayo hadi sasa. Na hata ameweza kudumisha uhusiano maalum kwa urafiki ambao alitaka kuukuza kwa watu wa kiyahudi.”