Tafuta

Papa Francisko na Emmanuel Van Lierde,wakati wa mkutano na wahariri wa Toleo la Tertio la kila Juma la Ubelgiji,mnamo 2020. Papa Francisko na Emmanuel Van Lierde,wakati wa mkutano na wahariri wa Toleo la Tertio la kila Juma la Ubelgiji,mnamo 2020.  (� Vatican Media)

Papa:lazima kuwa na ujasiri wa kuota ndoto ya uchumi tofauti kwa ajili ya huduma ya wote

Tunachapisha baadhi ya ndondoo za mahojiano ya Gazeti la kila Juma la Ubergiji “Tertio”, yaliyochapishwa Februari 28.Katika mazungumzo.Papa anakabiliana na mada nyingi:kuanzia na Mtaguso II wa Vatican,hali ya sasa,mchakato wa kisinodi,vita nchini Ukraine hadi migogoro iliyosahauliwa ulimwenguni. Anawaalika kushirikiana katika mtindo wa kiuchumi Jumuishi.

Na Angella Rwezaula; - Vatican

Waandishi wa habari za gazeti la kila Juma la Ubeligiti liitwali “Tertio” walikuwa tayari amepata fursa ya kumuhoji kwa kirefu Papa Francisko mnamo tarehe 17 Novemba 2016. Sababu ya mahojiano hayo ilikuwa kwa upande mmoja fursa ya kumbukumbu ya  miaka  100 tangu kuibuka kwa Vita ya I ya Ulimwengu, na kwa kwa upande mwingine, kuhusiana mashambulizi ya kigaidi huko Paris, Ufaransa mnamo Novemba 2015 na mnamo tarehe  22 Machi 2016 huko Bruxelles. Miaka minne baadaye  imetokea fursa ya kuomba tena mahojiano, katika fursa nyingine ya kumbu kumbu ya miaka 10 ya Upapa wake ambayo inatafanyika mnamo tarehe 13 Machi 2023. Hapa tunakuletea ndondoo za mahojiano hayo kama ifuatavyo:

Mambo makuu ya kuelewa upapa wako ni Mtaguso wa II wa Vatican. Kwa nini mwendelezo wa sasa wa Mtaguso huo ulikuwa ndani ya moyoni mwako? Ni ni kitu gani kilichopo nyuma yake?

Wanahistoria husema kuwa inahitaji karne moja ili maamuzi ya Mtaguso kuweza kuwa na matokeo kamili na kuwekwa katika matendo. Sisi tunayo miaka 40 ya kuweza kufikia karne hiyo…. Mtaguso ulikuwa moja ya mambo yale ambayo Mungu hutimizwa katika historia kwa njia ya watu watakatifu. Labda Mtakatifu Yohane XXIII alipoanzisha mtaguso hip hakuna aliyezingatia ni kitu gani kingetokea.  Wanasema hata yeye mwenyewe alikuwa anafikiri ungeweza kuhitimishwa ndani ya mwezi mmoja, lakini Kardinali mmoja aliibuka na neno kwa kusema: “Unaanza kununua viti vyenye thamani na kila kitu kingine, kiitachukua miaka.” Papa Yohanne XXIII,  alizingatia hilo, kwani alikuwa ni mtu aliye wazi katika miito ya Bwana. Na ndivyo hivyo Mungu anazungumza kwa watu wake. Yeye pale alituzungamza kiukweli na sisi. Mtaguso haukupelekea mabadiliko ya Kanisa tu. Haukuwa ni masuala  ya upyaishwaji, tu lakini hata kuwa changamoto moja ya kufanya Kanisa liwe daima zaidi hai. Mtaguso haupyaishi, unalifanya Kanisa kuwa kijana.  Kanisa ni mama ambaye anakwenda mbele daima. Mtaguso ulifungua milango ya ukomavu mkuu, maelewano zaidi ya ishara za nyakati. Katika Lumen genitium (Lg) kwa mfano, katika ya Dogma kuhusu Kanisa,  ni moja  ya hati za kiutamaduni  zaidi na wakati huohuo za kisasa, kwa sababu katika muundo wa Kanisa, tamaduni, kama zinaeleweka vema daima ni za kisasa. Kwa hiyo ni kwa sababu tamaduni zinaendelea kuongezeka na kukua…

Mwendelezo wa sasa na wa kutimiza Mtaguso, unajumuisha katika kutia moyo mchakato wa Kisinodi. Je hii ina maana gani hasa?

Kuna jambo moja ambalo halitakiwi kutoa mtazamo wake. Katika hitimisho la Mtaguso, Papa Paulo VI alibaki ameshangazwa kuona kwamba Kanisa la Magharibi lilikuwa karibu limepoteza umuhimu wake wa kisinodi,  na wakati Makanisa Katoliki ya Mshariki, yalikuwa yametambua kuhifadhi. Kwa hiyo alitangaza kuunda Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu, kwa lengo la kuhamasisha kwa upya, Sinodi katika Kanisa. Katika mchakato wa safari ya miaka sitini, hali hiyo iliendelea kuongezeka zaidi. Pole pole baadhi ya mambo yaliweza kuweka wazi. Kwa mfano, ikiwa maaskofu walikuwa na haki ya kupiga kura tu. Mara kadha hilo halikuwa wazi na ikiwa wanawake wangeweza kupiga kura… Katika Sinodi iliyopita  kuhusu Amazonia, iliyofanyika mnamo 2019, kulikuwa na ukomavu katika maana hiyo… kwa sasa tuko hapa na tunapaswa kwenda mbele. Ndicho tunachofanya kwa njia ya mchakato wa sasa wa Kisinodi na Sinodi mbili juu ya mchakato huo itatusaidia kuweka wazi maana na mtindo wa mchakato wa maamuzi katika Kanisa. 

Katika mahojiano yaliyotangulia ya mnamo 2016, ulikuwa umetaja juu ya vita ya tatu ulimwenguni ambavyo tunaishi. Leo hii hali halisi haikuboreka katu na zaidi imekuwa mbaya ambapo bado kuna vita kama vile Ukraine.Diplomasia ya Vatican ina nafasi gani?

Vatican, imeweka ndani ya moyo  wake mgogoro huo tangu siku ya kwanza. Siku ya pili baada ya mwanzo wa uvamizi, nilikwenda mimi mwenyewe katika Ubalozi wa Urussi. Ni kitu ambacho hakikuwahi kufanywa kama Papa… Na nilielezea uwezekano wa utashi wangu wa kwenda Moscow, ili kufanya kwa namna kwamba mgogoro husiendelee. Tangu mwanzo hadi leo hii, Vatican daima imekuwa kitovu cha matendo. Baadhi ya Makardinali wamekwenda tarari Ukraine… Na wakati huo huo, siachi katu kuzungumza na watu wa Urussi ili wafanye chochote. Vita hivi havisemekani, ni vya ukatili mkubwa. Kuna wauaji huko wanaopigana. Baadhi ni wakatili sana, wakatili sana. Kuna mateso; ya watoto ambao wanateswa. Watoto wengi ambao wako Italia na mama zao, ambao wakikumbia walikuja kunitembelea. Sikuona mtoto wa Ukraine akicheka. Kwa sababu gani Watoto hao hawacheki? Ni nini waliona? Inatisha, inatisha kweli. Watu hao wanateseka, wanateseka kwa kuvamiwa. Ninawasiliana hata na baadhi ya wa Ukraine. Rais Volodymyr Zelensky, alituma wawakilishi kadhaa kuzungumza nami. Sisi hapa tunafanya kile kiwezekanacho kwa ajili ya kusaidia watu. Lakini mateso ni makubwa sana. Ninakumbuka kile walichokuwa wananiambia wazazi wangu: “Vita ni upuuzi”. Sisi tunahisi sana kuguswa katika ardhi hiyo kwa sababu vita inafanyika karibu na sisi.

Lakini ni kwa miaka sasa, kuna vita  ulimwenguni ambavyo hatuwekei maanani: huko Myanmar, Siria ambapo tayari ni miaka 13  ya vita, nchini Yemen, mahali ambapo watoto hawana elimu na wala mkate, wanateseka kwa njaaa…  Kwa kifupi, ulimwengu umetengenezwa daima na vita. Katika hili kuna jambo moja linalotakiwa kutangaza. Ni kuhusu kiwanda kikubwa cha kutengeneza silaha. Wakati Nchi Tajiri zinaanza kuwa dhaifu, wanasema kwamba zinahitaji vita ili kwenda mbele na kugeuka kuwa ya nguvu zaidi. Na silaha zinaandaliwa kwa ajili hiyo. Katika Nchi zetu, kwa ukleri ambao unapungua, na waamini wachache, uongozi wa Kanisa, unatabia ya kusisitiza juu ya liturujia na tangazao. Je Kanisa halipaswi kujionesha zaidi sura yake ya kijamii na kinabii ikiwa linataka kuonekana zaidi leo hii?

Havipingani. Sala, kuabudu na ibada sio kujiunda ndani ya Sakrestia. Ni mambo ambayo hayapingani. Kanisa ambalo haliadhimishi Ekaristi sio Kanisa. Lakini pia sio Kanisa ambalo linajificha katika Sakrestia. Kujiweka vizuri katika Sakrestia sio ibada sahihi. Maadhimisho ya Ekaristi, yana matokeo yake. Kuna kipande cha mkate. Hii inamaanisha wajibu wa kijamii na wajibu wa kuwajali wengine. Sala na juhudi za matendo vinakwenda njia moja. Kuabudu Mungu na huduma kwa kaka na dada zetu, ni mambo yanayokwenda sambamba, kwa sababu kila kaka na dada tunamuona Yesu.

Mfumo wa soko la uliberali mamboleo umefikia kikomo.Ni kwa namna gani ‘Uchumi wa Francisko’ unaweza kutoa mbadala?

Lazima kuwa na ujasiri wa kuota ndoto za uchumi ambazo si huria kabisa…Hii inahitaji kuwa na busara kwa uchumi, kwani ikiwa inajikita ndani sana juu ya fedha peke yake, na takwimu  za tarakimu tu ambazo hazina vyombo vya kweli nyuma yake, basi uchumi unaporomoka na unaweza kusababisha usaliti mkubwa. Kwa hiyo uchumi lazima uwe uchumi kijamii. Kielelezo  cha chumi wa soko, kwa mujibu wa Papa Yohane Paulo II aliongeza,  ‘Kijamii’, kwa hiyo uchumi wa kijamii wa soko. Ni lazima kulizingatia akilini suala la kijamii. Katika wakati huu wa mgogoro wa kiuchumi, ni kuna mashaka ya safu za migogoro ambazo hazielezeki. Sehemu kubwa ya watu ulimwenguni hawana chakula cha kutosha, hawana mahali pa kutosha kuishi. Utajiri huko kwenye mikono ya watu wachache ambao wanaendesha makampuni makubwa, na ambayo wakati mwingine ni nyenye tabia ya kunyonya. Uchumi daima lazima uwe wa kijamii na katika huduma ya kijamii.

Mahojiano ya Papa katika Gazeti la Kila Juma Tertio la Ubelgiji
28 February 2023, 15:39