Kard.Parolin:Elimu ni nguvu ya amani,lazima ihakikishwe kwa wasichana
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Elimu sio tu sehemu muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kibinafsi, lakini pia njia bora na yenye nguvu zaidi ya kukuza kuishi pamoja kwa amani kati ya watu na mataifa". Hili lilisisitizwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, katika ujumbe wa video uliotumwa katika meza mduata iliyopewa kichua “Kuthubutu kwa amani. Njia za elimu, iliyohamasishwa katika mkesha wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, tarehe 7 Machi 2023 na Kitivo cha Kipapa cha Sayansi ya Elimu ‘Auxilium’, kwa kushirikiana na mabalozi nane wanawake walioidhinishwa na Vatican kutoka mabara matano. Katika ujumbe unaofungua meza ya mduara sanjari na Siku ya 36 ya Kitivo cha ‘Auxilium’ cha Shirika la Mabinti wa Maria wa Msaada wa Wakristo, Kardinali Parolin, kwa lugha ya Kiingereza, alisisitiza kuwa elimu huwapatia wasichana na wavulana zana pekee, kuelewa ukweli wa leo hii, lakini pia kujenga ukweli wa kesho pamoja.
Lakini pia anasisitiza juu ya janga la kielimu la sasa ambalo huamua upatikanaji wa elimu amba bado haupo katika sehemu nying. Pia kama matokeo ya maamuzi ya kiitikadi, alishutumu kwamba watoto wengi hawajapata elimu wanayostahili, na mara nyingi wasichana ndio wanaolipa gharama kubwa zaidi. Hii inasababisha madhara makubwa kwa jamii nzima na kwa hiyo, kwa upande wake lengo la upatikanaji sawa wa elimu kwa wote bado linahitaji juhudi kubwa na dhamira kubwa ya kisiasa". Hatimaye, Kardinali Parolin alikumbuka maneno ya Baba Mtakatifu Francisko kuhusu umuhimu wa nafasi ya mwanamke, ya kuhifadhi na kuendeleza amani katika jamii na kati ya mataifa, hasa katika michakato ya amani, kuzuia migogoro na diplomasia”. Kwa sababu hiyo hupatikanaji wa elimu kwa wanawake na wasichana ni wa umuhimu mkubwa na unapaswa kuhakikishwa.
Mkutano huo katika ukumbi wa Yohane Paulo II wa Kitivo Auxilium unakusudia kuwa, fursa ya kutafakari na majadiliano juu ya thamani ya elimu kama nyenzo muhimu kwa mabadiliko chanya katika jamii na utatuzi wa migogoro; juu ya ulinzi wa waliotengwa na ushiriki wa walio wachache, kuanzia mitazamo tofauti ya kimataifa. Kwa kusisitiza zaidi Mkuu huyo Piera Ruffinatto, alinukuu mwanamke mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel, ambaye ni mwanaharakati wa Pakistani Malala Yousafzai mnamo mwaka wa 2014, akiwa na umri wa miaka 17 tu, ambaye alisema: “Hebu tuchukue vitabu vyetu na kalamu zetu. Ni silaha zetu zenye nguvu zaidi. Mtoto mmoja, mwalimu mmoja, kitabu kimoja na kalamu moja vinaweza kubadilisha ulimwengu.”
Aliyekuwa akiongoza meza hiyo Alessandra Morelli, mwakilishi wa zamani wa UNHCR na mtaalamu wa sera za kibinadamu, alifungua meza hiyo ya mduara kwa ushuhuda wa Chiara Porro, balozi wa Australia, ambaye, kama wenzake, sio tu anabainisha janga na masuala muhimu katika mazingira ya nchi yake lakini piarasilimali za kibinafsi na za kitaasisi zenye uwezo wa kutengeneza fursa na michakato ya kielimu inayopendelea ukuaji wa watu ambao ni wapenda amani. Akizungumzia elimu-jumuishi kama njia ya upatanisho na jamii za kiasili, Balozi Porro anataja programu ya kujifunza kwa masafa ‘School of the Air’, ambayo kwa zaidi ya miaka 70 imeruhusu wavulana na wasichana kufikia na kusoma maeneo ya mbali zaidi ya Australia. ‘Outland’, inayoishi zaidi ya kilomita elfu moja kutoka shuleni. Anakumbuka sura ya mtakatifu wa kwanza na wa pekee wa Australia, Mary MacKillop, ambaye alianzisha Masista wa Mtakatifu Joseph wa Moyo Mtakatifu, ambao waliendesha shule katika maeneo ya vijijini ya Australia, akizingatia hasa mahitaji ya jamii za kiasili. Katika misheni katika Wilaya ya Kaskazini, ambako uhusiano na wamisionari Wakatoliki ungali hai sana, balozi huyo anakutana na Miriam Rose Ungunmerr Baumann, mwalimu wa kwanza wa asili aliyeidhinishwa katika eneo hilo kubwa, ambaye alifunzwa katika shule ya Wamishonari wa Patakatifu. Moyo.
Mabalozi wengine saba walioithinishwa na Vatican waliongilia kati mjadala ni baada ya Chiara Porro ni Juvita Rodrigues Barreto De Ataíde Gonçalves, wa Timor est, Alexandra Valkenburg-Roelofs, ambasciatrice wa Umoja wa Ulaya , Angelina Baiden-Amissah, wa Ghana, María Isabel Celaá Diéguez, wa Hispania Teresa Susana Subieta Serrano, wa Bolivia, Florence Mangin, Ufaransa na Majlinda Dodaj, wa mambo ya nje wa Albania.