Tafuta

Ulikuwa mkutano kati ya Marcelo Figueroa  na Papa Roma Ulikuwa mkutano kati ya Marcelo Figueroa na Papa Roma 

Miaka 10 ya Papa,Figueroa:Ni Papa wa Uekumene na kipaumbele katika ziara za kitume

Figueroa,Mwanabiblia na mwandishi anamfafanua Papa kwa miaka 10 ya upapa wake kwa mtazamo wa Uekumene katika msingi ya kibinadamu na sayari.Uekumene wa upendo,huruma,amani,mshikamano,mwili na wa damu.Katika ziara 40 za kitume kwa nchi sitini,alionesha uekumene katika ratiba zake.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Katika kumbu kumbu ya miaka 10 ya Upapa wa Papa Francisko ambao tanatimiza tarehe 13 Machi,  Bwana Marcelo Figueroa, Mtaalam wa Biblia na Mwandishi ameandika juu yake kwa mtazamo wa Uekumene kwamba, Uekumene bila shaka ni moja ya nguzo msingi au njia ya kushawishi maana zaidi ya upapa wa Papa Francisko. Figueroa amesema kwamba hapo na maana ya uekumene kwa upande mmoja (katika  lugha ya kigiriki Oikoumene, nchi inayoishi watu), ili kuhitimisha kile ambacho wanajua kama majadiliano ya mchanganyiko wa dini na kidini. Hata hivyo kwa upande wa Papa Bergogli, lazima kupanua mtazamo huo. Kwa kutafakari juu ya Mtazamo na mchango wake wa kiekumene ni muhimu ni kujumuisha sura katika kuelekea mwingiliano wa tamaduni na ulimwengu, muunganisho wa ulimwengu ulioundwa, uhusiano wa mifumo ya ikolojia na tamaduni za pembeni na maarufu. Wazo hilo la mwisho ni la msingi kwetu kufunika katika nuru ya  mawazo ya Bergoglio juu ya uongofu fungamani wa kiekumene.

Ili kuweza kupata jibu lazima kufikiria watu maskini na wale ambao wanaishi katika mahali asili,  kwenye kiungo cha uumbaji na asili cha mtazamo wa haliye juu na kidini kama mtazamo wake kuhusu hali ya kiekumene. Hayo yote yanaweza kueleweka kwa wazi kwa kutumia lenzi kuu juu ya kiini cha Kristo ambacho ni cha Papa Francisko. Kiini hicho kinajifafanua katika utajiri wa kutunza maono yake ya Yesu kama hakikisho la siri zote katika hekima na fahamu (Wakolosai 2,3) kuunga mkono utambulisho wake wa Kikristo bila misingi katika uimara wa umwilisho unaoponya majeraha ya wanadamu wote (rej. Yn 1:14) na kuimarisha ukatoliki wake kwa mtazamo wa upatanisho wa mazungumzo.

Bwana Figueroa ameandika kwamba ni idadi kubwa ya mwelekeo wa kiekumene ambao Papa Francisko ameuendeleza tangu amekuwa Askofu wa Roma. Kwa hiyo aliufafanua uekumene katika msingi wa hali ambayo ni kibinadamu na sayari. Amezungumzia uekumene wa upendo, wa huruma, wa amani, wa mshikamano, wa mwili na wa damu. Katika ziara zake 40 za kitume ambazo alitembelea nchi sitini, daima alionesha uekuemene kama nafasi msingi katika ratiba yake.  Ziara zake za kitume hazikuwa chache za kiekumene, kama ile ya mwisho aliyotimiza nchini Sudan Kusini. Hata Sinodi ya Amazonia ilikuwa ni Sinodi ya kiekumene, katika mawazo na mwenendo wake, na  hati za ushuhuda. Zaidi Papa Francisko alikutana na viongozi wengi wa kidini wa kiorothodox, wayahudi, waislamu, waprotestanti na aina nyingina za dini za jadi ulimwenguni.

Na katika masuala ya Vatican, Nyaraka mbili zinajiunga katika wazo na urithi ambao bado ni ujenzi wa Papa Francisko kama vile Laudato Si inayoanza kwa kurejea mchango wa Patriaki Bartholomeo I na Fratelli tutti ambao, unakumbusha unakumbusha mikutano na hati ya pamoja na Imam Ahmad Al-Tayyeb.  Kwa hiyo vyanzo hivi viwili visivyoisha vya masomo, tafakari, uchambuzi na utendaji kimsingi ni vya kiekumene. Bwana Figuero  bado ameeleza  hata juu utambuzi na maumivu ya Papa Francisko ambaye amekuwa kama sauti ya kinabii ambaye alitaja mapema kabisa juu ya vita vya dunia vilivyomegeka vipande vipande katika ulimwengu. Ni miito mingi sana, ikiwemo ujumbe, mahubiri, tamasha, hotuba, mikutano ya kiekumene ya maombi kwa ajili ya amani, lakini pia ni pamoja na matendo yake madhubuti ya ukaribu mbele ya janga la maumivu ya watu wanaoteseka. Ya radi na ushujaa ni shutuma zake za nguvu za kivita za silaha. Aidha juhudi zake za kutekeleza uekumene kama diplomasia ya kuleta amani hazikuchoka. Kwa hiyo ili kujua nguvu yake katika suala ya uekunene na ishara zake, lugha za ukimya wake, maneno yake ya kina na maana ya mungu katika matendo yake ya dhati yatakuwa ni muhimu sana kuyaelewa maono na utume wa Papa Francisko.

12 March 2023, 19:07