Tafuta

Papa ametumia ishara ya Kung'ara kwa Yesu  Mlimani katika Ujumbe wa Kwaresima 2023. Papa ametumia ishara ya Kung'ara kwa Yesu Mlimani katika Ujumbe wa Kwaresima 2023.  (© Musei Vaticani)

Ujumbe wa Papa wa Kwaresima 2023:Mchakato wa Kwaresima ni sawa&wa Kisinodi

Kipindi hiki cha Kiliturujia,Bwana anakwenda nasi na kutupeleka kandoni.Katika Kwaresima tunaalikwa kupanda juu mlimani pamoja na Yesu ili kuishi na Watu watakatifu wa Mungu.Mchakato wa safari ya kufunga na kujinyima wa Kwaresima ni sawa sana na ule wa Kisinodi,vyote viwili vina hatima moja ya kung’ara,binafsi na Kikanisa.Ni katika Ujumbe wa Papa wa Kwaresima 2023.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Injili ya Matayo, Marko na Luka zinakubaliana katika kusimulia tukio la Kung’ara kwa Yesu (kugeuka sura). Katika tukio hilo tunaona jibu la Bwana la kutoeleweka kwa  mitume wake waliokuwa wameonesha mbele yake. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko anaanza ujumbe wake wa Kwaresima kwa mwaka 2023, uliochapishwa tarehe 17 Februari, ukiongozwa na kauli mbiu: “Kujinyima kwa ajili ya Kwaresima, mchakato wa kisinodi”. Akiendelea Baba Mtakatifu anasema, mapema kabla ukweli kulikuwa na mabishano ya kweli kati ya Mwalimu na Simoni Petro, ambaye mara baada ya kukiri imani yake kwa Yesu, kama Kristo, Mwana wa Mungu, alikuwa amekataa tangazo lake la mateso na msalaba. Na Yesu alikuwa amemkaripia kwa nguvu akisema: “Nenda  nyuma yangu, shetani! Ukikwazo kwangu; kwa sababu huyawazi yaliyo ya  Mungu bali ya  wanadamu”(Mt 16,23) Na ndiyo tazama kwamba siku sita baadaye Yesu alikwenda juu mlimani ( Mt 17,1).

Injili ya kung'ara kwa Yesu inatangawa kila Dominika ya II ya Kwaresima

Injili ya Kung’ara  (au kugeuka sura), inatangazwa kila mwaka katika Dominika ya Pili ya Kwaresima. Kwa hakika katika kipindi hiki cha Kiliturujia, Bwana anakwenda nasi na kutupeleka kandoni. Hata ikiwa shughuli zetu za kawaida zinatuhitaji kubaki katika mahali pale pale daima, kwa kuishi kila siku mara nyingi na marudio ambayo wakati mwingine yanakera, katika kipindi cha Kwaresima tunaalikwa kupanda juu mlimani pamoja na Yesu  ili kuishi na Watu watakatifu wa Mungu, sehemu ya uzoefu wa kusali kwa kina kujinyima. Kufunga wakati wa Kwaresima, unaongozwa daima na Neema, ili kushinda madhaifu yetu ya imani, na uvumilivu wa kufuasa Yesu katika safari ya msalaba.

Ili kumwelewa Yesu lazima uache usukumwe kandoni na juu

Ni kama vile kile alichokuwa anahitaji Petro na mitume wengine, Papa anakazia kusema. Ili kujikita kwa kina katika ufahamu wa Mwalimu, kwa kumuelewa na kukaribisha hadi mwisho fumbo la wokovu wa Mungu, lililofanyika katika zawadi ya Kanisa lake kwa ajili ya upendo,ni lazima kuacha usukumwe na Yeye kandoni na juu, kwa kuacha uwastani na ubatili. Lazima kujiweka katika mwendo, safari yenye mpando, ambao unahitaji nguvu, sadaka na kijunda kama ile ya kupanda mlimani.  Mahitaji haya ni muhimu hata kwa ajili ya mchakato wa kisinodi, ambao kama Kanisa tumo tunaendelea na juhudi ya kutimiza. Itakuwa vizuri kutafakari juu ya uhusiano ambao upo katika kufunga  kipindi cha  kwaresima na uzoefu wa kisinodi.

Yesu alichagua mitume watatu kwenda Tabor 

Katika mafungo juu ya Mlima Tabor, Yesu alikwenda pamoja na mitume watatu, aliowachagua kuwa mashuhuda wa tukio moja la kipekee. Alitaka uzoefu ule wa neema usiwe pekee yake, lakini wa kushirikisha, kama alivyo yeye, na mengineyo, katika maisha yetu ya imani. Yesu anafuatwa kwa pamoja. Ni pamoja kama Kanisa la hija katika wakati, ni kuishi katika mwaka wa kiliturujia na ndani mwake, kwa hiyo Kwaresima katika kutembea na wale ambao Bwana ametuwekea karibu kama wasindikizaji wa safari. Sawa sawa na hiyo, kufunga kwa Yesu na kwa mitume katika Mlima wa Tabor, tunaweza kusema kuwa safari yetu ya Kwaresima ni ya kisinodi, kwa sababu tunatimiza pamoja katika njia sawa, mitume na mwalimu mmoja. Hata hivyo tunajua kuwa Yeye mwenyewe ni Njia na hivyo mchakato wa kiliturujia na ule  Sinodi, Kanisa halifanyi cha zaidi ya kuingia ndani kwa kina na ukamilifu wa kweli katika huduma ya Kristo Mwokozi.

Neema ya kuona utukufu  na ukuu usio wa kawaida

Baba Mtakatifu kwa hiyo katika ujumbe huu wa kwaresima  amesema, tunafikia wakati wa mwisho. Injili ambayo Yesu aling’aa mbele yao, uso wake uling’ara kama jua na mavazi yake yakamelemeta kama mwanga (Mt 17,2). Na ndiyo Juu, iliyo hatima ya safari. Mwisho wa mpando wakati wao wako juu ya mlima na Yesu, mitume watatu walipewa neema ya kuuona utukufu wake, mwanga mkuu, usio wa kawaida, ambao haukutoka nje, lakini uliangaza kutoka kwake mwenyewe. Uzuri wa Mungu katika maono hayo yalikuwa makuu yasiyolinganishwa na ugumu wowote ambao mitume wangeweza kuwa wamefanya katika kupanda huko Tabor. Kwa hiyo Papa amebainisha kuwa  kama ilivyo kila jitihada ya kupanda mlima, kiukweli, lazima kuwa na mtazamo mzuri wa njia: lakini mandhari ambayo inafunguliwa mwishoni inashangaza na kulipa mshangao wake. Hata katika mchakato wa sinodi, inaonesha mara nyingi ugumu na wakati mwingine tunaweza kukata tamaa. Lakini kile kinachotusubiri bila shaka ni jambo la kushangaza na la ajabu, ambalo linatusaidia kuelewa vema mapenzi ya Mungu na utume wetu katika huduma ya Ufalme wake. Uzoefu wa mitume juu ya Mlima Tabor ulitajirishwa sana wakati karibu na Yesu aliyeng’ara kulitokea sura ya Musa na Helia, ambao wote wawili wanafafanulia kama Sheria na Manabii (Mt 17,3).

Mchakato wa kufunga wakati wa Kwaresima ni sawa sawa na Sinodi 

Upya wa Kristo ni utimilifu wa mapatano ya kale na ahadi na sheria ya Mungu haiwezi kutengenishwa na watu wake na ambayo inaoneshwa wazi maana ya kina. Sawa wasa na hiyo mchakato wa sinodi umesimikwa mzizi katika tamaduni ya Kanisa na wakati huo huo ufunguzi kuelekea mapya. Utamaduni ni kisima cha kujifunza ili kutafuta njia moja kwa kuzuia mapngamizi ya vishawishi vya vya ghafla. Mchakato wa safari ya kufunga na kujinyima ya Kwaresima ni sawa sana na ile ya Kisinodi, vyote viwili vina hatima moja ya kung’ara , binafsi na kikanisa. Mabadiliko ambayo yote pamoja katika muktadha huo  unapata mtindo mmoja katika ule wa Yesu na unafanya kazi kwa neema ya huduma ya Pasaka. Ili mabadiliko hayo yawepo inawezekana kutimiza katika sisi mwaka huu, ambapo Papa amependekeza njia mbili za kufuata ili kupanda pamoja kwa Yesu na kufika kwake yeye katika hatima.

Yesu anazungumza nasi, na je sisi tuzungumzeje naye?

Ya kwanza inahusu sharti ambalo Mungu Baba anawambia mitume juu ya mlima Tabor, wakati walikuwa wanatafakari Kung’ara kwa Yesu. Sauti kutoka kwenye mawingu ilisema “ Msikilize” (Mt 17,5). Kwanza kabisa maelekezo yako wazi: Kusikiliza Yesu. Kwaresima ni kipindi cha neema katika kipindi ambacho tunajiweka katika usikivu wake na Yeye anazungumza nasi. Na jinsi gani anazungumza?  Kwanza kabisa katika Neno la Mungu, ambalo Kanisa linatupatia kupitia Liturujia: tusiache lianguke katika utupu; ikiwa hatuwezi kushiriki daima katika Misa, basi tusome Masomo ya kibiblia kila siku hata kwa msaada wa Inteneti, Papa ameshauri. Zaidi katika maandiko, Bwana anazungumza nasi katika ndugu, hasa katika nyuso na katika historia za wale ambao wanahitaji msaada. Baba Mtakatifu amependa kuongeza hata mantiki nyingine, ambayo ni muhimu katika mchakato wa sinodi: Kusikiliza  Yesu kunapitia hasa kwa njia ya kaka na dada wa Kanisa  usikivu ule wa pamoja ambao kwa baadhi ya awamu ni lengo msingi lakini ambao kiukweli unabaki daima muhimu katika njia na mtindo wa Kanisa la Kisinodi.

Usijifiche nyuma ya udini unaofanywa na matukio

Kwa kusikia sauti ya Baba, mitume walianguka kifudifudi na kuwa na hofu kubwa. Lakini Yesu aliwakaribia, akawagusa na kusema: “Hamkeni na msiogope. Kwa kuinua  macho yao hawakuona yeyote zaidi ya Yesu peke yake (Mt 17, 6-8). Hapo ndipo elekezo la pili la Kwaresima hii, kwamba: usijifiche nyuma ya udini uliofanywa kwa matukio maalum, wa uzoefu wa kupendekeza, wa hofu ya kukabiliana na hali halisi ngumu kila siku, ugumu wake na mapingamizi. Mwanga ambao Yesu anaonesha kwa mitume wake ni utangulizi wa utukufu wa pasaka, na kueleka hitaji lile la kwenda kufuata Yeye peke yake. Kwaresima inaelekeza Pasaka, kwa hiyo mafungo sio lengo peke yake, lakini inatuandaa kuishi kwa imani, tumaini na upendo mateso na msalaba ili kufikia utukufu.

Mchakato wa Sinodi usikukatishe tamaa

Hata mchakato wa Sinodi, usitukatishe tamaa ya kuwa tumefika wakati Mungu anatupatia neema kwa baadhi ya uzoefu wa nguvu ya umoja. Hata hapo Bwana anarudia kusema kwetu “hamkeni na msiogope” Tutelemka katika uwanja na neema tuliyofanya uzoefu itusaidie kuwa mafundi wa kisinodi wa maisha ya kawaida katika jumuiya zetu. Baba Mtakatifu amebainisha kuwa Roho Mtakatifu atuongoze katika kufunga na Yesu, ili kufanya uzoefu wa kifahari wa Mungu na hivyo kwa kutiwa nguvu katika imani kumfuata pamoja na safari na Yesu utukufu kwa watu wake na mwanga wa watu, Baba Mtakatifu amehitimisha ujumbe wake wa Kwaresima 2023.

Ujumbe wa Papa kwa ajili ya Kwaresima 2023
17 February 2023, 11:30