Huzuni ya Papa juu ya ajali ya treni nchini Ugiriki
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amehuzunishwa na tendo la ajali iliyofanya kupoteza maisha na majeraha yaliyosababishwa na treni zilizogongana huko Larissa, Ugiriki. Katika barua iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Jumatano tarehe Mosi Machi 2023, Baba Mtakatifu anawahakikishia maombi yake kwa wale wote waliofikiwa na mkasa huo na kwa familia za wahanga, akizikabidhi roho za marehemu kwa huruma ya Mungu Mwenyezi. Baba Mtakatifu Francisko aidha amewabariki waokoaji na wale wanaosaidia, akiwashukuru kwa kujitolea na mshikamano wao.
Ajali hiyo
Mgongano kati ya treni ya mizigo na treni ya abiria ulifanyika Jumanne jioni tarehe 28 Februari 2023 kati ya Athene na Thessalonike, karibu na jiji la Larissa. Idadi ya waliofariki ni takriban 32 na 85 kujeruhiwa. Kulingana na ujenzi upya wa tukio hilo, mabehewa matatu yaliacha njia dakika chache kabla ya saa sita usiku katikati mwa nchi, kufuatia mgongano kati ya treni ya mizigo na msafara wa abiria 350. Kupitia vyombo vya habari vya Ugiriki, vimebainisha kuwa hii ndiyo ajali mbaya zaidi ya treni ambayo Ugiriki haijawahi kutokea. Wazima moto na magari ya kubebea wagonjwa walihudhuria eneo la tukio. Cranes pia zilitumika kujaribu kuondoa uchafu na kuinua mabehewa yaliyopinduka, kwa ukombozi wa watu walionaswa unaendelea na inafanyika katika mazingira magumu.
Watu wengi wamejeruhiwa vibaya sana hata na moto
Hakika moja ya mabehewa hayo yalishika moto na watu kadhaa walikwama ndani. Maafisa wa hospitali ya jiji la Larissa walisema takriban watu 60 walijeruhiwa, wengi wao vibaya. Mkuu wa mkoa alizungumza juu ya mgongano wa nguvu sana. “Treni ilikuwa imechelewa na ilikuwa imesimama kwa dakika chache tuliposikia kelele kubwa ya kushangaza, na baadhi ya abiria waliokuwa kwenye treni hiyo walishuhudia.