Kwa mara nyingine Papa ametuma msaada kwa watu wa Ukraine
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya katekesi yake tarehe 29 Machi kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro ya “Tudumu katika sala na ukaribu na Ukraine iliyouawa” ni kielelezo cha umakini wa mara kwa mara kwa nchi hiyo ambayo sasa imekuwa katika vita kwa zaidi ya mwaka mmoja. Tahadhari ambayo mara nyingi imetafsiriwa katika wito wa amani na misaada thabiti. Msaada wa mwisho uliwasili Kharkiv, Asubuhi Jumatano 29 Machi 2023 kwa Lori lililokuwa limepakia jenereta, vyakula, madawa na ambalo lilikuwa limeondoka Jumamosi tarehe 25 Machi 2023 kutoka Kanisa la Mtakatifu Sofia jijini Roma, mahali ambapo hukutana jumuiya ya Kiukreni nchini Italia.
Ukaribu wa Papa kwa nchi inayoteseka
Tangu kuanza kwa vita, Kanisa limechukua jukumu la kutafuta mahitaji ya wale ambao familia zao ziko mbali, na kuwa na wasiwasi wa wengi, kuungana zaidi katika kukabiliana na janga la migogoro. Kwa niaba ya Papa kupitia Baraza la Kipapa la Huduma ya upendo, ilitayarisha mzigo huo. Kwa hiyo Mwenyekiti wa Baraza hilo la Kipapa Kardinali Konrad Krajewski, alipenda kuwashukuru madereva wote ambao kwa ujasiri, wakipinga shida, walifanikiwa kuingia nchini Ukraine, na hivyo kufikisha mzigo huo. Dhamira ya kutekelezwa kwa busara na umakini kwa sababu, alisema Kardinali Krajewski, kuwa vita havijaisha, na hivyo mambo yanaendelea mabomu na kupigana. Na ni baada tu ya msafara huo kufika ndipo aliweza kueleza jambo hilo. Lazima waendelee kujitolea na kuiombea nchi ya Ukraine inayoteswa.