Tafuta

Barua ya Papa kwa Lino Banfi kufuati na kifo cha mke wake Lucia iliyosomwa wakati wa maziko. Barua ya Papa kwa Lino Banfi kufuati na kifo cha mke wake Lucia iliyosomwa wakati wa maziko.   (ANSA)

Upendo wa Papa kwa Lino Banfi:'wewe ni babu wa Taifa zima'

Baba Mtakatifu ameelekeza salamu za rambi rambi kwa Lino Banfi,msanii maarufu wa kiitaliano kufuatia na kifo cha mke wake Lucia iliyosomwa wakati wa mazishi yake.“Mababu wanajua kuwa na nguvu hata wakati wa mateso na wewe ni Babu wa Taifa zima,endelea kushuhudia upendo ambao uliwaunganisha."

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Ni zaidi ya miaka 60 ya maisha ya ndoa kati ya Lucia na Lino. Hadi kufikia kutamani kwamba hata kifo kingeweza kuwa njia ya kufanya pamoja wakiwa wamekumbatiana, kama ambavyo mara nyingi na katika fursa nyingi hayo yametokea. Ilikuwa ndiyo shauku ya Bi Lucia Zagaria, Mke wa Bwana Lino Banfi, aliyezimika roho Jumatano tarehe 23 Februari 2023 usiku akiwa na umri wa miaka 85 katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Madawa jijini Roma mahali alipokuwa anatibiwa kwa kipindi.

'Abuelo d'italia'

Hata hivyo Msanii wa kitaaliano  alikuwa amemsimulia Papa Francisko juu ya wazo la mke wake Lucia wakati wa kukutana naye mjini Vatican mnamo tarehe 2 Machi 2022, katika siku yao ya kumbu kumbu ya kutimiza miaka 60 ya ndoa. Katika mkutano huo, kwa mujibu wa Bwana Banfi wakati wa mahojiano mara baada ya kukutana na Papa alikuwa amedhirisha wazi jinsi ambavyo waliweza kufanya uzoefu mzuri na hisia za kirafiki, ambapo Baba Mtakatifu alikuwa amemfafanua Bwana Lino Banfi kama “abuelo d’Italia”,  yaani  “Babu wa Italia", kufuatia  na nafasi ya jina la filamu moja ambayo likuwa anaitwa 'Babu Libero' iliyodumu kwa miaka mingi na kwa mafanikio na umaarufu mkubwa katika “Historia ya Daktari katika familia”. Kwa maana hiyo masizishi yalifanyika katika Parokia ya Mtakatifu Ippolito kwa kuongozwa na Kardinali Francesco Coccopalmerio.

'Chukua urithi wa imani na wema wa mke wako Lucia'

Kutokana na  urafiki uliochanganyikana na hisia ya huzuni, inaonekana katika maneno ambayo Baba Mtakatifu Francisko alimwandikia kumpa pole Bwana Lino Banfi ambayo ilisomwa wakati wa mazishi kwamba: “Ndugu mpendwa, baada ya kupata habari za kifo cha Lucia, ninakupa wewe na familia yako salamu zangu za rambirambi, nikikuhakikishia maombi kwa ajili ya roho yake. Imani katika Kristo, Tumaini letu, ikuunge mkono wakati huu wa uchungu. Bibi na babu wanajua kuwa na nguvu hata katika mateso na wewe ni babu wa taifa zima”. Kwa hiyo Baba Mtakatifu akieleza Bwana Banfi kwa upendo ameongeza: “Chukua urithi wa imani na wema wa mke wako Lucia kwa kuendelea kutoa ushuhuda wa uzuri wa kifungo cha upendo ambacho kimewafungamanisha pamoja, uzuri usio na kifani wa familia. Ninakuonesha upendo wangu na, nikiomba ulinzi wa Bikira Mtakatifu, ninakubariki wewe na wote wanaoomboleza kifo cha Lucia. Kindugu Francisko”,, salamu zake Papa za Rambi rambi zinahitimishwa.

'Kwaheri Mama, sasa huko namna hiyo'

Aliyetoa taarifa ya kifo Bi Lucia Zagaria alikuwa ni mwanae Rosanna kupitia ukurasa wa Instagram aliandika kwamba: “Kwa heri Mama sasa huko namna hiyo. Safari njema”. Bi Lucia alikuwa ameuguwa kwa muda alioana miaka 60 iliyopita na msanii Banfi maarufu "Nonno Libero", ambao walifanikiwa kuwa na watoto wawili Rosanna, ambaye pia ni msanii na kaka yake, Walter, mkurugenzi na mtayarishaji wa filamu.

 

25 February 2023, 10:32